Leo tuikumbuke World Cup ya 2010 pale South Africa

Leo tuikumbuke World Cup ya 2010 pale South Africa

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Ilikuwa ni michuano ya kwanza kabisa kufanyika Afrika. Lakini ni michuano iliyoacha historia kubwa sana kwa wapenzi wapenda kandanda ulimwenguni kote.

Mpira ulipigwa kwelikweli, nakumbuka ule mpira wa michuano uliotengenezwa na kampuni ya Adidas ukijulikana kama Jabulani.

Mavuvuzela pia yalikuwa ni sehemu ya kivutio cha michuano ile japo mabeberu hawakuyapenda kabisa.

Mechi ambayo siwezi kuisahau ni robo fainali ya England Vs Germany, ambapo Frank Lampard alipiga mkwaju ukagonga mwamba wa ju ukaingia halafu mpira ukatoka, refa akasema sio goli mpira uendelee.

Waingereza wakaishia kutolewa, wakalalamika kila sehemu na matokeo yake FIFA ikaleta Goal line technology kwenye michuano ya mwaka 2014.

Mchezaji ambaye nilimkubali sana ni Diego Forlan jinsi alivyojulia kupiga mashuti kwa mpira wa Jabulani kiasi cha kubatizwa "Master of Jabulani"

Kikubwa zilikuwa ni fainali za aina za pekee sana na zitabaki daima katika mioyo yetu sisi Waafrika.

Unakumbuka tukio gani, goli gani, mechi gani katika fainalibza kombe la dunia za mwaka 2010 pale bondeni kwa madiba
 
Nimekumbuka mechi ya ufumbuzi kati ya south na mexico nimekumbuka mechi ya robo fainali kati ya Netherlands na Brazil wisley sjinder kweny ubora wake alimaliza hii game nakumbka mechi ya Portugal na Ivory coast kweny group stage yan matukio. Ni mengi
Mkuu game ya ufunguz ilikuwa SA vs Uruguay
 
Ilikuwa inamvuto wa kipekee ,nakumbuka rafu ya Nigel de Jong aliyo mchezea Alonso nilikuwa naipiga kwenye chandimu ikiaanza mida ya vurugu mechi
De-Jong-Alonso-Foul-Holland-Spain-World-Cup-F_2476492(1).jpg
 
Back
Top Bottom