Elections 2015 Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!

Elections 2015 Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!

Kama watu kama Pasco ndio washauri wa Lowasa, basi jina lake lazima lichujwe kwenye kamati ya maadili kwani wameshindwa hata kumshauri jinsi bora ya kuongeza umaarufu wake zaidi ya kuwanunua "masheikh, wachungaji, madereva wa bodaboda, na wanachuo" feki na kuishia kupata fedheha badala ya umaarufu.

Kama kungekuwa kuna kiwango cha chini (minimum qualification) za kuchangia hapa jukwaani, hakika makanjanja kama Pasco wasingepata nafasi za kuchangia.
 
Me sioni kama kuna mtu anafaa kuongiza nchi hii

Bora tukose wote na kukinusuru chama kisimeguke vipande.CCM wanalijua hilo watateua wanawake,Sitashangaa Spika Makinda au Waziri Migiro kuwa finalist kwa tiketi ya CCM.
 
Wanabodi,

Hii ni tetesi ya habari mbaya kwa wapenzi wa kipenzi cha watu, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kuwa pamoja na Mhe. Lowassa kuwa ndie mtu anayekubalika sana kuliko mtu mwingine yoyote ndani ya CCM, wale wasiolitakia mema taifa hili, wamepania kupanga njama za kumhujumu kwa kuhakikisha kuwa jina lake halitaingia hata ndani ya kikao cha CC kujadiliwa!, wamepanga kumchinjia baharini kwenye kamati ya maadili, itakayoyajadili majina wagombea kabla ya kuyaingiza kwenye Kamati Kuu, kujadiliwa!.

Lengo la hujuma hiyo ni kufuatia Lowassa kukubalika kupindukia, jina lake likifika tuu CC, hakuna wa kumkata, hivyo wahafidhina wa CCM, wanaounga mkono kambi ya mmoja wa wagombea, wameapa kuhakikisha jina la Lowassa, halivuki kisingiti cha kamati ya maadili, hivyo kumchinjia rasmi baharini, ili mgombea wao apete kwa mteremko!.

Naomba nisitaje chanzo cha habari hizi, kwa kutumia kanuni ya "the confidentiality of the source"
ila kwa vile hizi ni tetesi tuu, zitakapothibitika ndipo nitaweka source!.

Kama kawaida yetu jf, habari kama hizi ambazo hazijathibitishwa, zimeletwa humu hivi hivi zilivyopokelewa, ili wewe kama mwana jf, be the first to know!, na information is power!, hivyo kutoa fursa kwa wenye uwezo wa kuizuia hii mipango dhalimu inayopangwa, kutaka kuwakosesha Watanzaia mgombea kipenzi chao, chaguo la wengi, na mwenye uwezo usio tia shaka kuyamaliza matatizo yote ya taifa letu Tanzania.

Hii ni thread ya info tip, tuu, hivyo naomba nisiulizwe swali lolote kuhusu hii news tip for your info tuu.

NB. Chama cha Mapinduzi ni taasisi huru yenye uwezo wa kufanya shughuli zake kwa uhuru vile ambavyo wataona wenyewe inafaa, ikiwemo vigezo na jinsi ya kuwachagua wagombea wake, ila kwa sisi ambao ni wakereketwa wa mustakali mwema wa nchi hii, kamwe hatutakubali, kuona watu wenye uwezo na wanaokubalika na wengi, wakienguliwa kwa mizengwe tuu, kitu ambacho CCM imekuwa ikikifanya mara nyingu huko nyuma na labda ni kweli ndicho walichopanga kukifanya mwaka huu!, yaani CCM imekuwa ikiwaengua wagombea wazuri kwa mizengwe na ikabaki salama!, lakini this time, nimewasikia baadhi ya wana CCM kindakindaki, kuwa wamejiapiza, this time CCM ikimuengua chaguo lao kwa mizengwe, patachimbika!.

Pasco
Haya mameno yako kwenye para ya mwisho kamtishe demu wako ya wa kingoni siyo watu wenye akili zao bana.
 
