Nguruvi3,
Unajua mkuu wangu ktk swala hili la Utengano Wa -Zanzibar wajanja sana. wanajua sana kwamba Muungano Ukivunjika bado watapata hisani zote kutokana na kuwepo kwa EAC maana kila wanachokihitaji toka kwetu kitakuwa ktk EAC hivyo huwana sababu ya kuendelea kuwepo ktk muungano wakati Jumuiya ya EAC inawapa advantage zote wanazozihitaji toka bara. Hao Wazanzibar waliopo Bara watalindwa na ushirika huu lakini sidhani kama hii Jumuiya inaweza kulazimisha Zanzibar kupokea wageni wasiowataka...
Mkuu Mkandara
Kwa mchango huu umeonesha kuwa unaweza kufanya uchambuzi na upembuzi. Nilifikiri kuwa mwanzoni unaona moves za UAMSHO (wa-zanzibar)ni za kidini na ubaguzi. Wengine na nyimbo yao "usultani, upemba, unguja, mwalabu, gozi"
Sasa kwa uchambuzi huu unaonesha kuwa Wazanzibar wanatizama maslahi yao kinchi, na sisi wengi wetu hapa JF tunakoleza udini tu na chuki miongoni mwa watanzania.
Tokea ilipofufuliwa EAC kama tungefuata ushauri wa mwanzilishi wa Muungano mwenyewe,hakuna UAMSHO au nani angepata mwanya kuparaganya udugu,uhusiano na mshikamano wa Tanzania (Tanganyika na Zanzibar).
Mwalimu alitoa rai kuwa itakapoanzishwa tena jumuiya ya Afrika Mashariki basi Tanzania iwe na serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar.
("Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Masharikizikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili- ya Zanzibar na ya Tanganyika ..." Uk 11 .link ya kitabu hii )
Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)
Tanzania ingekuwa na sauti kubwa katika EAC kwa uwepo wa Tanganyika na Zanzibar kama serikali zanazojitegemea. Wabunge 9 kila mwanachama,ingefanya 18 kwa Tanzania. Influencial voting block.
Kitafute kijarida cha shirikisho ndani ya shirikisho ukipitie kwa utuo.