kama Tanganyika inalipa madeni sikiliza hii kitu
Video – yale mamlaka ya Tanganyika yote tupeni Zanzibar sasa na Tanganyika bebeni unyonge wa Zanzibar sasa!
Hakuna haja ya kufanya mambo nusu nusu, BLM waandae muswada wa kujitenga ASP, na mchakato uanze 'yesterday' ili by 1/1/2013 Zanzibar or niseme Jamhuri ya Zanzibar iwe huru. Hili litakuwa jambo la heri kabisa.
unamuambia nani humu jf ??? Waonaje ukaweka muhadhara au ukawaona wenyewe blm
hivi hawa mbu bado wapo ndani ya neti tu??
Aaaargh, wapi rungu??
Jana nimesikia BLW wakisema wanataka mgao wa 4.5 uongozwe hadi 11%. Wanasema sasa hivi wanapata mgao wa 7% kutoka hazina Dar ambayo ni Hazina ya Muungano a.k.a Tanganyika.
Hawajasema wao wanachangia nini katika hilo pato la taifa ili wadai zaidi au hata kupata tu!
BLW wanadai wapewe fungu la elimu ya juu kutoka hazina ya muungano. Hapa ndipo nasema Wazanzibar ni wanafiki sana. Siku zote wanasema Tanganyika imeongeza MAMBO 11 ya muungano hadi kufikia 22. Wanasahau kuwa elimu ya juu haikuwa suala la muungano, lakini wanapotaka pesa za elimu ya juu wanasema ni haki yao!
Hakuna hata mmoja aliyesimama na kusema hataki muungano, sasa hapa ndipo nachanganyikiwa wale wazanzibar 'wengi' wanawakilishwa na nani? UAMSHO au BLW , na je BLW ni vibaraka na wasaliti kama viongozi wa muungano kutoka Zanzibar?
Joka Kuu, huu mgao wa asilimia 7 ni zawadi. Bajeti yao ya mwaka huu ni bilioni 307 matumizi, na bilioni 341 fedha za maendeleo kwa ujumla wa bilioni 600.Nguruvi3,..kuhusu mgao wa mapato, kuna afisa wa TRA Zanzibar amedai kwamba makusanyo yote ya TRA Zanzibar hubakia huko huko. Hakuna wanachowasilisha makao makuu Dar-Es-Salaam. sasa mpaka hapo najiuliza, Zanzibar inachangia kiasi gani ktk shughuli za muungano?
..Pia huu mgao tunaowapa wa asilimia 4.5, na sasa unasema asilimia 7, unapatikana vipi? Mbona unapingana na vigezo vya mchango wao, na ukubwa wa uchumi wa Zanzibar?
..Kutokana na Zanzibar kushindwa kuchangia mfuko wa muungano na hivyo kuwa mzigo kwa wa-Tanganyika nadhani hakuna haja ya kuwa na muungano, au hata "mkataba". Suluhisho la kuduma la matatizo ktk mahusiano baina ya Tanganyika na Zanzibar ni nchi hizi mbili kuwa wanachama wa East Africa community au SADC.
not ukalimu bali ni ukarimu, anyway,,,,,,, sisi hatutakukumbukeni kwa lolote bali kwa maovu na ufisadi na unyonyaji wa visiwa vidogo vya zanzibar,na waende wakapewe misaada na ndugu zao wa Oman!lkn for sure watatukumbuka na ukalimu wetu!!
Joka Kuu, huu mgao wa asilimia 7 ni zawadi. Bajeti yao ya mwaka huu ni bilioni 307 matumizi, na bilioni 341 fedha za maendeleo kwa ujumla wa bilioni 600.
Utaona kuwa fedha zao za maendeleo ni nyingi kuliko za matumizi kwasababu
1. Hawana bajeti ya vyombo vya ulinzi na usalama
2. Hawana bajeti ya kuhudumia viongozi wao wastaafu kwa kada zote
3. Hawana bajeti ya mishahara kwasababu inatoka hazina Dar es salaam
4. Hawana bajeti ya elimu ya juu kwasababu watoto wao wanasoma kwa pesa za Muungano
5. Hawana bajeti ya wabunge wao walioko Dodoma
6. Hawana bajeti ya nishati kama umeme serikalini hadi majumbani, si Ikulu wala BLW wantumia umeme wa bureee!
Kuna umuhimu wa kuwaeleza viongozi wetu hasa wabunge kusimamia masilahi yetu.
Tuwaunge UAMSHO mkono na jitihada zao ili tutue hili zigo la misumari
LET ZANZIBAR GO! Jamani hatuna cha kupoteza waacheni waende hata kesho, kwanini tubebe mzigo na matusi ikiwa ni pamoja na kumwgiwa petroli na vibiriti kwa hisani zetu?
Kwa nini hatudai Tanganyika yetu kama hawa jamaa wanafaidi kutunyonya?
Hivi hatuwezi kuwafundisha njia rahisi watanganyika kama tulivyowaeleza njia rahisi wazanzibari kutoka katika Muungano?
Tuanzishe Rebirth of Tanganyika movement 2012.