Lowassa ni mwizi hafai kuwa kiongozi. Lowassa ni fisadi hafai kuwa kiongozi, huko kupendwa na wengi siyo bali ananunua kupedwa

Anapendwa na wengi wangapi? Acheni ubabaishaji. Kama atapita CCM basi tusubiri tuone october kama kweli anapendwa na wengi!
 
Sasa kamati ya maadili kama itapitia kwa haki sizani kama huyo mzee wenu atapita..alikosA maadaili awamu iliyopita kwa dhamana ndogo aliyoachiwa akashindwa ndio ataweza hii dhamana kubwa?!!au ule nao ulikuwa mpango wa kukwamisha mbio zake za uraisi..#watanzania tusiwe vigeu geu!!!
 
Safari yetu ya Matumaini haiwezi kuzuiliwa na watu wanao ropoka na kubwabwaja hovyo, ndio maana huwa tunawapuuza kwani tukiwajibu tutakua tumewapa heshima. Mh Lowasa ndio chaguo la wengi na tumaini la watanzania.
 
MWEKUNDU wewe ni kiziwi? si alisha mwambia mwenyekiti nini hujui? au wewe sio mtu mzima?Mtu mzima ukiambiwa sio lazima ujibu unaweza guna au kukohoa ina maana ndiyo.Natumaini umepata jibu,kama sivyo uliza wajumbe wa kamati kuu ya chama chako/au nje nkapa

Tulioibiwa ni sisi wadanganyika au mwenyekiti?? Mzalendo huwaga msema kweli! au ndo historia itamhukumu??

[TABLE="width: 608"]
[TR]
[TD]
Ufisadi ni ajali ya kisiasa?



[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Ansbert Ngurumo
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]


