TANZIA Leopold Kweyamba Lwajabe amekutwa amefariki Mkuranga baada ya kupotea wiki iliyopita

Nguvu kutoka juu, imeasisi na kubariki utekaji nchi hii. Shime watanzania tuseme hapana ili nguvu hii toka juu ikome kueneza kansa hii.

Leo kwa mwingine, kesho kwako.
Inabidi tukemee matukio na namna hii ya watu kutekwa kisha kupotea kabisa au kuuawa.

Lakini itabidi tusipende kutumia hisia katika masuala mazito ya namna hii.....kama hauna uhakika na muuaji ni vizuri ukakemea mauaji na sio kumshutumu mtu au watu Fulani moja kwa moja.

Usilolijia ni sawa na usiku wa giza.

Serikali itabeba lawama kila siku maana matukio yamekuwa ys mfululizo na hatua hazichujukiwi kama inavyotakiwa.
 
*MKURUGENZI Msaidizi wa miradi katika wizara ya fedha na mipango, Mhandisi Leopold Lwajabe (56), ameripotiwa kufariki dunia katika mazingira ya kutatanisha.*

Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Kigogo huyo mwandamizi katika wizara ya fedha, mwili wake umekutwa umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali ya wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani.
“Niko hapa hospitali ya Mkuranga mkoani Pwani. Nimeona mwili wa ndugu yangu Leopald Kweyamba Lwajebe, ukiwa umehifadhiwa katika chumba cha maiti,” ameeleza Mugisha Bagoka Brassio, ndugu wa Mhandisi Lwajabe.
Anasema, “tumeambia na viongozi wa hospitali hii, kwamba mwili wa ndugu yetu uliletwa hapa hospitali na askari poli. Uchunguzi wa polisi unaonyesha kuwa kifo chake kimetokana na kunyongwa shingo yake kwa kutumia kamba.”
Kwa mujibu wa Brassio, polisi wamemueleza kuwa mwili wa kaka yake huyo waliukuta kwenye kichaka ukiwa unaning’inia, huku shingo ikiwa imefungwa kamba.
Mhandishi Lwajabe alitoweka ofisini kwake, Alhamisi ya tarehe 25 Julai mwaka huu, baada ya kuwaaga wafanyakazi wenzake, kwamba anatakiwa kuripoti kituo cha Polisi cha Mburahati, kwa ajili ya mahojiano juu ya tuhuma zilizokuwa zinamkabili.
MwanaHALISI ONLINE halijaweza kufahamu, Mhandisi Lwajabe alikuwa anakabiliwa na tuhuma gani.
Mhandisi Lwajabe, kwa muda mrefu amekuwa mfanyakazi katika wizara ya fedha na mipango, akisimamia Idara ya fedha za Nje, kitengo cha mfuko wa maendeleo wa umoja wa Ulaya (EU).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mugisha Bagoka Brassio, ni kwamba kaka yake huyo alianza kupata misukosuko siku 10 zilizopita, baada ya kuhojiwa na polisi kwa masuala ambayo hakuyataja.
Anasema, “Jumanne ya tarehe 16 Julai 2019, majira ya saa tatu asubuhi, Mhandisi Lwajabe aliaga ofisini kwake, kwamba anakwenda kuonana na mtu aliyempigia simu. Hakurejea tena ofisini kwake.”
Anasema, kwa sababu ndugu yao hakurejea nyumbani, familia iliamua kutoa taarifa kesho yake, tarehe 17 Julai 2019 katika Kituo cha Polisi cha Kati, jijini Dar es Salaam na walifanikiwa kufungua jarada la uchunguzi lenye Na. CD/RB/4122/2019.
Mwanandugu huyo anasema, jeshi la polisi liliwambia kuwa watulie na Polisi watafanya jitihada za kumtafuta na ikiwa hajarejea nyumbani baada ya saa 72, warudi tena kuripoti kituoni hapo.
Badala yake, Brassio anasema, “siku iliyofuata, watu wasiojulikana walimrudisha Lwajabe kwa gari na kumshusha nyumbani kwake, alfajiri ya Ijumaa, tarehe 18 Julai 2019.”
Taarifa zinasema, Mhandisi Lwajabe alinukuliwa akiwambia wanafamilia yake – kabla ya kufikwa na mauti – kwamba ameelekezwa na watu waliokuwa naye kuripoti kwenye kituo cha Polisi cha Mburahati kwa mahojiano zaidi.
“Tumefanya jitihada mbalimbali kumtafuta mpendwa wetu ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa polisi Kituo cha Kati (Central Police Station), lakini hakuna tulichoambulia,” ameeleza Brassio.
Mhandisi Lwajabe anaingia katika orodha ya watu wanaodaiwa kutekwa na baadaye kupotezwa nchini na wanaoitwa na serikali, “watu wasiojulikana.”
Mhandisi Leopold Kweyamba Lwajabe, amezaliwa katika kijiji cha Ihembe, kata ya Ihembe, wilayani Karagwe, mkoani Kagera. Ameacha mke na mtoto mmoja anayefahamika kwa jina la Doreen Leopald Lwajabe.
 
