TANZIA Leopold Kweyamba Lwajabe amekutwa amefariki Mkuranga baada ya kupotea wiki iliyopita

Wangemteka Musiba na Bashite tusikie tafrani yake itakuwaje?!
Musiba kawaonya wanaotaka kufanya hivyo kwae akina january na Zitto kuwa watajikuta matako yao yamekuwa makubwa na midomo imepakwa lipstick [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nguvu kutoka juu, imeasisi na kubariki utekaji nchi hii. Shime watanzania tuseme hapana ili nguvu hii toka juu ikome kueneza kansa hii.

Leo kwa mwingine, kesho kwako.
unamaanisha Mungu au?
 
Watu kuuliwa ni kawaida duniani kote hata huko Ulaya watu wanauliwa, Marekani kila dakika moja wanauwawa watu hamsini"- Cyprian Musiba(Dw Interview, Saturday 27. July, 2019.

The future is not so bright
dk 1 = watu 50
saa 1 = watu 3,000
siku 1 = watu 72,000
wiki 1 = watu 504,000
mwaka 1 = watu 26,208,000

hivi hiyo "marekani" bado kweli kuna watu hai hadi leo au ni makaburi tu yamebaki?
 
Wakuu, Habari zilitufikia hivi punde ni kwamba aliyekua mkuu wa Kitengo cha EU, Wizara ya Fedha Leopord Lwajabe Amekutwa Amefariki huko Mkuranga.

Lwajabe alitekwa na watu wasiojulikana Akiwa ofisini kwake baada ya kupigiwa simu Stoke nje ya Ofisi, Walimshikilia kwa siku 3 kisha kumutelekeza Nyumbani kwake Kinyerezi,Tabata. Baada ya ndugu na majirani kumuhoji alidai alichanganyikiwa tu.

Juzi alhamisi wiki iliyopita alitekwa tena na baada ya ndugu kutoa taarifa Polisi walisema wasubiri baada ya SAA 72, Leo hii Asubuhi mwili wake Amekutwa akining'inia huko Mkuranga.

Taarifa zaidi zinakuja
======

Mkurugenzi msaidizi wa miradi inayotekelezwa na Umoja wa Ulaya nchini kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, Leopold Lwajabe amekutwa amekufa wilayani Mkuranga.

Taarifa za zilizotolewa na msemaji wa wizara hiyo, Benny Mwaipaja zimesema wamejiridhisha kuhusu kifo hicho, muda mfupi wakijiandaa kutoa taarifa ya kumtafuta.

“Alitoweka wakati fulani wiki iliyopita lakini akaonekana. Ilikuwa ni muda mfupi baada ya kurejea nyumbani kwake kutoka kazini. Alipoonekana alitakiwa kwenda kutoa maelezo polisi lakini kabla hajafanya hivyo, akapotea tena. Leo ilikuwa tutoe taarifa kwa vyombo vya habari kumtafuta,” amesema Mwaipaja.

Mkwaipaja amesema walisitisha kutoa taarifa hiyo baada ya kupokea fununu za mwili wake kuonekana huko Mkuranga hivyo wakatuma watu kwenda kujiridhisha na kukuta ni kweli.

Kifo hicho kimethibitishwa leo, Julai 29.
Hii ni hatari sana kwa ustawi wa taifa letu.
 
Inasikitisha sana
Ila hakuna kisicho na mwisho.
MOLA WETU MLEZI ni muadilifu sana, kuumba UMAUTI?
YANADHIBITIWA HAYA NA ALLAH NI HAKIMU MUADILIFU ,HAMDHULUMU YEYOTE watayakuta haya wayafanyayo, na watauma vidole kwa majuto ha hayatawasaidia lolote.

WAFIWA POLENI MSITIRINI NDG YENU NA KUWENI NA SUBRA,
 
Poleni wafiwa.
Amani nchi hii inazidi kumongonyo kwa kasi.
Mungu Baba tuepushe na dhahama hii!!
 
Wakuu, Habari zilitufikia hivi punde ni kwamba aliyekua mkuu wa Kitengo cha EU, Wizara ya Fedha Leopord Lwajabe Amekutwa Amefariki huko Mkuranga.

Lwajabe alitekwa na watu wasiojulikana Akiwa ofisini kwake baada ya kupigiwa simu Stoke nje ya Ofisi, Walimshikilia kwa siku 3 kisha kumutelekeza Nyumbani kwake Kinyerezi,Tabata. Baada ya ndugu na majirani kumuhoji alidai alichanganyikiwa tu.

Juzi alhamisi wiki iliyopita alitekwa tena na baada ya ndugu kutoa taarifa Polisi walisema wasubiri baada ya SAA 72, Leo hii Asubuhi mwili wake Amekutwa akining'inia huko Mkuranga.

Taarifa zaidi zinakuja
======

Mkurugenzi msaidizi wa miradi inayotekelezwa na Umoja wa Ulaya nchini kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, Leopold Lwajabe amekutwa amekufa wilayani Mkuranga.

Taarifa za zilizotolewa na msemaji wa wizara hiyo, Benny Mwaipaja zimesema wamejiridhisha kuhusu kifo hicho, muda mfupi wakijiandaa kutoa taarifa ya kumtafuta.

“Alitoweka wakati fulani wiki iliyopita lakini akaonekana. Ilikuwa ni muda mfupi baada ya kurejea nyumbani kwake kutoka kazini. Alipoonekana alitakiwa kwenda kutoa maelezo polisi lakini kabla hajafanya hivyo, akapotea tena. Leo ilikuwa tutoe taarifa kwa vyombo vya habari kumtafuta,” amesema Mwaipaja.

Mkwaipaja amesema walisitisha kutoa taarifa hiyo baada ya kupokea fununu za mwili wake kuonekana huko Mkuranga hivyo wakatuma watu kwenda kujiridhisha na kukuta ni kweli.

Kifo hicho kimethibitishwa leo, Julai 29.

Alichanganyikiwa kwa mara ya pili ndiyo akajinyonga au? aliwahi kuwa na tatizo la akili hapo awali au?

Pole sana kwa wanafamilia hasa mke na watoto.maana sijui sasa ukurasa gani wa maisha utakuwa unafunguka kwao.Mungu awasaidie so sad kwa kweli
 
Hakuna lenye mwanzo likakosa mwisho, tunasubiria 2020 tuone yatakayojiri
 
Familia fungeni novena na mtoe sadaka kama ni wakristo

kama ni Muslims nendeni Pemba Tumbatu mkasome Albdili ya kumshtakia mwenyezi mungu ili kila alieusika na kifo cha mpendwa wenu kwa kutoa order , kwa kushiriki mahuaji apate hukumu anayostaili
 
Back
Top Bottom