LHRC, Amnesty International wataka Mbowe aachiwe na uhuru wa kisiasa uheshimiwe Tanzania

LHRC, Amnesty International wataka Mbowe aachiwe na uhuru wa kisiasa uheshimiwe Tanzania

Mbowe atuhumiwa kwa mauaji ya viongozi wa Serikali​

Mbowe atuhumiwa kwa mauaji ya viongozi wa Serikali.jpg

Summary

  • Baada ya kushikiliwa kwa takribani siku mbili, Jeshi la Polisi limesema kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe anakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo za kupanga njama za kufanya vitendo vya kigaidi na kuua viongozi wa Serikali.
New Content Item (1)

By Mwandishi Wetu
More by this Author

Baada ya kushikiliwa kwa takribani siku mbili, Jeshi la Polisi limesema kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe anakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo za kupanga njama za kufanya vitendo vya kigaidi na kuua viongozi wa Serikali.

Taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime imesema kuwa kumekuwa na upotoshaji mkubwa kwamba, Mbowe alikamatwa kwa tuhuma za kupanga na kuandaa kongamano la Katiba mpya jijini Mwanza, jambo ambalo si kweli.

“Mbowe alikuwa anafahamu fika kuwa tuhuma zinazomkabili zilikuwa zinachunguzwa na wakati wowote angehitajika Polisi kwa hatua za kisheria mara tu uchunguzi wake utakapokamilika. Hatua hiyo imefikiwa sasa,” alisema Misime. chanzo. Mbowe atuhumiwa kwa mauaji ya viongozi wa Serikali
 
kwa hali hii ya Mbowe na wenzake kupanga Mauaji!! hawa sio binaadamu kabisaa ni zaidi ya wanyama.
Wauaji, wacha sheria ifanye kazi.
watanzania tunataka amani, magaidi waacha wakae huko gerezani.
 
Kombe Jiwe kafa kwa Korona? Mi najua tofauti
Kuna watu wanaamini hivyo na ukiwaambia tofauti na hivyo ni ugomvi, kwahiyo inabidi tuheshimu tu imani za watu utafanyaje sasa?
Maana ukimuuliza sababu za msingi zilizomfanya kufikiri kuwa Jiwe kafa na corona? hana hizo sababu zaidi ya kukwambia aliidharau corona. Kwahiyo unaacha tu maana kama nafsi yake mwenyewe inafarijika kwa yeye kuamini kuwa Jiwe kafa kwa corona basi unamuachia imani yake ajifurahishe.
 
View attachment 1863353
Mbowe pamoja na wenzake 11 kutoka chama cha Chadema walikamatwa na polisi usiku wa kuamkia Jumatano jijini Mwanza.

Mashirika yanayotetea haki za binadamu yameikosoa vikali hatua ya Jeshi la Polisini nchini Tanzania ya kuwakamata baadha ya viongozi wa chama cha upinzani nchini humo Chadema.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania na shirika kimataifa la Amnesty International ni miongoni mwa waliojitokeza na kupinga hatua hiyo.

Kwa upande wake, Amnesty International imeitaka serikali kusitisha mara moja kile ilichokiita kuendelea kudhibitiwa kwa upinzani nchini Tanzania.

Wito huu uliotolewa na mashirika haya, unakuja baada ya viongozi na wanachama kumi na mbili akiwemo kiongozi mkuu wa Chadema Freeman Mbowe kutiwa mbaroni huko jijini Mwanza usiku wa kuamkia tarehe 21 mwezi Julai.

Mbali na kukamatwa kwa viongozi hao, polisi pia iliweka doria katika moja wapo ya hoteli ambayo kulipangwa kufanyika kongamano kubwa lililopanga kujadili madai ya katiba mpya.

Rais Samia Suluhu

Chadema wanashinikiza mchakato wa katiba mpya licha ya Rais Samia kutangaza kuwa si kipaumbele chake kwa sasa

Mbowe ahojiwa Dar es Salaam​

Kwa upande wake, chama cha upinzani Chadema, kimesema mwenyekiti wake Freeman Mbowe hatimaye amefikishwa katika kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa katika ukurasa wa twitter wa chama hicho, imesema Freeman Mbowe "amepelekwa katika kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam baada ya polisi kufanya upekuzi nyumbani kwake na kuchukua laptop yake pamoja ya tablets za watoto."

Wakati huohuo, jeshi la polisi mkoa wa Mwanza limethibitisha kumshikiliaMbowe kwa mahojiano.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Ramadhani Ng'anzi amewaambia wanahabari kuwa Mbowe alitiwa mbaroni alfajiri ya kuamkia jana Jumatano Julai 21 katika hoteli aliyofikia.