Very sad.
Tuwe na subra maana kila safari in mwisho wake.
Mzee ruksa aliwahi kusema kila zama na kitabu chake.
 
Wakuu, Habari zilitufikia hivi punde ni kwamba aliyekua mkuu wa Kitengo cha EU, Wizara ya Fedha Leopord Lwajabe Amekutwa Amefariki huko Mkuranga.

Lwajabe alitekwa na watu wasiojulikana Akiwa ofisini kwake baada ya kupigiwa simu Stoke nje ya Ofisi, Walimshikilia kwa siku 3 kisha kumutelekeza Nyumbani kwake Kinyerezi,Tabata. Baada ya ndugu na majirani kumuhoji alidai alichanganyikiwa tu.

Juzi alhamisi wiki iliyopita alitekwa tena na baada ya ndugu kutoa taarifa Polisi walisema wasubiri baada ya SAA 72, Leo hii Asubuhi mwili wake Amekutwa akining'inia huko Mkuranga.

Taarifa zaidi zinakuja
======

Mkurugenzi msaidizi wa miradi inayotekelezwa na Umoja wa Ulaya nchini kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, Leopold Lwajabe amekutwa amekufa wilayani Mkuranga.

Taarifa za zilizotolewa na msemaji wa wizara hiyo, Benny Mwaipaja zimesema wamejiridhisha kuhusu kifo hicho, muda mfupi wakijiandaa kutoa taarifa ya kumtafuta.

“Alitoweka wakati fulani wiki iliyopita lakini akaonekana. Ilikuwa ni muda mfupi baada ya kurejea nyumbani kwake kutoka kazini. Alipoonekana alitakiwa kwenda kutoa maelezo polisi lakini kabla hajafanya hivyo, akapotea tena. Leo ilikuwa tutoe taarifa kwa vyombo vya habari kumtafuta,” amesema Mwaipaja.

Mkwaipaja amesema walisitisha kutoa taarifa hiyo baada ya kupokea fununu za mwili wake kuonekana huko Mkuranga hivyo wakatuma watu kwenda kujiridhisha na kukuta ni kweli.

Kifo hicho kimethibitishwa leo, Julai 29.

Zaidi soma...

*MKURUGENZI Msaidizi wa miradi katika wizara ya fedha na mipango, Mhandisi Leopold Lwajabe (56), ameripotiwa kufariki dunia katika mazingira ya kutatanisha.*

Kigogo huyo mwandamizi katika wizara ya fedha, mwili wake umekutwa umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali ya wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani.

“Niko hapa hospitali ya Mkuranga mkoani Pwani. Nimeona mwili wa ndugu yangu Leopald Kweyamba Lwajebe, ukiwa umehifadhiwa katika chumba cha maiti,” ameeleza Mugisha Bagoka Brassio, ndugu wa Mhandisi Lwajabe.

Anasema, “tumeambia na viongozi wa hospitali hii, kwamba mwili wa ndugu yetu uliletwa hapa hospitali na askari poli. Uchunguzi wa polisi unaonyesha kuwa kifo chake kimetokana na kunyongwa shingo yake kwa kutumia kamba.”
Kwa mujibu wa Brassio, polisi wamemueleza kuwa mwili wa kaka yake huyo waliukuta kwenye kichaka ukiwa unaning’inia, huku shingo ikiwa imefungwa kamba.

Mhandishi Lwajabe alitoweka ofisini kwake, Alhamisi ya tarehe 25 Julai mwaka huu, baada ya kuwaaga wafanyakazi wenzake, kwamba anatakiwa kuripoti kituo cha Polisi cha Mburahati, kwa ajili ya mahojiano juu ya tuhuma zilizokuwa zinamkabili.
MwanaHALISI ONLINE halijaweza kufahamu, Mhandisi Lwajabe alikuwa anakabiliwa na tuhuma gani.

