A
Kwamba vichwa vinavyopelekeshwa na mapenzi ni makini kuliko vichwa vyenye uzoefu na maisha?
Weka takwimu za ajali kwa kigezo cha umri,uone vijana watakavyo kuamgusha.
Kwa upande wangu ningeangalia ubora wa miundo mbinu(barabara),na upatikanaji vipuli kwa bei nzuri ingeokoa maisha ya wengi.
Duh mnakabia juu wazee...πππKuna report yeyote ile inayoonyesha kua wazee ndio chanzo cha ajali nyingi Barabarani?
Tuna utulivu mkuu, vijana na subaru zao wakiwa nyuma ya wazee na Toyota Gaia zao wanaona ni washamba fulani hivi wasiojua maisha ni nini wanaovateki tu hata pasiporuhusu.Duh mnakabia juu wazee...πππ
Bila picha huyo dingi aliyeshindwa kuendesha chombo huo unabaki kuwa UMBEA.Nina wasiwasi kuhusu mfumo wa utoaji wa leseni za udereva, ambao unaonekana kutokuwa na ukomo wa umri wa mtu kuendelea kuendesha gari.
Kuna baadhi ya wazee ambao umri wao umeenda sana, pamoja na watu wenye changamoto za kiafya au ulemavu, lakini bado wanapewa au kuendelea kutumia leseni za udereva bila tathmini ya mara kwa mara ya uwezo wao wa kuendesha kwa usalama.
Kwa mtazamo wangu, suala hili linapaswa kuangaliwa kwa umakini kwa sababu usalama barabarani unapaswa kuwa kipaumbele. Kadri umri unavyoongezeka, baadhi ya uwezo muhimu kwa dereva kama kuona, kusikia, umakini na mwitikio wa haraka unaweza kupungua. Ikiwa dereva hana uwezo unaohitajika, anaweza kuhatarisha maisha yake na ya watumiaji wengine wa barabara.
Nashauri kuwe na ukomo au utaratibu maalum wa kufanya tathmini za afya na uwezo wa kuendesha kulingana na umri, badala ya leseni kuendelea kutumika bila kuangalia mabadiliko ya uwezo wa dereva. Hii inaweza kusaidia kupunguza ajali na kuhakikisha wanaopewa leseni wana uwezo wa kuendesha magari kwa usalama.