Leteni kero zenu tupo tayari kuzisikiliza na kuzitatua-SACP Simon Maigwa

Leteni kero zenu tupo tayari kuzisikiliza na kuzitatua-SACP Simon Maigwa

Ndagullachrles

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
256
Reaction score
259
Jeshi la polisi mkoani kilimanjaro limetoa wito kwa wananchi kujenga utamaduni wa kufikisha changamoto za kiusalama kwa jeshi la polisi kabla hazijageuka kuwa migogoro au matukio ya uhalifu .
Wito huo ni sehemu ya ujumbe wa kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa jeshi la polisi Nchini (SACP ),Simon Maigwa alioutoa leo, Oktoba 7, 2026, alipokuwa mgeni rasmi katika hafla fupi ya ufunguzi wa Wiki ya Huduma kwa Mteja iliyoandaliwa na Benki ya Azania, Tawi la Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Amesema baadhi ya wananchi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali za kiusalama ambazo, zisipotatuliwa kwa wakati, zinaweza kuibua migogoro na kuchangia kutokea kwa matukio ya uhalifu katika jamii.

“Wananchi wenye kero za kiusalama wasisite kuzifikisha Polisii,ni muhimu kuzungumza na Jeshi la Polisi ili kero hizo zisikilizwe na kutafutiwa ufumbuzi kabla hazijawa chanzo cha migogoro au uhalifu,” amesema SACP Maigwa.

Aidha, Kamanda Maigwa amesisitiza umuhimu wa wananchi kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na Jeshi la Polisi, ikiwemo programu ya “Ongea na Kamanda”, inayolenga kutoa nafasi kwa wananchi kuwasilisha kero, changamoto na masuala mbalimbali yanayohusu usalama ili ziweze kusikilizwa na kufanyiwa kazi.

Amesema ushirikiano kati ya wananchi na Jeshi la Polisi ni muhimu katika kuimarisha usalama, kuzuia uhalifu na kuhakikisha changamoto zinazowakabili wananchi zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati.

Kamanda Maigwa amewahakikishia wananchi kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kusikiliza kero zao, kuzifanyia kazi na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria, huku akiwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani na usalama katika jamii.

Kwa upande wake, Meneja wa Benki ya Azania, Tawi la Moshi, Yusuph Lenga, amemshukuru Kamanda Maigwa kwa ushirikiano uliopo kati ya Jeshi la Polisi na wananchi katika kuhakikisha shughuli za kibiashara na huduma za kibenki zinafanyika katika mazingira ya amani na usalama.

Lenga amesema wameamua kumwalika Kamanda Maigwa kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo kutokana na kutambua na kuthamini mchango mkubwa wa Jeshi la Polisi katika kulinda amani na usalama, akieleza kuwa bila uwepo wa amani na usalama, shughuli za biashara na maendeleo ya kiuchumi haziwezi kufanyika kwa ufanisi.
 

Attachments

  • IMG-20261007-WA0165.jpg
    IMG-20261007-WA0165.jpg
    443.6 KB · Views: 10
  • IMG-20261007-WA0184.jpg
    IMG-20261007-WA0184.jpg
    451.9 KB · Views: 8
  • IMG-20261007-WA0173.jpg
    IMG-20261007-WA0173.jpg
    255.8 KB · Views: 8
  • IMG-20261007-WA0168.jpg
    IMG-20261007-WA0168.jpg
    460.6 KB · Views: 8
  • IMG-20261007-WA0171.jpg
    IMG-20261007-WA0171.jpg
    410.5 KB · Views: 9
  • IMG-20261007-WA0176.jpg
    IMG-20261007-WA0176.jpg
    132.2 KB · Views: 7
Back
Top Bottom