WIKI hii, kuna mtu amejitambulisha kwangu kama msomaji mwaminifu wa safu hii; na amenitania akisema:
“Mzee wa Maswali Magumu… naona umekuwa kiongozi wa uasi dhidi ya kauli za wakubwa. Matunda ya kazi yako na wengine tumeanza kuyaona. Endelea… nchi yetu inahitaji ukombozi wa kifikra. Sasa tumegundua kuwa akina ‘ndiyo mzee’ wanachangia kuizamisha nchi yetu kwenye ufisadi…”
Kwangu, haya ni maneno mazito sana. Yanatoka kwa mtu nisiyemfahamu. Yanaweza kupata tafsiri zaidi ya 100 kutoka kwa watu mbalimbali.
Tungeweza kujadili na kuchambua kwa kirefu maneno kadhaa katika kauli hiyo, kwa mfano, uasi, kauli za wakubwa, matunda yaliyopatikana, ukombozi wa kifikra, kina ndiyo mzee, ufisadi na mengineyo yanayojitokeza kwenye ujumbe huu nliotumiwa.
Lakini msingi mkuu wa ujumbe huu ni mmoja. Na unaweza kuelezwa kwa neno moja - uasi.
Wakati umefika, Watanzania wanapaswa wajifunze kuasi. Si uasi wa hovyo hovyo, bali uasi katika mambo ya msingi; uasi unaoonyesha kwamba wamekua; wamekomaa.
Watanzania wanahitaji kuonyesha kwamba sasa wanajua; wafanye uasi unaoonyesha kwamba sasa wapo tayari. Ndiyo ishara ya kuonyesha kuwa wamechukia, na wanaweza kuchukua hatua.
Uasi wa wananchi ndiyo umejitokeza katika ripoti ya Kamati ya Bunge iliyokuwa inaichunguza kampuni ya kitapeli ya Richmond. Bila uasi, Bunge lisingeunda kamati hiyo.
Ndiyo! Wakati wa kushangilia makosa ya wakubwa umepita. Hizi ni zama za uasi dhidi ya utawala mbovu unaoambatana na matumizi mabaya ya madaraka. Ni uasi dhidi ya ufisadi.
Watanzania wameanza kuasi. Wabunge wameanza kuasi. Nchi imechangamka. Viongozi bado wamezubaa; hawajui kinachoendelea!
Na faida mojawapo ya uasi huu imeonekana wiki iliyopita. Mawaziri wamejiuzulu, na Baraza la Mawaziri limevunjwa. Kama tungekuwa watiifu, kina ‘ndiyo mzee,’ nina hakika hili lisigetokea.
Ndiyo! Nakubali. Uasi wa Watanzania umeanza kuzaa matunda. Juzi waliwazomea mawaziri wa Kikwete; jana wameshangilia anguko lao. Leo wana kazi nyingine; kesho ni mapinduzi. Huu ni mwanzo, si mwisho.
Sasa Rais Kikwete amesikia, kinyume cha matarajio yake, kwamba nguvu ya wananchi imeshinda. Wananchi wamethibitisha kuwa ‘kelele za mlango’ zinaweza kumzuia mwenye nyumba kulala.
Lakini kuna jambo bado linanipa wasiwasi. Mwenye nyumba wetu (Kikwete) hajapata tafsiri sahihi ya kishindo cha nguvu ya umma. Walau hadi Alhamisi wiki hii, alipokuwa anawahutubia wazee wa Dar es Salaam, alikuwa hajatambua hisia halisi za Watanzania.
Vinginevyo, angeepuka kabisa kuwamwagia sifa kemkem mawaziri waliolazimishwa kujiuzulu kwa sababu ya tuhuma za ufisadi. Walau asingewataja kwa majina, kuwasifu na kuwasikitikia.
Zaidi ya hayo, asingewaita “waadilifu, wazalendo na waaminifu” katika mazingira ambayo ‘kila mtu’ anajadili ufisadi wao. Kwa hili, Kikwete amejitenga na Watanzania. Maneno haya yamemchafua.
Watanzania wanashangilia anguko la ‘mafisadi,’ huku baadhi yao wakidhani rais yuko upande wa wananchi; kumbe mwenzao yuko kambi nyingine kabisa. Anaonyesha masikitiko ya wazi.
Hivi hakujiuliza kwa nini wananchi nchi nzima walishangilia sana kujiuzulu kwa mawaziri wake, hasa waziri mkuu? Na alipozitazama nyuso za wazee alikuwa anawahutubia aliona wanakubaliana naye? Mwitikio alioutarajia ndio waliompa?
Kwa maneno haya, hata waliokuwa wameanza kudhani kwamba Kikwete alishirikiana na Spika wa Bunge, Samwel Sitta kuitumia Kamati ya Bunge kama njia ya ‘kuondokana’ na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, wamepata jibu.
Wao walidhani kwamba isingekuwa rahisi kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Dk. Harrison Mwakyembe, kuwa jasiri na muwazi hivyo, bila kuwa na baraka za Rais Kikwete. Walikosea. Katika zama za uasi mtakatifu kama huu, hilo linawezekana.
Bahati mbaya, walichelewa kujua msimamo wa Rais Kikwete kuhusu suala la Richmond; kwamba katika hili yuko na Lowassa.
