LHRC: Wakuu wa Wilaya hawana mamlaka ya Kipolisi kutoa amri ya raia kuwekwa ndani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Akitoa taarifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini, Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Wakili Fulgence Massawe, amesema kuwa kumekuwa na ongezeko la matumizi mabaya ya madaraka kwa baadhi ya viongozi, hususan wa kisiasa.

Ametolea mfano tukio la hivi karibuni la Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti, ambaye aliagiza watu aliowadai kuwa walikuwa wanauza na kununua viwanja wawekwe ndani.

Your browser is not able to display this video.

Amesema kuwa amri hiyo ilikuwa kinyume na sheria, akisisitiza kwamba Mkuu wa Wilaya hana mamlaka ya kutoa amri ya watu kuwekwa ndani, hususan katika masuala ya jinai, kwa kuwa hana vyombo vya kufanya upelelezi.

“Ni msimamo wa LHRC kwamba wakuu wa wilaya hawana mamlaka ya kipolisi kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai na Sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi Wasaidizi. Inafahamika kwamba vipo vyombo vya kikatiba, ikiwemo Jeshi la Polisi, vilivyopewa mamlaka ya kushughulikia masuala ya jinai, na si Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa au Waziri. Hii ni kutokana na ukweli kwamba Mkuu wa Wilaya au Mkoa hana vyombo vya kiupelelezi au kiuchunguzi,” amesema Massawe.





​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…