Namuonea huruma huyo mama kama naye ataendekeza huo ujuha, basi mbona msifunge hospitali zote na hata kufuta elimu yote ya sayansi na kuwafuta madaktari wote wakachome mkaa vijijini na kufanya mengine. Mumejitoa ufahamu hadi kuonekana kituko cha dunia, kirusi kinawatafuna kuanzia mtu wa kawaida mpaka kwenye kichwa cha nchi lakini bado mumedumaa na kushupaza shingo.
Huyo Yesu unayemtaja, tupo wengi tunamuamini na tunaamini katika uponyaji wake, mimi nikiwemo kama Mkristo, lakini siwezi nikamlazimishia kwa mtu mwingine ambaye anaamini kitu kingine tofauti na imani yangu, na ndio maana taifa lina katiba na sheria ambazo zinahakikisha usawa, kwamba kila mtu na imani yake lakini tukutane kwenye katiba na kuchagua namna ya kuishi pamoja.
Urais ni taasisi, sio mtu binafsi na imani zake za kiroho.
Nina jamaa yangu mshikaji sana Tanzania, yaani zaidi ya ndugu nimepata taarifa anaumwa kwa hizo changamoto zenu, mpaka imenitia hofu sana sina amani moyoni.