Yeye mwenyewe anabaki kuwashangaa wabunge na wananchi wanaowazomea na kuwashindilia maneno mazito watuhumiwa wa Richmond, hata baada ya kujiuzulu. Kikwete haoni ufisadi wa Lowassa katika suala hili.
Bahati nzuri ametamka mwenyewe kile anachokiona kwa Lowassa – ajali ya kisiasa! Ni sababu hiyo hiyo iliyonifanya niandike Jumapili iliyopita kwamba, Lowassa amebeba mzigo wa Kikwete.
Nilisema Lowassa hakufanya uamuzi wa kuibeba Richmond peke yake. Ndiyo maana aliweza kujiamini, na hakuchukuliwa hatua yoyote kwa miaka miwili hadi Bunge lilipoamua kufanya uasi kwa kuitikia nguvu na kauli ya wananchi.
Na hii kauli ya juzi ya Rais Kikwete (kwamba hii ni ajali tu ya kisiasa), ni kichocheo kingine cha uasi wa Watanzania ambao unakuja. Ndiyo maana baadhi yetu hatubaki tu kushangilia na kupigia makofi hotuba za rais.
Tunajua kwamba katika kauli zake nyingi, ukweli unawekwa pembeni, propaganda inatangulizwa, ili kuwahadaa au kuwapoza wananchi. Ni maneno mengi, matamu; hakuna hatua. Na hatua zinapokuwapo, hazilingani na maneno yaliyotamkwa.
Nitatoa mfano wa hivi karibuni. Mwishoni mwa Januari, Rais Kikwete alilihutubia taifa akidokeza ubaya wa kuwa na mawaziri na wabunge wafanyabiashara. Alidokeza kwamba ataanzisha mchakato wa kisheria ili kuhakikisha wenye biashara wanakaa mbali na madaraka ya kisiasa.
Kina ‘ndiyo mzee’ waliwahi kupiga makofi. Tena baadhi ya waandishi wakasema sasa ‘tunarejea enzi za Azimio la Arusha.’ Wengine wakathubutu kusema ‘sasa Kikwete kawa Nyerere!’
Wanaolijua Azimio la Arusha vizuri, na wanaomfahamu fika Julius Kambarage Nyerere, wataendelea kuiona hii kuwa ni kufuru!
Baada ya ripoti ya Mwakyembe kuja na mapendekezo kadhaa, mojawapo likifanana na hilo alilotoa Kikwete juu ya wanasiasa wafanyabiashara, baadhi ya wadadisi wa mambo wakasema: “Kikwete alipata taarifa za kikachero kuhusu ripoti ya Mwakyembe kabla haijawasilishwa bungeni, akalichomoa hilo ili kupoza machungu ya wananchi wanaomlaani kwa kuiuza nchi kwa rafiki zake wafanyabiashara, ambao naye aliona kwamba mwisho wao serikalini unakaribia, ingawa hakujua mwisho wao ungekuja lini na kwa namna gani.”
Baadhi yetu tulitarajia kwamba maswali tuliyomhoji yangemsaidia kutuonyesha alivyo makini. Fursa ya kuonyesha umakini alikuwa nayo hasa baada ya Lowassa kumsaidia kuvunja baraza.
Alipounda upya baraza lake na kuwatangaza wateule wapya, sikuona waziri asiye ‘mfanyabiashara.’ Lakini wale waliokuwa wanadhani kuwa mfanyabiashara lazima afanane na Nazir Karamagi au Rostam Aziz, au hata Lowassa, wakasema “ameunda baraza lisilo na wafanyabiashara.” Kweli?
Kwani mfanyabiashara ni nani? Mfuga kuku? Mwenye mashamba ya tumbaku au miwa? Mmiliki wa daladala? Mmiliki wa shule binafsi? Mwenye mgodi wa dhahabu? Mwenye hisa katika kiwanda chochote? Mwenye duka la mitumba au bidhaa zozote? Mwenye saluni ya urembo? Mwenye kampuni yoyote binafsi? Ni nani huyo mfanyabiashara tunayemlenga, au anayezungumzwa na Kikwete? Mbona ndio hao wamejaa kwenye baraza jipya la mawaziri?
Lakini hoja yangu mimi ni tofauti. Sichukii wafanyabiashara wanasiasa. Sikubaliani na Kikwete (na wanaofanana naye katika hili) kwamba wafanyabiashara wasiwe wanasiasa au wanasiasa wasiwe wafanyabiashara.
Sitaki wanasiasa malofa na ombaomba ambao ni rahisi kutumiwa na wenye pesa. Wao hawatakuwa wafanyabiashara, lakini watawatumikia ‘wafadhili’ wao na njaa zao. Tunayo mifano mingi ya wafanyabiashara waliowatumia wanasiasa baada ya kufadhili kampeni zao na kuhakikisha ushindi wao.
Wako mbali kabisa na Ikulu, wizara na Bunge. Lakini wana nguvu kuliko mawaziri na wabunge wenyewe. Kisa? Pesa yao.
Hatujasahau yanayosemwa kuhusu mzozo wa mradi wa makaa ya mawe ya Mchuchuma na Liganga. Wanasiasa wametumika, na wanaendelea kutumika, kuuza rasilimali za taifa kwa wafadhili wao.
