TANZIA Leopold Kweyamba Lwajabe amekutwa amefariki Mkuranga baada ya kupotea wiki iliyopita

Hapa lazima kuna jambo linafukuta chini kwa chini. Ni kwanini atekwe wakati huu wa kuelekea uchaguzi....muda ambao pesa nyingi huchotwa ovyo kutoka BoT na kuelekezwa kwenye siasa? Kagoma kutoa fedha au nini? Yajayo yanasikitisha.
 
mzee kangi kasema hakuna kutangaza habari za uongo uongo za kutekwa watu.wengine uwa wanajiteka Na kujiua
 
Kabla ya awamu hii kumaliza ngwe yake, sijui kuna mtu atakuwa amebakia juu ya ardhi hii ya Tanzania!! Watakuwa wamebaki wanyama tu ndani ya CHATO national park na kwingineko.
Hii hali inatisha!

Hakuna mtu aliye salama tena, chini ya utawala huu wa awamu ya tano
 
Mmmhh jamaniii..... Pole kwa wote mlioguswa na msiba huu apumzike kwa amani
 
Kwani marehemu alikuwa mwanasiasa???
Awamu hii kama una mishe zako zinazokuingizia kipato ni vyema ukatulia, Mambo ya kujiingiza katika siasa mwisho wake ndio kama huu...

Kama huwezi kuisifia ni vyema ukaacha kujihusisha na siasa...

Apumzike kwa amani.
 
Maskini nchi yangu , na wanyonge ndio sisi tupigwe, watuteke , watuue, tudhulumiwe haki zetu , elimu za watoto wetu ndio tia maji maji.

Lakini hatuishi kupiga vigeregere kwa namba moja na sifa kedekede kuwa ndio mtetetezi wa wanyonge
 
Hawa wauaji huemda wanataka wawaue raia wote wabaki wajitawale wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…