Expensive life
JF-Expert Member
- May 2, 2020
- 2,971
- 9,437
Moja kati ya silaha kubwa sana ya wanasiasa kuwabakiza madaraka pale mambo yao yanapoenda kombo basi huwa ni jeshi la polisi.
Polisi ukiondoa yale mavazi yao na wao ni wananchi wa kawaida tu, hali ya maisha ni sawa tu na sisi raia wa kawaida.
Ugumu wa maisha tuliyonayo wananchi na wao pia wanapitia. Mishahara duni, wengi wao watoto wao wanasoma na watoto wetu kwenye hizi shule zetu, hospital tunatibiwa pamoja, yaani kadhia zote tunapata pamoja.
Ajabu ni kwamba wamekuwa wakilinda maslahi ya wanasiasa kila uchwao, ajabu ni kuwa hata wanasiasa wenyewe hawana muda nao, wanaofaidika ni mabosi zao.
Nenda kwenye makazi yao, wenyewe wanaita kota, utalia zingine zimechakaa chakari 🤔
Nyie tupigeni tu virungu lakini msoto wa kimaisha tunapitia wote.