Hatutaki siasa zinazopendekezwa za kuwatumikia wafanyabiashara, bali tunataka biashara zinazotumikia siasa.
Wapo baadhi ya wafadhili wa CCM wasiopenda kujitaja, na wasiopenda kutajwa na mtu. Lakini vitabu vyao vya hundi vinawataja. Tunawajua. Wako karibu na wakubwa kwenye chama na serikali. Wao si wanasiasa wa waziwazi, ingawa dalili zipo kwamba wanazengea kuingia kwenye siasa.
Lakini kila tenda kubwa serikalini ikitangazwa, wamo! Wenye mahoteli wanapelekewa mikutano mikubwa mikubwa na yenye pesa nyingi za serikali. Wenye biashara za kuingiza bidhaa kutoka nje ya nchi, wanapewa upendeleo maalumu au msamaha wa kodi. Kisa? Ni wafadhili wa wakubwa.
Haya ndiyo mambo ambayo Kikwete alipaswa ayatazame na kuyafanyia kazi. Hawa ndio wafanyabiashara wanaokomaza ufisadi. Wanawatumia wanasiasa wetu, hasa hasa wale wenye njaa na tamaa.
Tunao wanasiasa wajanja wajanja na wakwepa kodi pia. Wengine wamejipenyeza pole pole kutoka kwenye ufadhili wa CCM na kuwa ‘vigogo’ wa chama. Baadhi yao wamo serikalini. Wengine ni aibu ya rais mwenyewe; na wengine ni aibu kwa taifa. Ni mzigo!
Baadhi yao wamekuwa na biashara zao huko nyuma, lakini zimekua kwa kasi katika miaka ya karibuni, hasa katika kipindi ambacho mabilioni yamechotwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania, wakiwa karibu na wakubwa!
Wengine, tena katika miaka miwili iliyopita, waliteuliwa kuongoza wizara zenye uhusiano wa moja kwa moja na biashara zao au za ndugu zao. Njia ya kuwandoa hawa na kuwazuia wengine kuwa kama wao ipo, lakini si kuharamisha biashara.
Kelele alizodhamiria kuzipoza Rais Kikwete zina mizizi yake. Hoja isiwe biashara ya mtu, bali uadilifu unaoambatana na biashara ya mtu; na uhusiano wake na wakubwa serikalini.
Kuwanyanyapaa wafanyabiashara kwa sababu tu ya biashara zao ni kuwaonea wivu, na ni ujinga. Ni udhaifu wa kushindwa kuona tatizo halisi. Au labda ni ujanja wa kuwasaidia wafanyabiashara ambao baada ya kuwa serikalini kwa muda sasa, wameamua kujiweka mbali ili kufanya mambo yao gizani.
Wakiwa nje ya serikali, wanajielekezea mifereji ya rasilimali zetu, mithili ya wakoloni na uchumi wetu tegemezi. Waliondoka, lakini ndio wanaofaidi rasilimali zetu wakiwa kwao Ulaya na kwingineko.
Na hata wanaporejea, hawaitwi wakoloni, bali wawekezaji. Wanapewa viti vya mbele; wanatukuzwa na watawala wetu wale wale wanaojivunia ‘uhuru’ wa nchi yetu!
Dhamira ‘nzuri’ ya Kikwete imekuja wakati usio wake. Hata akipunguza tena ukubwa wa baraza, ni vigumu kuwapata mawaziri 20 au 15 wasio wafanyabiashara.
Kwa hali ilivyo sasa, ni vigumu kuwa na viongozi na washauri wao wasio wafanyabiashara. Uteuzi wake wa juzi, umeonyesha kwamba hiyo ndoto atakufa nayo.
Ni vema atambue kuwa dunia ya sasa na tunayoiendea, ni dunia ya biashara. Wakati ujao ni wa biashara. Tunachohitaji si kuwanyanyapaa wafanyabiashara, bali kutafuta njia na sera mwafaka za kuhakikisha biashara hizi zinatumika kulinufaisha taifa.
Tuondoe na kudhibiti migongano ya kimaslahi katika biashara za wanasiasa wetu. Rais atumie vizuri mamlaka yake ya uteuzi kuhakikisha hashiriki kuuza nchi kwa wafanyabiashara wasio waaminifu.
Lakini atambue pia kuwa kimsingi, ufumbuzi halisi wa tatizo hili ni vema uwe wa kikatiba kuliko tu wa kisheria na hisia.
Ni dhana inayopaswa ijadiliwe kwa upana wake, si kwa mtazamo wa Azimio la Arusha, ambalo halipo; wala Azimio la Zanzibar, la kijambazi ambalo halijafutwa; bali kwa kuzingatia mahitaji halisi ya kitaifa, si ya watawala peke yao.
Na hata litakapoletwa, lisifanywe tu ajenda ya propaganda za walio madarakani, katika jaribio la kujikosha na ufisadi.
Litekelezwe kwa kuzingatia visheni pana ya kitaifa, na vita dhidi ya ufisadi, si kwa nia ya kuepusha ‘ajali za kisiasa’ za wakati huu.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Wanabodi,

