BARAZA LA MAWAZIRI LA LOWASSA
- Waziri Mkuu Professor Juma Kapuya
- Waziri Maliasili na Utalii Mghana Msindai
- Waziri wa Nishati na Madini William Ngereja
- Bunge Sera na Uratibu Hamis Mgeja
- Wanawake na Watoto Sophia Simba
- Habari Michezo na Utamaduni Beatrice Shelukindo
Jazeni wengine, halafu eti hawa ndio tunategemea kutuletea mabadiliko Tanzania, utani mwingine umepitiliza!
Mkuu nakuhakikishia jina la Lowasa halitafika kwenye vikao vinavyoweza kulipitisha. Unafikiri nje ya hao wajumbe wake aliowanunua ndani ya ccm, nje ya ccm nguvu yake kisiasa ikoje? Anaweza kukimbia chama chake bado akatikisa kama ilivyokuwa kwa mrema? Usimlinganishe Kikwete na mkapa, Kikwete anazifahamu vyema siasa chafu anazocheza Lowasa, na bila shaka kesha andaa dawa yake...hivi Mkapa naye akiwa Raisi na Mwenyekiti wa CCM si alijiapiza kwamba atawakomesha wanamtandao?
..nini kilimtokea na dakika za mwisho kabisa akabadili msimamo na kumuunga mkono mgombea "anayependwa" na wananchi?
..najua CCM imepata kuwaengua watu wazito kama Cygwiyemwisi John Malecela, lakini sidhani kama Lowassa na wanaomuunga mkono are push overs kama Malecela.
cc Nyamizi, Pasco
Mkuu nakuhakikishia jina la Lowasa halitafika kwenye vikao vinavyoweza kulipitisha. Unafikiri nje ya hao wajumbe wake aliowanunua ndani ya ccm, nje ya ccm nguvu yake kisiasa ikoje? Anaweza kukimbia chama chake bado akatikisa kama ilivyokuwa kwa mrema? Usimlinganishe Kikwete na mkapa, Kikwete anazifahamu vyema siasa chafu anazocheza Lowasa, na bila shaka kesha andaa dawa yake.
Mbona kishamtupa kitambo! Muulize Pasco akueleze ni mara ngapi lowasa ameomba kukutana na Kikwete akashindwa. Hukushangaa alivyowaomba masheikh wake feki toka Bagamoyo wamfikishie ujumbe kwa mheshimiwa rais bila kujua kwamba alikuwa anaongeza mafuta kwenye moto aliotakiwa kuuzima?..mimi sidhani kama Kikwete anaweza kumtupa Lowassa.
..hawa wametoka mbali mno, tangu mwaka 95 na inawezakana kabla ya hapo.
..Lowassa ametoa mchango mkubwa sana kumfikisha Kikwete hapo alipo.
..hata ile kashfa ya Richmond, Lowassa took the hit kuwakinga wengine.
..kumbuka Dr.Mwakyembe alisema kuna mambo hawajayatoa ili kutoiabisha serikali. Lakini ripoti hiyo ilifikia mpaka kumuaibisha Waziri Mkuu, sasa huyo aliyefichiwa mambo yake alikuwa nani?
..Nakubali kwamba JK anazijua sana siasa za nchi hii, lakini sidhani kama ni mtu katili mwenye kuweza kumdhulumu mtu waliyetoka naye mbali na aliyemhangaikia kama Edward Lowassa.
cc Pasco
Mbona kishamtupa kitambo! Muulize Pasco akueleze ni mara ngapi lowasa ameomba kukutana na Kikwete akashindwa. Hukushangaa alivyowaomba masheikh wake feki toka Bagamoyo wamfikishie ujumbe kwa mheshimiwa rais bila kujua kwamba alikuwa anaongeza mafuta kwenye moto aliotakiwa kuuzima?
Mwaka huu tutavunja record nyingine duniani FISADI awe raisi ?Tanzania my country akitaka aupate uraisi namshauri EL awe muwazi atuaambie hadharani deal la Richmond alipiga na nani huko CCM hiko ndo kizingiti kinachomwangamiza
Ndiyo maana kwenye post #163 nimesema usimlinganishe mkapa na Kikwete. Tuombe uzima, Lowasa atatupwa nje ya kinyang'anyiro na atalazimishwa kumsapoti na kumfanyia kampeni atakayepitishwa na chama. Hatakuwa na chaguo isipokuwa kutekeleza...mbona mbinu hizi anazotumia Lowassa ndizo alizotumia JK kupata huo Uraisi.
..si ni huyu huyu JK aliyekuwa akichafua wenzake wakina Sumaye, Salim Ahmed Salim, kwenye vyombo vya habari?
..je, mmesahau tuhuma za wajumbe wa mkutano mkuu kanda ya ziwa kupewa bahasha wakati wakielekea Dodoma?
..pia mmesahau utetezi wa Lowassa kuhusu Richmond ktk kikao kilichoongozwa na JK, mpaka ikafikia Mzee Mkapa kuokoa jahazi?
..mimi nitaendelea kuamini kwamba JK na Lowassa ni wamoja mpaka pale vikao rasmi vya chama vitakampomchinja Lowassa.
cc Pasco