Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,922
- 3,252
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Fulgence Massawe ametoa wito kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), kujitokeza hadharani na kuwahakikishia wadau kuwa uchaguzi utakuwa huru na wa haki.
Massawe ametoa wito huo leo Julai 24, katika mahojiano katika kipindi cha Maswali na Majibu kinachorushwa na Jambo TV, akisema mara kwa mara, hakikisho la uchaguzi ulio huru na wa haki hutolewa na Serikali ambayo nayo inagombea, huku tume ikiwa kimya.