Mhandisi Lwajabe, kwa muda mrefu amekuwa mfanyakazi katika wizara ya fedha na mipango, akisimamia Idara ya fedha za Nje, kitengo cha mfuko wa maendeleo wa umoja wa Ulaya (EU).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mugisha Bagoka Brassio, ni kwamba kaka yake huyo alianza kupata misukosuko siku 10 zilizopita, baada ya kuhojiwa na polisi kwa masuala ambayo hakuyataja.

Anasema, “Jumanne ya tarehe 16 Julai 2019, majira ya saa tatu asubuhi, Mhandisi Lwajabe aliaga ofisini kwake, kwamba anakwenda kuonana na mtu aliyempigia simu. Hakurejea tena ofisini kwake.”

Anasema, kwa sababu ndugu yao hakurejea nyumbani, familia iliamua kutoa taarifa kesho yake, tarehe 17 Julai 2019 katika Kituo cha Polisi cha Kati, jijini Dar es Salaam na walifanikiwa kufungua jarada la uchunguzi lenye Na. CD/RB/4122/2019.

Mwanandugu huyo anasema, jeshi la polisi liliwambia kuwa watulie na Polisi watafanya jitihada za kumtafuta na ikiwa hajarejea nyumbani baada ya saa 72, warudi tena kuripoti kituoni hapo.
Badala yake, Brassio anasema, “siku iliyofuata, watu wasiojulikana walimrudisha Lwajabe kwa gari na kumshusha nyumbani kwake, alfajiri ya Ijumaa, tarehe 18 Julai 2019.”

Taarifa zinasema, Mhandisi Lwajabe alinukuliwa akiwambia wanafamilia yake – kabla ya kufikwa na mauti – kwamba ameelekezwa na watu waliokuwa naye kuripoti kwenye kituo cha Polisi cha Mburahati kwa mahojiano zaidi

“Tumefanya jitihada mbalimbali kumtafuta mpendwa wetu ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa polisi Kituo cha Kati (Central Police Station), lakini hakuna tulichoambulia,” ameeleza Brassio.

Mhandisi Lwajabe anaingia katika orodha ya watu wanaodaiwa kutekwa na baadaye kupotezwa nchini na wanaoitwa na serikali, “watu wasiojulikana.”

Mhandisi Leopold Kweyamba Lwajabe, amezaliwa katika kijiji cha Ihembe, kata ya Ihembe, wilayani Karagwe, mkoani Kagera. Ameacha mke na mtoto mmoja anayefahamika kwa jina la Doreen Leopald Lwajabe.
Anasimamia kitengo cha EU umoja wa ulaya,tena si huko ulaya ambapo tunaambiwa "kuna mabeberu" wasiotutakia wema kwenye kujenga uchumi wetu!?Huyu atakuwa amehisiwa au amekuwa anavujisha siri za Nchi kwa mabeberu,wazee wa secret service AKA wasiojurikana wamefanya yao!
 
Haya mambo yameshamiri kipindi ambacho anapata opposition kidogo kutoka chama chake! Ile ngwe nyingine akipita tuhesabu maumivu zaidi ya hapa. 2020 tusipepese macho jamani. Lazima tubadili hii hali.
 
Familia fungeni novena na mtoe sadaka kama ni wakristo

kama ni Muslims nendeni Pemba Tumbatu mkasome Albdili ya kumshtakia mwenyezi mungu ili kila alieusika na kifo cha mpendwa wenu kwa kutoa order , kwa kushiriki mahuaji apate hukumu anayostaili

Kama wanapita humu naomba hii comment wasiichukulie mzaha mzaha.
 
..................Inasikitisha!!!Mungu amlaze mahala pema,ni njia yetu sote siyo mwenye mamlaka siyo tajiri siyo “WASIOJULIKANA” wote sisi kwa wakati wetu tutaipitia hii scene.

Mbele ya kifo...akuna aliye salama.
 
EU kitengo cha nini, ayo matukio ya vifo na kutekwa inabidi yaolozeshwe, kuna siku yatatumika ICC KAMA ushahidi, jinai haina ukomo,, iko siku yatamgharimu mtu, ni suala la muda tu kwakweli, inasikitisha jamani
Hakika kuna siku yatagharimu Mtu na nyumbu wake _mda ni hakimu
 
Back
Top Bottom