TANZIA Leopold Kweyamba Lwajabe amekutwa amefariki Mkuranga baada ya kupotea wiki iliyopita

Watu kuuliwa ni kawaida duniani kote hata huko Ulaya watu wanauliwa, Marekani kila dakika moja wanauwawa watu hamsini"- Cyprian Musiba(Dw Interview, Saturday 27. July, 2019.

The future is not so bright
Baada ya kuisikia hii nimeapa sitagusa Marekani.
 
Mara mkuranga umekutwa mwili, mara alirudishwa kwa kinyerezi akadai alichanganyikiwa! so which is which? au umechanganyikiwa wewe mleta habari? Ukiwa mwongo usiwe msahaulifu
 
Dar es Salaam. Mkurugenzi msaidizi wa miradi inayotekelezwa na Umoja wa Ulaya nchini kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, Leopold Lwajabe amekutwa amekufa wilayani Mkuranga.
Taarifa za zilizotolewa na msemaji wa wizara hiyo, Benny Mwaipaja zimesema wamejiridhisha kuhusu kifo hicho, muda mfupi wakijiandaa kutoa taarifa ya kumtafuta.
“Alitoweka wakati fulani wiki iliyopita lakini akaonekana. Ilikuwa ni muda mfupi baada ya kurejea nyumbani kwake kutoka kazini. Alipoonekana alitakiwa kwenda kutoa maelezo polisi lakini kabla hajafanya hivyo, akapotea tena. Leo ilikuwa tutoe taarifa kwa vyombo vya habari kumtafuta,” amesema Mwaipaja.
Mkwaipaja amesema walisitisha kutoa taarifa hiyo baada ya kupokea fununu za mwili wake kuonekana huko Mkuranga hivyo wakatuma watu kwenda kujiridhisha na kukuta ni kweli. Kifo hicho kimethibitishwa leo, Julai 29.
 
Duh labda waliomteka walimpa options na fursa ya kuaga familia na kumalizia viporo kazini
 
Ni bora kujitanguliza kabla ya kubambikwa kesi ya uhujumu uchumi... Mungu amrehemu marehemu wetu!
 
Pengine alipotekwa mara ya kwanza angesema yaliyomkuta huko ambayo labda alionywa asiyaongee(akaishia kusema alichanganyikiwa) ingesaidia kidogo usalama wake au pangepatikana pa kuanzia kuwapata wahusika.
Sijui ugumu unatoka wapi kusema yaliyowakuta watekwaji!Inaweza kuwa wanakutana na mazito zaidi ya tunayoyafikiria labda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…