Nonda,
..zingatia hapo kwenye RED.
..Tanganyika iliyoungana na Zanzibar haikuwa landlocked.
..sasa tutakuwa vipi landlocked ikiwa muungano utavunjika??
NB:
..the 10 mile coastal strip, pamoja na eneo la Mombasa, Sultani waliokuwa madarakani waliyauza na kutia pesa mfukoni.
Nilifikiri tunaogopa kivuli cha maili 10?
Sasa tunaogopa nini kudai kuirudisha Tanganyika?
Kwa nini tunapigizana kelele na mtu laki 9.5?
Nani mwenye nguvu na sauti baina ya mtu laki 9.5 na mtu 40 milioni?
Kama mtu 40 milioni zinataka Tanganyika back nani atazuia hili?
Mimi mpaka mida hii nashindwa kuelewa kwa nini tumeweka mkazo kuwa wazanzibari wajikate wakati tutakapoirudisha Tanganyika tutakuwa tumemaliza mazingaombwe ya muungano.
Vitu/mambo yatakuwa wazi, wala mtu hatahitaji darubini, mipaka, mamlaka, sheria zitakuwa wazi. Sio kama sasa mkorogo tu, tirigivyogo, shagala bagala!
Muungano, mambo ya Muungano, mambo ya Zanzibar, mambo ya bara(Tanganyika), Zanzibar ipo, Tanganyika haipo, Serikali ya Zanzibar ipo, serikali ya muungano ipo, serikali ya mambo ya Tanganyika haipo.
Serikali ya muungano ndio hiyo hiyo wakala wa serikali ya Tanganyika, mgongano wa kimaslahi na ulalamishi.
Tanzania nchi moja lakini kila upande una mambo yake halafu kuna mambo ya pamoja! Unaelewa chochote hapo?
Upande mmoja unadai unachangia/unatoa kila kitu na upande mwengine "unapokea" unaopokea mgao unadai unanyonywa! Unaelewa chochote hapo?
Ya nini mazingaombwe yote haya? Hatujachoka nayo?
Miaka 48 tunajitahidi uongeza mambo ya muungano ili Tanzania iwe nchi moja na pia tunataka kuleta serikali moja. Kwa miaka isiyopungua 46 upande mmoja unalia unafanyiwa rafu. Tunajifanya kuziba masikio,
Mpaka mida hii kuna mambo hayajawa ya muungano, yet tunasema Tanzania ni nchi moja. Kweli Tanzania ni mazingaombwe tu, usanii.
Warioba kapewa hadidu rejea za katiba mpya, juzi amesema watu wajadili wanavyotaka,waseme watakayo kuhusu Muungano. Huyu mzee anatania watu 40milioni na laki 9.5?
Mtu 40 milioni zitamke ,tunataka Tanganyika yetu, zimwambie Warioba achukue
bara yake, arudishe Tanganyika yetu!
Mzee wa mazingaombwe anapewa jukumu la kukusanya maoni yetu.
Utani kwenye vitu vya msingi utatumaliza.