Elections 2015 Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!



Kwa kuongezea Lowassa ni mwenyekiti wa kamati ya katiba na bunge lakini vikao hauhudhurii ingawaje analipwa! Kamwachia fisadi mwenzie Ngeleja akaimu! Kwa sasa hahudhurii vikao anadai anaumwa lakini kujipigia debe mtaani haumwi. Uroho wa madaraka wa mzee fisi.
 
Pasco..kwanza nieleze wazi kuwa Lowassa huwa anatumia nguvu nyingi sana kujipendezesha apendwe. Ni kweli patachimbika kwa maana wafadhili wamewekeza sana kwake ili tu waweze kuvuna kikubwa pale atakapofanikiwa URAIS..(King Makers). Nafahamu wajua ubaya wa King Makers..lazima warudishe gharama zao kwanza ndo uanze kuhudumia wananchi. Lakini kingine EL hapendi pamoja na maamuzi yake magumu na uelewa wake mzuri wa Nchi yetu hii kwa nini hapeni kulaani au kutoa miongozo juu ya hii hali ya UFISADI ambayo ndio tatizo kubwa sana kwa maendeleo ya Vijana na Nchi kwa ujumla. Msaidie kujibu tuweze kumpenda zaidi. Mwisho ndani ya CCM yangu wasafi hawatakiwi kushika madaraka na wenyewe pia (wasafi) wanayaogopa sanaaa madaraka.
 
haitoshi kujisafisha
 
Kama ufisadi hata aliyeko madarakani sasa ni fisadi au hamuoni?
Nyerere amekaa madarakani mika 25 sijawahi hata siku moja kusikia Makongolo Nyerere ni tajiri, lkini huyu miaka mitatu tu Ridhiwani Kikwete milionea kazipata wapi kama sio ufisadi wa familia?
Lowassa atapeta tu.
 
Natamani nione CCM wenye "balls" za kumtoa Lowassa
 
Hakuna cha Lowassa, Pinda, Membe wala yeyote katika wale waliopewa adhabu.
Mgombea wa ccm atakuwa mtu ambaye wala hatajwi kwa wakati huu.
Miaka kumi inayomalizika imetosha. Vyama vyetu ni kama magari mabovu. Sitajali Rais anatoka wapi bora awe muadilifu.
Tunahitaji Levy Mwanawasa wetu ili awafunge mafisi.
 

Mkuu ukisikia baadhi ya watu wengine wanafoka sana wakimshambulia Lowassa sio kwamba wanataka mtendaji safi bali wapo kimaslahi zaidi kwa huyo au yule wanaetaka awajaze mapesa.
 
Mimi mwenyewe CCM ndakindaki na katika kitu naomba ni Lowassa akatwe asiwe Rais. Waheshimiwa hakikisheni Lowassa hafiki popote.

Akatwe abakishwe nani? Membe? Pinda? January? Mwigulu? Sita? MNA utani nyie... Kama hatumpi Dr Slaa hii nchi ni bora huyo Laigwanani, hao wengine watokao ndani ya ccm ni majanga matupu
 
Mimi naona mngetupumzisha na habari za mtu huyu ili bongo ziweze kufikiri walau kuhusu wengine.
 

Si Ishara nzuri muda ni mfupi wananchi kumchunguza ,wakati mwigine waweza ukauziwa mbuzi kwenye gunia.
 
Si Ishara nzuri muda ni mfupi wananchi kumchunguza ,wakati mwigine waweza ukauziwa mbuzi kwenye gunia.

Mkuu, unayo hoja ya msingi lakini hatua tuliyofikia, bora tupate watu wengine tuwapime hata kwa huo mwezi mmoja. Naamini hawatakuwa wageni kabisa. Wanafahamika kwenye utumishi wao sehemu mbalimbali.

Watu waadilifu wapo lakini ni vigumu kujitokeza katika mazingira tuliyonayo nchini mwetu kwa sasa. Mafisi ndio wapo kimbelembele utafikiri kuna mzoga mahali. Hao wakifanikiwa nchi nzima wataifanya mzoga!
 

Tunapita wakati mgumu.Ebu tusubili mwali
 
pole sana ndugu mwanaccm pasco , bila shaka lowasa ataondolewa lakini hii haitaokoa chama chako , rais wa nchi hii atatoka UKAWA , jk ndio kiongozi wa mwisho kutokea kwenye chama kichakavu .
 
Kwa taarifa yako hakuna atakayekata jina la lowassa kwa misingi ipi? hiyo hofu toa kabisa wananchi tutavamia hiyo kamati
 
Kwa kuwa umesema ni tetesi sisemi kitu maana hizo ni ndoto ambazo huja usingizini baada ya mtu kuwaza sana mchana juu ya hizo. Asubuhi njema Pasco.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…