LHRC, Amnesty International wataka Mbowe aachiwe na uhuru wa kisiasa uheshimiwe Tanzania

LHRC, Amnesty International wataka Mbowe aachiwe na uhuru wa kisiasa uheshimiwe Tanzania

Samia mpaka namuone huruma yani anguko lake litakuwa ni anguko la kijinga sana.

Huyu mama alikuwa na nafasi ya kunyamaza na kuachana na wakosoaji akafanya mambo yaliyo na maslahi kwa nchi angeua kabisa upinzani.

Ila hiki anachokifanya yaani atoamini yatakayomkuta

Subiri tamko la TEC ndio mtaelewa mfumo wa kutumia nguvu hauna kabisa nafasi katika dunia ya leo.
Mtu mwenyewe kaupata urais wakiwa hawamtaki. Badala ya kwenda vizuri sasa anataka kunasa kwenye mtego
 
LHRC, Amnesty International, Mbowe ana kesi ya ugaidi na hii ni mara ya pili anashutumiwa kuwa gaidi, mnataka mtuhumiwa wa ugaidi aachiwe huru bila ya kufuata taratibu za kisheria ?

Hata Lissu ambaye ni makamu mwenyekiti kasema hawamtolei dhamana. Tulieni sheria ifuate mkondo wake🐒
 
Masalia ya Jiwe na walamba viatu bado mpo
kinacho takiwa ni kwa Viongozi wa Chadema wafuate na kuheshimu sheria za nchi, wasijaribu kudharau mamlaka iliyopo, wakiheshimu sheria hakuna atakaye wasumbua ila wakiamua kuvunja sheria za nchi kwa makusudi hakuna atakaye wavumilia.
Amani ya nchi yetu ni muhimu kuliko Mbowe na wenzake.
 
LHRC, Amnesty International, Mbowe ana kesi ya ugaidi na hii ni mara ya pili anashutumiwa kuwa gaidi, mnataka mtuhumiwa wa ugaidi aachiwe huru bila ya kufuata taratibu za kisheria ?

Hata Lissu ambaye ni makamu mwenyekiti kasema hawamtolei dhamana. Tulieni sheria ifuate mkondo wake[emoji205]
aise Gaidi hafai kabisaa maaana huyo ni hatari wa usalama wa taifa lolote lile, jambo la msingi ushahidi tu uwepo, wasifiche kitu waweke bayana.
Ugaidi ni kosa kubwa sana.
Dunia yote sasa inapambana na Ugaidi.
Guantanamo imejengwa mahususi kwajili ya Magaidi.
vitendo vya ugaidi sio vya kufumbia macho hata kidogo.
 
View attachment 1863353
Mbowe pamoja na wenzake 11 kutoka chama cha Chadema walikamatwa na polisi usiku wa kuamkia Jumatano jijini Mwanza.

Mashirika yanayotetea haki za binadamu yameikosoa vikali hatua ya Jeshi la Polisini nchini Tanzania ya kuwakamata baadha ya viongozi wa chama cha upinzani nchini humo Chadema.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania na shirika kimataifa la Amnesty International ni miongoni mwa waliojitokeza na kupinga hatua hiyo.

Kwa upande wake, Amnesty International imeitaka serikali kusitisha mara moja kile ilichokiita kuendelea kudhibitiwa kwa upinzani nchini Tanzania.

Wito huu uliotolewa na mashirika haya, unakuja baada ya viongozi na wanachama kumi na mbili akiwemo kiongozi mkuu wa Chadema Freeman Mbowe kutiwa mbaroni huko jijini Mwanza usiku wa kuamkia tarehe 21 mwezi Julai.

Mbali na kukamatwa kwa viongozi hao, polisi pia iliweka doria katika moja wapo ya hoteli ambayo kulipangwa kufanyika kongamano kubwa lililopanga kujadili madai ya katiba mpya.

Rais Samia Suluhu

Chadema wanashinikiza mchakato wa katiba mpya licha ya Rais Samia kutangaza kuwa si kipaumbele chake kwa sasa

Mbowe ahojiwa Dar es Salaam​

Kwa upande wake, chama cha upinzani Chadema, kimesema mwenyekiti wake Freeman Mbowe hatimaye amefikishwa katika kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa katika ukurasa wa twitter wa chama hicho, imesema Freeman Mbowe "amepelekwa katika kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam baada ya polisi kufanya upekuzi nyumbani kwake na kuchukua laptop yake pamoja ya tablets za watoto."

Wakati huohuo, jeshi la polisi mkoa wa Mwanza limethibitisha kumshikiliaMbowe kwa mahojiano.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Ramadhani Ng'anzi amewaambia wanahabari kuwa Mbowe alitiwa mbaroni alfajiri ya kuamkia jana Jumatano Julai 21 katika hoteli aliyofikia.

"Baada ya kumkamata, wenzetu wa Dar es Salaam nao walitueleza kuwa wanamtafuta kwa makosa mengine anayodaiwa kuyafanya huko; hivyo tulimsafirisha kwenda Dar es Salaam anakoendelea kuhojiwa," amesema Kamanda Ng'anzi.

Mbowe anatarajiwa kurejeshwa Mwanza baada ya mahojiano ili aunganishwe na wenzake 15 wanaoshikoliwa kuhusiana na kongamano la Katiba Mpya lililozuiwa na jeshi hilo jana.

