Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muungano


Mkuu Mkandara

Kwa mchango huu umeonesha kuwa unaweza kufanya uchambuzi na upembuzi. Nilifikiri kuwa mwanzoni unaona moves za UAMSHO (wa-zanzibar)ni za kidini na ubaguzi. Wengine na nyimbo yao "usultani, upemba, unguja, mwalabu, gozi"

Sasa kwa uchambuzi huu unaonesha kuwa Wazanzibar wanatizama maslahi yao kinchi, na sisi wengi wetu hapa JF tunakoleza udini tu na chuki miongoni mwa watanzania.

Tokea ilipofufuliwa EAC kama tungefuata ushauri wa mwanzilishi wa Muungano mwenyewe,hakuna UAMSHO au nani angepata mwanya kuparaganya udugu,uhusiano na mshikamano wa Tanzania (Tanganyika na Zanzibar).

Mwalimu alitoa rai kuwa itakapoanzishwa tena jumuiya ya Afrika Mashariki basi Tanzania iwe na serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar.

(
"Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Masharikizikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili- ya Zanzibar na ya Tanganyika ..." Uk 11 .link ya kitabu hii )

Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)

Tanzania ingekuwa na sauti kubwa katika EAC kwa uwepo wa Tanganyika na Zanzibar kama serikali zanazojitegemea. Wabunge 9 kila mwanachama,ingefanya 18 kwa Tanzania. Influencial voting block.

Kitafute kijarida cha shirikisho ndani ya shirikisho ukipitie kwa utuo.


 

Mkandara,

..wa-Zanzibari wanataka "mkataba" na wa-Tanganyika kabla ya kwenda huko kwenye EAC, au SADC.

..wanajua tukikutana kwenye EAC basi Mzanzibari atakuwa sawa na Mkenya,au Mganda, anapokanyaga ardhi ya Tanganyika.

..wakati wa kampeni Maalim Seif aliulizwa kama akipewa madaraka atapendekeza Zanzibar iwe na Central Bank na sarafu yao wenyewe akakataa.

..ukichunguza utaona kwamba wa-Zanzibari wanataka na dola yao lakini wakati huohuo wanataka kuendelea kutunyonya wa-Tanganyika. Ndiyo maana unasikia mapendekezo ya kuwa na "muungano wa mkataba."

..napenda kuwaonya wa-Tanganyika kwamba tusikubali mkataba wa aina yoyote ile na Zanzibar bila kushirikisha mataifa mengine.
 
Nonda Pleeease, Huyo rais wenu mwenyewe Dr. Shein ana kadi ya bara, iwe kujiandikisha kupiga kura ama account zake sasa haya ya kujenga Uzanzibar kwa uzawa kusema kweli sidhani kama tunaijenga nchi hamjawa wayahudi....
Mkandara

Hawa Nonda wako wawili?
Mmoja Mtanganyika, mmoja mzanzibar?
Au wa Tatu, Nonda mtanzania?

Huyu naye ni Mzanzibari? link https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/277714-zanzibar-is-gone.html#post4040193

Nonda huyu anaendika hapa ana "chogo" cm 20 ishirini mkuu!

Turudi kwenye mada na hoja.
 
Nonda said:
Kwa mchango huu umeonesha kuwa unaweza kufanya uchambuzi na upembuzi. Nilifikiri kuwa mwanzoni unaona moves za UAMSHO (wa-zanzibar)ni za kidini na ubaguzi. Wengine na nyimbo yao "usultani, upemba, unguja, mwalabu, gozi"


Nonda,

..UAMSHO ni ma-radical na hoja zao zimejikita ktk ubaguzi,chuki,na upotoshaji.

..kuna kauli nyingi sana za upotoshaji na chuki ambazo zinatolewa ktk mihadhara yao.

..hata ukiangalia ktk Mzalendo.net utakutana na wachangiaji wengi sana wenye chuki na ubaguzi.

..kuna MODERATES ambao wanajenga zaidi hoja ya KIUCHUMI na KIJAMII wakizingatia kwamba kuna manufaa ambayo Zanzibar inayapata ktk muungano huu na wangependa waendelee kunufaika nayo.

..moderates hao ambao wanajumuisha wasomi wa Kizanzibari pamoja na jumuiya kama ZANZINET wamekuja na mapendekezo ya kuwepo kwa "MKATABA" baina ya Tanganyika na Zanzibar.

