Umenielewa sawa Zinedine.
Pia nisome katika michango mingine niliyotoa. Nimesema kuwa mimi si mmoja ya wanaoamini kuwa UAMSHO wanamkono katika uchomaji wa makanisa. They are framed in order to be silenced.
Nani amefanya hiyo kitu?....Ving'ang'anizi. Kadas zinazopenda kung'ang'ania madaraka ndio zina mkono hapo.
Unawabambikizia UAMSHO dhambi ya kuchoma kanisa. Unaziba mdomo wao kujitia kimbele mbele katika kutaka kura ya maoni na ukarabati wa Muungano, wakati huo huo unapata mtu kama M.Mwakijiji na Nguruvi3 anasema UAMSHO wamechoma makanisa na kuamsha hisia jazba ya waislamu vs wakristo, wazanzibari vs wabara (watanganyika)
Wajanja wameua ndege wawili kwa jiwe moja.
Hii "framing" ikifanikiwa basi nakubaliana na wewe kuwa JUMIKI watakuwa wamewapotezea watu muda wa kuvua samaki. Kama watweza kujipapatua na tuhuma hizi basi watakuwa wamesaidia sana kutika kupata mjadala wa wai na mpana juu ya Muungano.
Ama hayo maelezo mekundu...hapo mkuu mimi Nonda nimetaja uhalisia "fact" tu. Kama ukilijua hulijui hilo na pia kama umekubali kujiunga na Let Zanzibar go! kwa mfumo/staili ya M. Mwanakijiji, Nguruvi3 basi ujitayarishe kwenda all the way ukijua kuwa wote waliojaribu mwanzoni wamekumbana na "maguvu", Tsunami ya ving'ang'anizi.
Hata hivyo niseme kuwa kama M.Mwanakijiji na Nguruvi3 wangeanzisha move kama ya UAMSHO yaani kama watanganyika kuilalamikia Muungano moja kwa moja na sio kuibuka na kuipinga UAMSHO basi hii move ingeoana na ile ya UAMSHO na mkandamizo (pressure) kutoka kundi la Zanzibar na mkandamizo ambao ungetoka kwa uwazi kwa upande wa Tanganyika ungeweza kuibinya Serikali ya Muungano na hapa Serikali wangekuwa hawana njia bali kufungua mjadala wa wazi na mpana wa Muungano na hatima yake.
Tuendelee na mjadala.
Mkuu Nonda, kwa akili za ki-imaan, hata mimi naamini viongozi wa JUMIKI hawajachoma na wasingelithubutu kuchoma kanisa, lakini kama umeangalia vidio zote au kuhudhuria mikutano ya JUMIKI huwezi kuwatenganisha JUMIKI na uchomaji wa makanisa au kuongezeka kwa chuki za Wazanzibari kwa Watanganyika(ikiwa zimeongezeka). Nahisi kama mkuu Nonda unachangia lakini hukujiridhisha vya kutosha juu ya harakati za UAMSHO namna zilivyopamba moto badala yake umestick kwenye historia ya siasa za CUFvsCCM enzi za Janjaweed, lah, JUMIKI iliwaaminisha, hamasisha, na wataka vijana kujua kuwa:
1. Hali yoyote mbaya ya kimaisha, kiimani au ki-utamaduni inayotokea Zanzibar,chanzo ni Muungano na Watanganyika
2. Watanganyika wamejazana Zanzibar kupita kiasi kuliko "wapemba" walivyojazana Tanganyika
3. Watanganyika wanaung'ang'ania sana Muungano kwa kuwa wanafaidika sana hivyo kuwataarisha vijana "kuwa tayari" kwa nafsi na kwa nguvu kuikomboa Nchi yao, kiasi ambacho walikuwa wanasubiri go ahead tu waanze kufanya chochote
4. JUMIKI iliwaaminisha kuwa Zanzibar haina sifa ya kuwa na Mkristo hata mmoja, kwa kuwa ni Nchi Takatifu na wakristo wote wa Zanzibar wameasili Bara kutokana na Muungano
5. Mapinduzi ya Zanzibar hayakufanywa na Wazanzibari na hayakuwa na sababu yoyote kwa kuwa Zanzibar ilikuwa tayari Huru, hili laweza kuwa kweli lakini tukumbuke kuwa kuna watu wanafahamika kuwa ni "koo za memba wa Baraza la Mapinduzi", na wengi wa wanafamilia zao ziko katika post tofauti za Serikali. Kwa mtizamo wangu hili litaleta mgogoro wa ndani kwa ndani hivyo kusababisha mgogoro mkubwa huko baadaye, JUMIKI wawaambie tu watu wao kuwa Mapinduzi yalikuwa "halali" na yamepita kwani ilikuwa ni sehemu za harakati za ujenzi wa Taifa hivyo kwa sasa tugange yajayo. (Zingatia hili)
6. JUMIKI wawaambie kuwa kuzorota kwa uchumi pia kunasababishwa kwa "spending policy" badala ya "investment spending", kwa kuwaambia kuwa Serikali imeongeza matumizi yake kutokana na ukubwa na maboresho ya service scheme za Serikali katika kipindi baada ya serikali ya umoja wa kitaifa tu, pasipo kuanza na hatua za kuwekeza mipango ya muda mrefu ya ku-offset kitakachojitokeza. Hii imefanya kusiwe na uwezo mkubwa wa kusimamia huduma za kijamii kutokana na mzigo huo, twapasa tulijue hili!
JUMIKI wawaambie watu wao waendelee na utaratibu wa kuvumiliana baina ya watu wa dini tofauti ikibidi wapate wawakilishi kutoka Jumuiya za Kikristo zilizoko Zanzibar katika harakati za kutaka kuvunja Muungano, ili jamii hii isione baada ya kuvunjika Muungano, then wao watakuwa "setback". Na hili litaondoa dhana kuwa harakati zinazoendelea ni za Uislamu v/s Ukiristo, Utanganyika,.
7. Waambie watu wao kutoa equal treatment kwa either Mtaliana, Mwingereza, Mtanganyika, Mkenya nk katika uharibifu wa Tamaduni za kizanzibari badala ya kuwa-classify watanganyika tu ndo waharibifu wa hayo lakini wataliana safi.
8. JUMIKI waje na 'alternative measures' za kujenga na kuendeleza Uchumi wa Zanzibar kutoka "Tourism-led economy" kwenda huko watakapopendekeza kwani, utalii ni miongoni mwa tools za kueneza utandawazi ambao kwa kiasi kikubwa always uko against na Dini(zote).
9. Wawaandae wazanzibari walioko Tanganyika kufanya 'mass capital and investment shift' kutoka Tanganyika kuja Zanzibar ili kuondoa economic imbalance itakayotokana na retaliation itakayosababishwa na kuvunjika kwa muungano, maana retaliation lazma zitakuwepo tu.
Nitarudi wacha ninywe chai kwanza naona kijua kinazidi kukaza hapa.