LHRC, TLS, Dk. Slaa wamfungulia Kesi ya Kikatiba Waziri Katambi kupinga amri ya kuzuia Mikutano ya Hadhara ya Kisiasa

LHRC, TLS, Dk. Slaa wamfungulia Kesi ya Kikatiba Waziri Katambi kupinga amri ya kuzuia Mikutano ya Hadhara ya Kisiasa

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
524
Reaction score
829
photo_2026-07-16_10-44-28.jpg

Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kwa kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na mwanasiasa maarufu, Dk Willbroad Slaa, wamefungua kesi ya kikatiba dhidi ya Waziri wa Mambo ya Naani ya Nchi, Patrobas Katambi na wenzake sita.

TLS na wenzake wamefungua kesi hiyo Mahakama Kuu, Masjala Noogo Tabora, chini ya hati ya dharura wakipinga kauli aliyoitoa bungeni hivi karibuni kuhusiana na zuio la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.

Mbali na Katambi, aliyeshtakiwa kwa jina lake, wadaiwa wengine katika kesi hiyo ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Pia, wamewaunganisha wadhamini waliosajiliwa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wadhamini waliosajiliwa wa chama cha ACT- Wazalendo.



Juni 26, 2026, akiwa bungeni jijini Dodoma wakati vikao vya Bunge vikiendelea, Waziri katambi alipiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa nchini kote kwa kile alichoeleza ni sababu za kiusalama, akamuelekeza IGP kutekeleza agizo hilo.

Zuio hilo, pia, liliwekewa msisitizo na Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba ambaye ni kiongozi wa shughuli za Serikali, akiwa katika moja ya ziara zake mkoani Singida.

Kwa mujibu wa walalamikaji, agizo hilo limeanza kutekelezwa na IGP na wasaidizi wake, maofisa au wakala wake.

Wanadai kuwa kauli na maelekezo hayo ni ya kibaguzi na yanakiuka Katiba hasa Ibara za 12, 13(1) (2) na (4) na 29(1) na (2) na zinaingilia uhuru wa kikatiba wa kujieleza kutoa maoni na mawasiliano zinazohifadhiwa na Katiba Ibara ya 18 na uhuru wa raia kushiriki katika masuala ya umma kinyume cha Ibara ya 21(1) na (2) ya Katiba.

Wanadai kuwa Katambi wala Waziri wa Mambo ya Ndani hawana mamlaka ya kikatiba kuzuia haki za kikatiba zinazotolewa na Katiba.

Hivyo, wanaiomba Mahakama itamke kuwa kauli alizozitoa Katambi katika wadhifa wake wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kuzuia mikutano inayoandaliwa na vyama vya siasa kikiwemo Chadema na ACT-Wazalendi, zinakiuka Katiba huku wakibainisha ibara mbalimbali.

Pia, wanaiomba Mahakama itamke kuwa si Katambi wala Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye ana mamlaka ya kikatiba wala ya kisheria kuzuia haki hizo za kikatiba.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa na jopo la majaji watatu, Isaya Arufani (kiongozi wa jopo) Ilvin Mugeta na Martha Mpaze.

Via: Mwananchi
 
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimemfungulia kesi ya kikatiba Waziri wa Mambo ya Ndani kutokana na kutoa amri ya kuzuia mikutano ya hadhara ya kisiasa.​

Kwa mujibu wa LHRC, amri hiyo haina msingi wa kisheria na haikubaliki katika nchi zinazozingatia misingi ya demokrasia.
Hii ni hatua nzuri katika nchi ya kistaarabu inayofuata utawala wa sheria. Tatizo la uongozi wa sasa ni kwamba sio wastaarabu katika kufuata utawala wa sheria.Sintashangaa LHRC walipofungua shauri tu tayari maagizo yametolewa toka juu jaji yupi asikilize hii kesi na atoe uamuzi gani
 
Hii ni hatua nzuri katika nchi ya kistaarabu inayofuata utawala wa sheria. Tatizo la uongozi wa sasa ni kwamba sio wastaarabu katika kufuata utawala wa sheria.Sintashangaa LHRC walipofungua shauri tu tayari maagizo yametolewa jaji yupi asikilize hii kesi na atoe uamuzi gani
Aliimba mama mmoja😀unia lukumbalukumba!
 
ACT(CCM B ) NA CHADEMA wamezuiwa kufanya mikutano, ila Waziri wa serikali ya mchongo mkuu, yeye anaendelea na ziara zake na chama chake!

Hii nchi aisee!

Ingalikuwa KUMILIKI SILAHA BINAFSI KUWA NI SWALA LA KAWAIDA KAMA R.S.A AMA U.S.A HIZI MBWA ZINGENYOOKA!
 

Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kwa kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na mwanasia

Via: Mwananchi
Yaani kuna kakundi utadhani nchi hii ni ya kwao tuu kazi yao ni kutoa maagizo.
Taabu naiona kwenye mahakama zetu maana wamegeuka kuwa kama parking lots za magari.
 
Hii ni hatua nzuri katika nchi ya kistaarabu inayofuata utawala wa sheria. Tatizo la uongozi wa sasa ni kwamba sio wastaarabu katika kufuata utawala wa sheria.Sintashangaa LHRC walipofungua shauri tu tayari maagizo yametolewa toka juu jaji yupi asikilize hii kesi na atoe uamuzi gani
Ndipo tulipofikishwa yaani imekuwa ngumu sana kuona utendaji uliotukuka wa mihili ya utawala wa nchi hii
 
Katibu Mkuu Mstaafu wa CHADEMA Taifa na aliyewahi kuwa Balozi wa Canada, Dkt. Wilbroad Slaa hii leo Julai 16, 2026 akizungumza na Wanahabari amesema ameamuwa kuungana na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) pamoja na Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC) kufungua kesi dhidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katambi pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Wambura kwa kufungia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.

Aidha, Dkt. Slaa amesema tamko hilo limevunja Katiba kwa kuwanyima wananchi haki zao za msingi.
 
Back
Top Bottom