Licha ya kuwepo kwa madini ya kutosha, bado mwamko wa Watanzania kuijua JamiiForums ni mdogo

Licha ya kuwepo kwa madini ya kutosha, bado mwamko wa Watanzania kuijua JamiiForums ni mdogo

Watu wengi wakiwa nje ya JF hawapendi kujionyesha kua wanaijua JF
Ila ukweli ni kwamba wanaijua JF vizuri sana,
sio kila anayekwambia kua haijui JF basi ni kweli kua haijui.
Hata mimi sipendi watu wajue kama nina akaunti Jf ndio maana hata app naogopa kuidownload nahofia kujua kuwa mimi ni Jf member .
 
Tangu nijiunge rasmi JamiiForums kiukweli sijawahi jutia, lakini bado watu wengi hawaijui. Yaani unaweza pita mtaani kati ya watu kumi utaowauliza ni mmoja tu ndo anayeijua, mwingine anakwambia "ndo nini hiyo".

Mpaka sasa, hata posts tu hazifikii idadi ya watanzania maana posts zipo 43 million, threads 1 million, na member laki sita. Kama mtu anavoshinda instagram siku nzima na mimi ni hivyo hivyo JamiiForums.

Je, tatizo ni nini maana JamiiForums sio popular kabisa among people.
JamiiForums is exclusively for great thinkers only !
 
Sababu ya mtandao kukosa watumiaji wengi ni Masharti mengi ambayo kwa watumiaji ni kama usumbufu.
JamiiForums inakandamizwa na Serikali vitu vidogo basi Serikali inawafungia.
JamiiForums isingekuwa chini ilipaswa kuwa juu lakini Serikali imekuwa ikiwakandamiza kwa masharti ya kipuuzi
 
Hawaijui kwasababu watz wengi hawapendi maandishi, mambo ya kusoma vitu virefu sio hobie yao.

Si waona hata hapa jf mtu akileta bandiko lake refu watu hulalama ati alifupishe.
 
Hata mimi sipendi watu wajue kama nina akaunti Jf ndio maana hata app naogopa kuidownload nahofia kujua kuwa mimi ni Jf member .
Kuna watu wana app lakim hawana account jf
 
Twende kwa mifano halisi, ni nondo gani unazipata humu ambazo huko mtaani hawazijui?
.
Screenshot_20230430-113713.jpg
 
watanzania wengi wanaitumia mitandao kwa mawasiliano na kujuana ni wachache wanaochimba madini kwenye mitandao..
 
Uongo mkubwa, mitandao yote mikubwa Ina hizo sifa. Kazi kwako kuamua unafuata yapi. