Naipendatz
JF-Expert Member
- Jul 27, 2011
- 5,096
- 8,234
Kituo cha sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimekumbusha Serikali ya Tanzania kubadili uamuzi wake wa kujitoa katika Mahakama ya Afrika na kurejea kwenye Mahakama hiyo ili kuimarisha heshima ya Taifa katika uwanda na kikanda.
Novemba 21, 2019 Serikali ya Tanzania ilifanya uamuzi wa kujitoa katika ibara ya 34(6) ya Mkataba wa nyongeza wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu uliokuwa ukiruhusu mtu au taasisi yoyote kuifikia Mahakama ya Afrika kudai haki.
Tanzania imekuwa nchi ya pili baada ya Rwanda kujitoa katika mkataba huo unaoruhusu mtu au taasisi kufungua kesi dhidi ya serikali pale ambapo kuna malalamiko ya kuvunjiwa haki yake.
Akizungumza na waandishi leo Oktoba 22, 2021 kuhusu maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Afrika ambayo hufanyika Oktoba 21, kila mwaka, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga, wanaona Tanzania inaweza kurudi katika mkataba huo na kuruhusu wananchi kufikia Mahakama hiyo na kupata mustakabadhi wa haki zao.
"LHRC inapenda kutumia maadhimisho haya kutoa wito kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia upya uamuzi wake wa kujitoa katika mkataba huo kwani itarudisha na kuimarisha heshima ya Jamhuri katika uwanda wa kikanda.
"Kumekuwa na dhana pamoja na tafsiri isiyo sahihi kwamba, watu waliyofungua kesi katika Mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu na Watu hawana nia nzuri na serikali baali wanataka kuichafua.
“LHRC inapenda kusahihisha dhana pamoja na tafsiri hiyo kuwa ni ishara ya kuimarika kwa demokrasia, ufikiaji wa haki, uvumilivu, na uongozi bora unaonyeshwa na Serikali," amesema.
Ameongeza kuwa wanaamini kwamba muundo wa Mahakama hiyo iliyopo Arusha ni wenye watu wanaojua misingi ya kiafrika, tamaduni, taratibu za sheria pamoja na mazingira, hivyo maamuzi yanayotolewa ni maamuzi ya haki na usawa.
Mwananchi