Wakuu, Habari zilitufikia hivi punde ni kwamba aliyekua mkuu wa Kitengo cha EU, Wizara ya Fedha Leopord Lwajabe Amekutwa Amefariki huko Mkuranga.
Lwajabe alitekwa na watu wasiojulikana Akiwa ofisini kwake baada ya kupigiwa simu Stoke nje ya Ofisi, Walimshikilia kwa siku 3 kisha kumutelekeza Nyumbani kwake Kinyerezi,Tabata. Baada ya ndugu na majirani kumuhoji alidai alichanganyikiwa tu.
Juzi alhamisi wiki iliyopita alitekwa tena na baada ya ndugu kutoa taarifa Polisi walisema wasubiri baada ya SAA 72, Leo hii Asubuhi mwili wake Amekutwa akining'inia huko Mkuranga.
Taarifa zaidi zinakuja
======
Mkurugenzi msaidizi wa miradi inayotekelezwa na Umoja wa Ulaya nchini kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, Leopold Lwajabe amekutwa amekufa wilayani Mkuranga.
Taarifa za zilizotolewa na msemaji wa wizara hiyo, Benny Mwaipaja zimesema wamejiridhisha kuhusu kifo hicho, muda mfupi wakijiandaa kutoa taarifa ya kumtafuta.
“Alitoweka wakati fulani wiki iliyopita lakini akaonekana. Ilikuwa ni muda mfupi baada ya kurejea nyumbani kwake kutoka kazini. Alipoonekana alitakiwa kwenda kutoa maelezo polisi lakini kabla hajafanya hivyo, akapotea tena. Leo ilikuwa tutoe taarifa kwa vyombo vya habari kumtafuta,” amesema Mwaipaja.
Mkwaipaja amesema walisitisha kutoa taarifa hiyo baada ya kupokea fununu za mwili wake kuonekana huko Mkuranga hivyo wakatuma watu kwenda kujiridhisha na kukuta ni kweli.
Kifo hicho kimethibitishwa leo, Julai 29.