Leo zamu ya wadada wa JamiiForums kutongoza wakaka wa humu! Tuone vocal zenu

Leo zamu ya wadada wa JamiiForums kutongoza wakaka wa humu! Tuone vocal zenu

Mm naona mwisho kukudharau tu Bora unyamaze tu ukute mkaka ambae anashobokewa na wadada na wew ukianza anakuweka kwenye kundilile lile japo inawezekana unapenda kweli
🤣🤣🤣🤣🤣 mimi nina staha siwezi fika huko
 
Sa unashindwa Nini luckyline halafu ukute hata yeye anawaza akuanze vipi.
Toa neno moja tu au fanya kitu kimoja Cha kumfanya awaze (kwani huyu dada ananionaje Mimi) Kisha yeye (kama ni mwanaume kamili) atamalizia.
Sina huo ubavu. Wacha iwe hivyo kimya kimya.nina aibu sana sijawahi kufanyagabhayo mambo
 
Sina huo ubavu. Wacha iwe hivyo kimya kimya.nina aibu sana sijawahi kufanyagabhayo mambo
Utapoteza nafasi uje kujilaumu. Ila nahisi bado Kuna upande wako haujamkubali. La sivyo aibu ungeziweka pembeni, ungetafuta namna ya kumfikishia ujumbe.
 
Enwei, ngoja nijaribu..!!

Kila nikiiona comment yako mahali hapa naishia kutabasamu, sababu zaidi ya yote huwa ninaona kujiamini kwako ndani yake, cha kushangaza ni kuwa mapigo ya moyo wangu hubadilika na kudunda kwa kasi nilionapo tu jina lako, hujikuta natabasamu na kucheka hata kwa vitu vidogo vitokavyo kwako na visivyo na maana kabisa,

Lengo hasa la kuyaandika yote haya ni kutaka kukueleza ni jinsi gani wautesa mtima wangu, ninahisi kuvutiwa na kila kitu kuhusu wewe, hata avatar isiyo yako halisi inanifanya niachie tabasamu mwanana,

Natamani niendelee kukuonesha ni namna gani nimebarikiwa kukutana na wewe mahala hapa, ila hapana muda si rafiki sana upande wetu, hivyo naomba tafadhali uubariki moyo wangu kwa kunikubalia niwe wako, niamini Mimi, kunikubali ni kati ya maamuzi machache hutokaa ujutie kuyafanya kamwe, ...... please be mine..!

(Huku nakutazama machoni kwa macho ya maqhaba, ukichomoa niite andazi niko nimekaa pale)

Nyie 😍 ngoja nifikirie 😀
 
Back
Top Bottom