Licha ya kuwepo kwa madini ya kutosha, bado mwamko wa Watanzania kuijua JamiiForums ni mdogo

Watu wengi wakiwa nje ya JF hawapendi kujionyesha kua wanaijua JF
Ila ukweli ni kwamba wanaijua JF vizuri sana,
sio kila anayekwambia kua haijui JF basi ni kweli kua haijui.
Hata mimi sipendi watu wajue kama nina akaunti Jf ndio maana hata app naogopa kuidownload nahofia kujua kuwa mimi ni Jf member .
 
JamiiForums is exclusively for great thinkers only !
 
Sababu ya mtandao kukosa watumiaji wengi ni Masharti mengi ambayo kwa watumiaji ni kama usumbufu.
JamiiForums inakandamizwa na Serikali vitu vidogo basi Serikali inawafungia.
JamiiForums isingekuwa chini ilipaswa kuwa juu lakini Serikali imekuwa ikiwakandamiza kwa masharti ya kipuuzi
 
Hawaijui kwasababu watz wengi hawapendi maandishi, mambo ya kusoma vitu virefu sio hobie yao.

Si waona hata hapa jf mtu akileta bandiko lake refu watu hulalama ati alifupishe.
 
Hata mimi sipendi watu wajue kama nina akaunti Jf ndio maana hata app naogopa kuidownload nahofia kujua kuwa mimi ni Jf member .
Kuna watu wana app lakim hawana account jf
 
watanzania wengi wanaitumia mitandao kwa mawasiliano na kujuana ni wachache wanaochimba madini kwenye mitandao..
 
Jamii Forums iache kucopyright vitu,ili watu waweze kuipeperusha.
 
Tena vijembe vya Jf kila siku kuwasakama walimu, nakubaliana na wewe mkuu
 
Watu wengi wakiwa nje ya JF hawapendi kujionyesha kua wanaijua JF.

Ila ukweli ni kwamba wanaijua JF vizuri sana.

sio kila anayekwambia kua haijui JF basi ni kweli kua haijui.
Na Mimi ni miongoni mwao wiki mbili zilizopita Kuna jamaa yangu sana alipitia changamoto tukiwa tumekutana tunaongea na kushauriana aliniambia alipita jf kusoma experience za watu na kuchukua ushauri.
Kilichonifurahisha zaidi ni kuona baadhi ya comments ameziscreenshot na yangu ikiwemo kati ya ambazo zimekua msaada sana kwake.

Nikamuuliza jf ndio nini akanijibu na kuisifia sana japo sidhani Kama anayo account humu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…