Kauli za hivi karibuni za Bw Mbowe​

Freeman Mbowe

CHANZO CHA PICHA,CHADEMA

Mwanzoni mwa wiki hii kiongozi wa Chadema Freeman Mbowe alifanya mkutano na waandishi wa habari ambapo alilalamikia kukamatwa kwa wafuasi wa chama hicho na polisi, pamoja na suala la mabadiliko ya katiba.

Chama kikuu cha Upinzani nchini Tanzania, CHADEMA kimesema hakitaendelea kumpigia magoti Rais wa nchi hiyo, Samia Hassan Suluhu kuhusu mustakabali wa taifa hilo, Bw Mbowe aliwaambia waandishi wa habari hivi Jumatatu.

Mwenyekititi huyo wa CHADEMA, aliyasema hayo kufuatia Jeshi la Polisi la nchi hiyo kuwakamata viongozi, wanachama wa chama hicho pamoja na viongozi wa dini 38 waliokuwa wahudhurie mkutano wa chama hicho kupitia baraza lake la vijana (BAVICHA) wenye lengo la kuhamasisha kupatikana kwa katiba mpya ya nchi hiyo.

Mara baada ya kuingia madarakani mwezi Machi mwaka huu, Rais Samia alitangazia umma dhamira yake ya kukutana na wapinzani ili kuzungumzia maswala mbalimbali ikiwemo ya kisiasa na namna gani ya kuendesha shughuli za siasa.

Licha ya kukutana na makundi mengine kama vijana, wazee na wanawake mpaka sasa Rais Samia hajakutaa na wapinzani. ''Hatuwezi kuendelea na ule utaratibu wa zamani, tuna haki ya kukutana tunakamatwa, tunapigwa, tunashitakiwa, tunasoteshwa mahakamani miaka miwili miaka mitatu, kisha tunaachiwa huru, ama tunahukumiwa vifungo batili tukikata rufaa sote tunashinda', alisema Mbowe
Pamoja na polisi kuzuia mkutano huo uliokua ufanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Boma wiki hii na kukamata watu hao 38, Kiongozi huyo wa Upinzani alisema, mkutano upo pale pale na utafanyika wiki hii na kama kukamatwa wako tayari kukamatwa wote.

Kama wanataka kuwaweka ndani wanachadema kwenye hoja hii ya katiba, wapanue kwanza na magereza, kwa sababu tuko tayari wote tuwekwe ndani , na wala hatutaomba dhamana' alisema Mbowe kabla ya kulaani kitendo cha Jeshi la Polisi Mwanza, kuwakamata viongozi wa dini na wafuasi wa chama hicho .

Chanzo: BBC Swahili
I saw it coming...Ilikuwa ni hesabu mbaya kwa CCM kumkamata Mbowe hasa wakati huu wa madai ya katiba mpya,wamempiga teke chura sasa wamemuongezea mwendo,walichotaka kuzuia sasa kitajulikana dunia nzima kuwa katiba mpya inatakiwa Tanzania.

Tatizo TISS inaongozwa na vilaza,haya sasa bado donors wanakuja,na dunia ya sasa sio kama ya akina Nyerere,dunia imestaarabika na mfumo ni democracy,udikteta hauna nafasi tena...make amends,release Mbowe or you put your international relations and investments into jeopardy!
 
Rais ameapa kulinda Amani na utulivu wa nchi hii na endapo akitokea mtu au watu wanaleta au kutishia Amani ya nchi lazima wachukuliwe hatu za kisheria, haijalishi ni kiongozi wa kisiasa au kiongozi wa kidini.
Mbowe na genge lake hako juu ya sheria, huwezi kusema eti yeye akifanya makosa basi aachwe tu.
Mbowe na viongozi wenzake wanachochea na kuhamasisha vurugu, hata ange kuwa marekani lazima angekamatwa na kufunguliwa mashitaka.
Amani ya nchi yetu ni Muhimu zaidi kuliko Mbowe na wenzake.
 
Wapi Robert Amsterdam na zile barua zake za kwenda Amnesty na The Hague! Hahahahahaha
Ngosha pumzika kwa amani!
 
Awamu hii ya 6 imejipambanua kufuata na kuheshimu utawala wa sheria ndio maana tumeshuhudia sote aliye kuwa DC wa hai kufunguliwa mashitaka na sasa yupo anakabiliwa na kesi zake huko mahakamani, vivyo hivyo kama mbowe na wenzake wakikutwa na tuhuma watafikishwa mahakamani kukabili mashitaka yao.
SHERIA NI MSUMENO
 
Na inaharibika tayari,tatizo ni CCM kutotaka kutii matakwa ya katiba iliyopo
usimchezee Mama, ni hatari, usidanganyike na majivu juu utaungua moto umefunikwa na majivu. ww nenda kichwa kichwa halafu utaona utakavyo babuka.
 
Wapi Robert Amsterdam na zile barua zake za kwenda Amnesty na The Hague! Hahahahahaha
Ngosha pumzika kwa amani!
Walijua baadae kuwa Ngosha ni maiti iliyokuwa inatembea ivyo hawakuona sababu ya kushtaki maiti
 
Samia mpaka namuone huruma yani anguko lake litakuwa ni anguko la kijinga sana.

Huyu mama alikuwa na nafasi ya kunyamaza na kuachana na wakosoaji akafanya mambo yaliyo na maslahi kwa nchi angeua kabisa upinzani.

Ila hiki anachokifanya yaani atoamini yatakayomkuta

Subiri tamko la TEC ndio mtaelewa mfumo wa kutumia nguvu hauna kabisa nafasi katika dunia ya leo.
Unajidanganya bure.
 
Back
Top Bottom