"Baada ya kumkamata, wenzetu wa Dar es Salaam nao walitueleza kuwa wanamtafuta kwa makosa mengine anayodaiwa kuyafanya huko; hivyo tulimsafirisha kwenda Dar es Salaam anakoendelea kuhojiwa," amesema Kamanda Ng'anzi.

Mbowe anatarajiwa kurejeshwa Mwanza baada ya mahojiano ili aunganishwe na wenzake 15 wanaoshikoliwa kuhusiana na kongamano la Katiba Mpya lililozuiwa na jeshi hilo jana.

Kauli za hivi karibuni za Bw Mbowe​

Freeman Mbowe

CHANZO CHA PICHA,CHADEMA

Mwanzoni mwa wiki hii kiongozi wa Chadema Freeman Mbowe alifanya mkutano na waandishi wa habari ambapo alilalamikia kukamatwa kwa wafuasi wa chama hicho na polisi, pamoja na suala la mabadiliko ya katiba.

Chama kikuu cha Upinzani nchini Tanzania, CHADEMA kimesema hakitaendelea kumpigia magoti Rais wa nchi hiyo, Samia Hassan Suluhu kuhusu mustakabali wa taifa hilo, Bw Mbowe aliwaambia waandishi wa habari hivi Jumatatu.

Mwenyekititi huyo wa CHADEMA, aliyasema hayo kufuatia Jeshi la Polisi la nchi hiyo kuwakamata viongozi, wanachama wa chama hicho pamoja na viongozi wa dini 38 waliokuwa wahudhurie mkutano wa chama hicho kupitia baraza lake la vijana (BAVICHA) wenye lengo la kuhamasisha kupatikana kwa katiba mpya ya nchi hiyo.

Mara baada ya kuingia madarakani mwezi Machi mwaka huu, Rais Samia alitangazia umma dhamira yake ya kukutana na wapinzani ili kuzungumzia maswala mbalimbali ikiwemo ya kisiasa na namna gani ya kuendesha shughuli za siasa.

Licha ya kukutana na makundi mengine kama vijana, wazee na wanawake mpaka sasa Rais Samia hajakutaa na wapinzani. ''Hatuwezi kuendelea na ule utaratibu wa zamani, tuna haki ya kukutana tunakamatwa, tunapigwa, tunashitakiwa, tunasoteshwa mahakamani miaka miwili miaka mitatu, kisha tunaachiwa huru, ama tunahukumiwa vifungo batili tukikata rufaa sote tunashinda', alisema Mbowe
Pamoja na polisi kuzuia mkutano huo uliokua ufanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Boma wiki hii na kukamata watu hao 38, Kiongozi huyo wa Upinzani alisema, mkutano upo pale pale na utafanyika wiki hii na kama kukamatwa wako tayari kukamatwa wote.

Kama wanataka kuwaweka ndani wanachadema kwenye hoja hii ya katiba, wapanue kwanza na magereza, kwa sababu tuko tayari wote tuwekwe ndani , na wala hatutaomba dhamana' alisema Mbowe kabla ya kulaani kitendo cha Jeshi la Polisi Mwanza, kuwakamata viongozi wa dini na wafuasi wa chama hicho .

Chanzo: BBC Swahili
LHRC mbona hawajasema sabaya nae aachiwe?
Wasubili vyombo vifanye kazi kwanza
 
CCM wanataka Mama atengwe na mataifa...kisa uroho wa madaraka wa CCM.

Washanza kupigiana kura 2025 urais..mama awamu ni moja.

CCM mafia
 
Kuna watu wanaamini hivyo na ukiwaambia tofauti na hivyo ni ugomvi, kwahiyo inabidi tuheshimu tu imani za watu utafanyaje sasa?
Maana ukimuuliza sababu za msingi zilizomfanya kufikiri kuwa Jiwe kafa na corona? hana hizo sababu zaidi ya kukwambia aliidharau corona. Kwahiyo unaacha tu maana kama nafsi yake mwenyewe inafarijika kwa yeye kuamini kuwa Jiwe kafa kwa corona basi unamuachia imani yake ajifurahishe.
Corona is really

FB_IMG_1634495256250.jpg
 
Hadi sasa CIA wapo katika hatua za mwisho za kuianza mission "SAVE MBOWE FROM ASSASINS"!!!nasubiria kwa hamu sana!!!
 
Kwa nchi zinazopigana kuutokomeza UGAIDI duniani wakifuatilia hii kesi wanatuona sisi hamnazo kabisa.
 
Back
Top Bottom