..sasa mkataba huo in essence ni mrija wa Zanzibar kuendelea kuinyonya Tanganyika kwasababu inajulikana bila shaka yoyote kwamba kwamba Tanganyika does not need Zanzibar kiuchumi wala kijamii.
 
Mkuu Mkandara,
Ni kweli kabisa wanataka wawe ndani ya EAC ili waendelee na kunufaika na Tanganyika.

Kuna matatizo mawili nayaona.
1. Kwa vile watakuwa wamewabagua Watanganyika, chuki hiyo itaendelea hadi kwa Wakenya na Waganda. Katika nchi radical kama Kenya huwezi kumzuia asifanye shughuli zake Zanzibar wakati wewe upo Mombasa.
Ni lazima wazanzibar watabaguliwa. Hakuna nchi katika EAC inayokaribiana sana kiutamaduni kama tulivyo na hapo watarudi tu.

2. Mkuu Joka kuu kasema hakuna kukubali mkataba wa aina yoyote. Hata EAC itakapokuwepo bado kila nchi itakuwa na mambo yake ambayo mengi yanaiathiri Zanzibar. Sasa hivi hakuna mkataba wala muungano, tunasubiri tu waondoke kabla ya July 1 2012 au Dec 2012!

3. Kuondoka kwa Zanzibar katika muungano katika hali ya matusi, ubaguzi na kejeli itaacha makovu ambayo yataendelea tu kuwaumiza. Unajua, kuna Wazambia wengi na wamalawi nchini, kuna Wakongo na Warundi, wote wanaishi vema kwasababu hatuna ugomvi nao. Waganda wanaishi vizuri sana hata baada ya vita kwasababu hakuna mganda aliyemkosea Mtanzania ukiacha Idd Amin na genge lake. Lakini angalia makovu ya mwaka 1977 ya Kenya. Nadiriki kusema Wakenya pengine wana wakati mgumu kuliko raia wengine kwasababu za ugomvi wa mwaka 1977 dharau na kejeli pamoja na ubaguzi.

Zanzibar kwa mwendo wa chuki watakuwa victim number 1 ndani ya EAC, hilo linakuja na litawaumiza. Litawaumiza kwasababu kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni Zanzibar haiwezi kukwepa kivuli cha Tanganyika hata siku moja. Kama itafanya hivyo ni kwa gharama kubwa sana.

Ukitaka kuona chuki ilivyotanda dhidi ya Wazanzibar ni pale jana uwanja wa taifa vijana wlipobeba bendera ya Tanganyika. Hatua inayokuja ni kuwatoa maofisini kwa mwikaju, na kisha wamachinga kusimika bendera katika maduka ya wapemba. Mzanzibar ataonekana mhalifu hata kama hana hatia na hilo naliona hata kama watu watafumba macho.
Hiki ndicho UAMSHO isichokiona na madhara yake ukisikika na lafudhi ya kizanzibar hata ndani ya EAC utakuwa victim
Time will tell

Kwa mantiki hiyo ni bora waende zao mapema sana ili watuache na matatizo yetu. Kenya ilipovunja EAC tumebaki kama taifa na sasa tupo strong pengine kuliko wakati mwingine.

LET ZANZIBAR GO!
 
Hivi bado wapo tu???? Wataondoka lini hawa zanzibar??? Kelele nyiingi lakini hawatoki
 

kwanza nakupongeza mleta hoja.
Pili kuna sehemu moja ambayo umeizungumza na nzito sana,hoja hio wengi wanaifahamu kuwa tayari zanzibar ishakuwa nchi kwa marekebisho yaliofanyiwa na smz,lakini ufahamu kuwa marekebisho yake kwa hatua ile imeipa zanzibar hadhi ndani ya muungano tu na sio nje ya muungano,kilicho baki kwa wazanzibari kudai zanzibar yao nje ya muungano kuwa nchi huru ni kiti cha umoja wa mataifa.
Kama unafahamu kuwa kiti ambacho kinachotumiwa kwa tanzania ndani ya UN ni kiti cha wazanzibari, kimeondolewa na kuitwa tanzania,kama haufahamu hilo nakupa kazi fanya hio kisha rudi hapa tena.
Kwa kumalizia jamuhuri ya watu wa zanzibar itarudishwa na wazanzibari wenyewe tena wananchi na sio viongozi kwa kikatiba viongizi wote hadi znz wapeapishwa kuulinda muungano kwa gharama zote.
 

Nasikitika na wewe umeingika katika kundi la wapotoshaji!