Hii ni tetesi ya habari mbaya kwa wapenzi wa kipenzi cha watu, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kuwa pamoja na Mhe. Lowassa kuwa ndie mtu anayekubalika sana kuliko mtu mwingine yoyote ndani ya CCM, wale wasiolitakia mema taifa hili, wamepania kupanga njama za kumhujumu kwa kuhakikisha kuwa jina lake halitaingia hata ndani ya kikao cha CC kujadiliwa!, wamepanga kumchinjia baharini kwenye kamati ya maadili, itakayoyajadili majina wagombea kabla ya kuyaingiza kwenye Kamati Kuu, kujadiliwa!.

Lengo la hujuma hiyo ni kufuatia Lowassa kukubalika kupindukia, jina lake likifika tuu CC, hakuna wa kumkata, hivyo wahafidhina wa CCM, wanaounga mkono kambi ya mmoja wa wagombea, wameapa kuhakikisha jina la Lowassa, halivuki kisingiti cha kamati ya maadili, hivyo kumchinjia rasmi baharini, ili mgombea wao apete kwa mteremko!.

Naomba nisitaje chanzo cha habari hizi, kwa kutumia kanuni ya "the confidentiality of the source"
ila kwa vile hizi ni tetesi tuu, zitakapothibitika ndipo nitaweka source!.

Kama kawaida yetu jf, habari kama hizi ambazo hazijathibitishwa, zimeletwa humu hivi hivi zilivyopokelewa, ili wewe kama mwana jf, be the first to know!, na information is power!, hivyo kutoa fursa kwa wenye uwezo wa kuizuia hii mipango dhalimu inayopangwa, kutaka kuwakosesha Watanzaia mgombea kipenzi chao, chaguo la wengi, na mwenye uwezo usio tia shaka kuyamaliza matatizo yote ya taifa letu Tanzania.

Hii ni thread ya info tip, tuu, hivyo naomba nisiulizwe swali lolote kuhusu hii news tip for your info tuu.

NB. Chama cha Mapinduzi ni taasisi huru yenye uwezo wa kufanya shughuli zake kwa uhuru vile ambavyo wataona wenyewe inafaa, ikiwemo vigezo na jinsi ya kuwachagua wagombea wake, ila kwa sisi ambao ni wakereketwa wa mustakali mwema wa nchi hii, kamwe hatutakubali, kuona watu wenye uwezo na wanaokubalika na wengi, wakienguliwa kwa mizengwe tuu, kitu ambacho CCM imekuwa ikikifanya mara nyingu huko nyuma na labda ni kweli ndicho walichopanga kukifanya mwaka huu!, yaani CCM imekuwa ikiwaengua wagombea wazuri kwa mizengwe na ikabaki salama!, lakini this time, nimewasikia baadhi ya wana CCM kindakindaki, kuwa wamejiapiza, this time CCM ikimuengua chaguo lao kwa mizengwe, patachimbika!.