Mwanakijiji, Nguvuri3, Mag3,FJM, Mkandara, Zinadine, Chilisosi, Raj Patel, JokaKuu,Taso,Masopakyindi, na kila menye uchungu na mama Tanganyika, sasa kampeni ihamie katika kudai Tanganyika.
Mtu laki 1.5 inayotoka Zanzibar iliyopo Tanganyika tunaweza kuipa uraia wa Tanganyika na hii kelele ya" tunanyonywa" itakuwa tumeipatia dawa yake.
It is so simple! Tunaogopa nini? Sasa ni wakati wa ukweli na uwazi.
Ni kwa watanganyika kuidai Tanganyika tu ndio njia rahisi ya kutatua kero hii ya Muungano.
Kwa nini hatuidai Tanganyika? Tunaogopa kuwa land-locked country? Mbona Ethiopia, Zambia zimeweza?
Kwa nini tunaendelea na Muungano unaotutia hasara?
Let Tanganyika be born again! Let us have our Tanganyika back! Let us reclaim her! Can't we?
Say no to uamsho
Nguruvi3,
..kwanini mabilioni ya pesa za wa-Tanganyika yaende kulipa wajumbe wa tume ambao hawako pale kutetea maslahi ya wa-Tanganyika??
..suala la Zanzibar kudai nusu ya wajumbe wa tume ya katiba lilipaswa kujibiwa kwamba SMZ watawajibika kulipia nusu ya gharama za posho ya wajumbe wa tume ya katiba.
..kwenye bunge la muungano kuna wabunge toka Zanzibar wanalipwa[according to uamsho] mil 12 kila mwezi kutokana na kodi za wa-Tanganyika.
..umefika wakati sasa wanasheria wakae pembeni ktk kuujadili muungano huu. nafasi hiyo wachukue wachumi na wataalamu wa fedha. u will never hear Prof.Shivji and the likes discussing jinsi muungano unavyowadhulumu kiuchumi wa-Tanganyika. kila siku ni makelele ya hati ya muungano, hati ya muungano...
..LET ZANZIBAR GO!!!
Kwa nini hatudai Tanganyika yetu kama hawa jamaa wanafaidi kutunyonya?
Hivi hatuwezi kuwafundisha njia rahisi watanganyika kama tulivyowaeleza njia rahisi wazanzibari kutoka katika Muungano?
Tuanzishe Rebirth of Tanganyika movement 2012.
Mwanakijiji, Nguvuri3, Mag3,FJM, Mkandara, Zinadine, Chilisosi, Raj Patel, JokaKuu,Taso,Masopakyindi, na kila menye uchungu na mama Tanganyika, sasa kampeni ihamie katika kudai Tanganyika.
Mtu laki 1.5 inayotoka Zanzibar iliyopo Tanganyika tunaweza kuipa uraia wa Tanganyika na hii kelele ya" tunanyonywa" itakuwa tumeipatia dawa yake.
It is so simple! Tunaogopa nini? Sasa ni wakati wa ukweli na uwazi.
Ni kwa watanganyika kuidai Tanganyika tu ndio njia rahisi ya kutatua kero hii ya Muungano.
Kwa nini hatuidai Tanganyika? Tunaogopa kuwa land-locked country? Mbona Ethiopia, Zambia zimeweza?
Kwa nini tunaendelea na Muungano unaotutia hasara?
Let Tanganyika be born again! Let us have our Tanganyika back! Let us reclaim her! Can't we?
Nilifikiri tunaogopa kivuli cha maili 10?Nonda,
..zingatia hapo kwenye RED.
..Tanganyika iliyoungana na Zanzibar haikuwa landlocked.
..sasa tutakuwa vipi landlocked ikiwa muungano utavunjika??
NB:
..the 10 mile coastal strip, pamoja na eneo la Mombasa, Sultani waliokuwa madarakani waliyauza na kutia pesa mfukoni.
JokaKuu
Kama Tanganyika haipo, watanganyika wametoka wapi?
Hili ndio kosa tunalolifanya!
Tudai kwanza Tanganyika iwepo, hapo itakuwa rahisi kushughulikia mambo haya. Leo Tanganyika inasemwa haipo, halafu utasikia serikali ya Zanzibar inajadiliana na serikali ya Muungano. Tuache utani huu.
Hivi tunaufahamu huu Muungano? Mimi naona huu Muungano ni kama monster, wa-tanganyika(wabara) wanalalama kunyonywa na Muungano, wazanzibari wanalalama kunyonywa na Muungano?
Kwa nini kuendelea na huu mzimu?
Kwa nini kauli za mtu laki 9.5 zinasikika zinapiga kelele kuwa hazitaki Muungano lakini sauti 40 milioni zimebana kimya? Kama vile ziko katika usingizi ile ya samaki. Mtu 40 milioni zimelala fofofo? Mtu milioni 40 hazijitambui?
Mtu milioni 40 haziwezi kuhoji mazingaombwe haya(muungano)?
We are vely zaifu! Mnyika ameliona hili.
Tanganyika first, Mazingaombwe(muungano) basi! Enough is enough!
Nonda said:Nilifikiri tunaogopa kivuli cha maili 10?
Sasa tunaogopa nini kudai kuirudisha Tanganyika?
Kwa nini tunapigizana kelele na mtu laki 9.5?