Kwa nini ifikie hiyo hatua ya kuachana kwa chuki? kwani wanachokitaka wazanzibar ni nini? si kura ya maoni itakayoamua mustakabari wa wazanzibar! Mbona vitisho vingi sana?
 
Naunga mkono hoja ila kinachonisumbua ni kuwa ujue kuna wazanzibar wengi wanafanya biashara bara na wengine wengi wameajiriwa bara kwenye sector binafsi na wengine bado wako vyuoni ukiongea nao hawa yaani hawana majibu ya kuridhia hawaupingi wala kuunga mkono sasa sijui wanahofu kuwa muda si mrefu watakosa keki huku bara? halafu ukweli usiopingika nimeishi zanzibar siku 40 nilikuwa kwenye training u kweli usiopingika kabisa mimi nilikuwa silijui hili kuna ubaguzi kati ya unguja na pemba halafu na umri wangu wote nilikuwa sijui pemba ni wapi na unguja ni wapi. niliona kabisa mtu wa unguja anamdharau mtu wa pemba na nilipouliza wanasema kuwa watu wa pemba hawafanyi kazi eti kukaa kwenye kahawa hapo nikagundua kitu kuwa kumbe kuna tatizo hapo nimesoma kwenye blog ya zanzibar kuwa watu wabara tunania mbaya ya kuwatengenisha waunguja na wapemba eti hakuna kitu kama hicho lakini ukweli kutoka mioyoni mwao wanalijua hilo kuwa kuna ubaguzi kati yao na kuna mzanzibari mmoja alijibu kuhusu hilo akasema ni kweli sisi waunguja tuna ubaguzi na hata kule pemba kuna barabara za kupitisha gutta tu gari hazipiti, alishambuliwa sana na waunguja kisa kasema ukweli. ILA CHA MSINGI TUWAACHE WAENDE WAKAJENGE NCHI YAO NA TENA WATAKUWA NDANI YA EAC. kwa walioa tanzania bara wanabahati watabaki il sidhani kwa walioa zanzibar watabaki huko maana walivyowabaguzi ni balaa.
 

ndugu yangu.
Naona ume base sana upande wako eti ubaguzi,nakuuliza hivi ushawahi kuwa zanziba uchaguzi wa 95,2000,maandamano ya 2001,2005,kama ulikuwepo miaka hio yote,zanzibar ilikuwa na utawala wa kibaguzi,wazanzibari wananyanyaswa kwa kutumia jeshi la muungano,watu waliuwawa hapa zanzibar,walibakwa,kuna walikuwa walemavu,kuna walikuwa mayatima,yote hayo kulinda ccm madarakani na ndio muungano wenyewe,hivi kwa aliki yako kama ni wewe mzanzibari utakuwa na imani na mtu kutoka bara ? Nakupa mfano ,ingekuwa nyinyi wazanzibar na sisa watanyanyika tukawafanyia haya yote mungekubali ? Tungeacha masualaya kiuchumi ? Hapa zanzibar sijaona police wala jwtz mtu mwenye asili ya kiarabu kwa nini ? Mpaka uwonekane una asili ya bara,iwe baba au mama au babu? Kwa nini ? Ubaguzi wa kutosha kwa muungano juu ya wazanzibari,hata mwalimu nyerere alishatamka kuwa angekuwa na uwezo angeviondowa visiwa vyetu,why ? Chuki na roho mbaya. Ukweli huo.
 
JokaKuu

Sauti za Zanzibar zinapokuja na malalamiko yao , tunawapuuza au huwa tunawapiga-date.
Ile sauti moja inayozimwa, baada ya muda inaibuka nyengine kali zaidi. Tunawa-radicalise! na kuwabeza.

Hoja yao ya msingi UAMSHO ni kura ya maoni juu ya kuutaka au kuukataa Muungano. Kuna kikundi ambacho kinataka kuwa-sabotage waonekane ni wahuni, ma-radical, wabaguzi kwa kuwabambikizia "uchomaji wa makanisa" ili kuua dai lao. Leo hakuna anaezungumzia au kuunga mkono kura ya maoni badala yake tunazungumzia, UAMSHO wadini, ma-radical, wanataka usultani, wanatuita machogo nk.

Unapoau hoja yao ya msingi katika upeo huu wa kuwadharau au kuwabambika majina ni kuwa hushughulikii kero wanayoiona, au tatizo wanaloliona bali tunawajengea jina ambalo jamii wakilisikia watawatoa maanani. Kwa tabia hii ni sawa na kufanya usafi nyumbani halafu unaweka uchafu chini ya zulia kuna siku, maradhi yatatuumbua.