Pasco

Pasco, naona unapambana kwa kila hali..ahhhaaa...huyo jamaa yenu kwishnei hiyo ndo taarifa yako..
 
Safari yetu ya Matumaini haiwezi kuzuiliwa na watu wanao ropoka na kubwabwaja hovyo, ndio maana huwa tunawapuuza kwani tukiwajibu tutakua tumewapa heshima. Mh Lowasa ndio chaguo la wengi na tumaini la watanzania.

Safari ya matumaini ya kuifisadi zaidi Tanzania! Ndio maana watu wamekomaa na Lowasa kwa vile wanajua huyu jamaa akiwa rais basi wao watapata nafasi za kufisadi uchumi wa nchi yetu maana boss wao mwenyewe ni kubwa la mafisadi!
 
Kama CCM ni kamati ya maadili na wajaribu huo mchezo wao wa kitoto
 
ujanja wa samaki ni majini tu huyu lowasa aka mwizi mkuu wa taifa anatapa tapa tu kama yeye mwanaume atoke nje ya ccm
 
Hivi kaka Pasco unaamini hadi leo kuwa Edward Lowassa atakuwa Rais wa Tanzania? Kwa lipi hasa? Mtakuwa na madodoki na magunzi mangapi kumsafisha? Kuongozwa naye ni pigo kwa nchi na vita dhidi ya ufisadi

Ngoja uje ushangae kwamba hata huyo unaemshabikia kumbe nae ni shabiki namba moja wa EL
 
Last edited by a moderator:
Cyo kwel bwana Luriga....Labda tujadl issue zngne lakn issue ya urais Lowasa ndo mpango mzima.
 
Kumkata Lowassa ni kuua CCM.

Jiandae kwenda ACT Mkuu maana hawatamleta, kwa sababu wanaficha maovu yao. Hawataki kusikia mtu atakayetibua deal za wakubwa.

Kuna tetesi kuwa deal la Richond lilikuwa la Mkuu wa Kaya na EL kabebeshwa ili aokoe serikali, sasa kwa kuwa mission yao ilifanikiwa wakati ule na hawakupata Virus sasa wamelisahau kinga na kuona si cha maana tena.
 
Naomba niwaulize wanaccm hivi ni kipi lowasa kafanya kikwete hakufanya kipi kipya?

Sasa kwanini msianze na huyo ambaye yuko madalakani ili wengine wa aina yake wasiufikilie huo urais kwa sababu watajua kitachowatokea.

Kama kweli kikwete na ccm wote ni wasafi kwanini wanatumia dola kizima sauti za wanyonge?

Kuna babu mmoja mwanajeshi kaniambia wakati wa kudai uhuru mkoloni hakutumia nguvu kubwa kama hii wanatumia ccm katika kukandamiza wananchi wake na kinyima jaki zao.
 
Hivi kaka Pasco unaamini hadi leo kuwa Edward Lowassa atakuwa Rais wa Tanzania? Kwa lipi hasa? Mtakuwa na madodoki na magunzi mangapi kumsafisha? Kuongozwa naye ni pigo kwa nchi na vita dhidi ya ufisadi

Kwa historia ya ccm mara nyingi pale panapotokea kuwa wagombea wawili wanashindana na iwapo kumchagua mmoja wao kunaweza kuleta mpasuko ndani ya chama chao mara zote huwa wanawengua wahusika wote na kumteua mtu mwingine!!! Kama mtakumbuka katika uchaguzi wa Jimbo la Urambo huko nyuma kulitokea ushindani mkubwa na mbaya uliozua uhasama wa kisiasa unaodumu hadi leo kati ya Samuel Sitta na Juma Kapuya; ccm waliamua kuwatosa wote wawili na wakamteua Karavina kugombea ubunge wa jimbo hilo!!! Sintaona ajabu iwapo wote wawili Lowassa na Membe wakachinjiwa baharini!!!
 
Back
Top Bottom