Link https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/277714-zanzibar-is-gone-2.html#post4041423


Chuki niisomayo ktk Mzalendo.net naisoma pia ktk JF


Hawa UAMSHO (wazanzibari),watu laki tisa wanajaribu kutuonesha njia ya kupata nafasi na muda wa kushughulikia matakwa na matatizo ya watu milioni 40 lakini sisi au miongoni mwetu tunalazimisha, tunang'ang'ana na kuwang'ang'ania watu laki tisa na ushee!

Ni uendawazimu au ni ukichaa? 48 miaka haijatosha kucheza hide and seek? Na kuacha kila upande unalalama?

Ni wazi kama Matola na Mungi wanavyoona kuwa Watanganyika wakitaka within 24 hrs Muungano uvunjike/ uvunjwe basi hakuna wa kuzuia hilo lisitokee. Au tunasubiri ije kutoana pua na macho kwanza ndio lifanyike hilo?
Links 1. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...tta-nyerere-na-wa-tz-bara-12.html#post3071074
link 2. https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/277714-zanzibar-is-gone.html#post4040193


Faida na hasara ya kuvunjika kwa muungano, kila upande utapiga mahesabu yake baadae lakini kwa hivi Muungano unavyoendeshwa na kulelewa utatuletea majanga.
 
ile chilisosi inakuchengua bado ??
Kamwewe mie nashangaa kuona bado hamjajitenga. mkitaka kujitenga si mumuambie shein tu atangaze zanzibar nchi hata kesho??. mie sioni sababu ya maandamano, mihadhara ,na kelele nyingine nyingi, nyie si muanze tuuuu!
 
kamwewe mie nashangaa kuona bado hamjajitenga. Mkitaka kujitenga si mumuambie shein tu atangaze zanzibar nchi hata kesho??. Mie sioni sababu ya maandamano, mihadhara ,na kelele nyingine nyingi, nyie si muanze tuuuu!

tumekosa mboga ya chilisosi
 
Sisi hatulalamika kuwa ni koloni, hatujawahi kuchoma moto watu na mali zao. Kama hivyo ndivyo una 'advocate' nachelea kusema ni hatari.
Kama unadhani UAMSHO style ni njia muafaka basi hebu sema uone balaa! mungu pishilia mbali!!!!!!

Pili, hakuna jina lingine la UAMSHO kama si boko haram, alshabaab kwasababu matendo yao kauli zao, ubaguzi wao na mtazamo wao ni phoyocopy. Anayekataa hili akamuone Psychiatrician

Tatu, JF hakuna chuki kuna darasa la kuwasadia njia rahisi ya kuondoka katika muungano.
Chuki za kuchoma wanadamu na majengo moto zinaanza kujitokeza kwa majibu kama yale uwanja wa taifa.
Ni vema mkawahi maana chuki hizi zikichukua sura ya UAMSHO, hakika wazazibar wataumia

Tunatoa nafasi Zanzibar wajitoe, vinginevyo hatunyanyua hata njiti ya kibiri au usufi kumwadhibu Mzanzibar.
Tutawaondoa kwa njia moja tu! Serikali moja ya JMT
 

yaelekea wewe ni polisi zaidi ya wale polisi waliowakamata waliochoma makanisa.
Tafadhali nenda kawakamate hao uamsho na uiambie mahakama iwaachie wale watu 30 walioshutumiwa kufanya hizo shutuma unazowatumia uwamsho
 

Kwa hiyo, ile kuchoma moto makanisa ni mbinu ya kuleta serikali moja?

Janja paka, panya ............

Pacha wako pia nasema hili. link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...tta-nyerere-na-wa-tz-bara-10.html#post3070223

Ofisi ya huyo Psychiatian iko wapi? Ulishafika huko?

Unafanya kazi nzuri mkuu Nguruvi3 ya kubuni majina.

Kwa hiyo, UAMSHO ni Al qaeda? au Boko haram?

Maumivu ya kichwa, huanza pole pole.....tumia HEDEX!
 
Me naona kuna sababu za kiusalama zilizofichika hapa...TSSA wanafahamu, na hii visit ya kiongozi wa Iran ktk kipindi crucial ina ring a bell kichwani, otherwise zanzibar haina economic advantages kwa bara zaidi ya hizo za kiusalama, nionavyo mimi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…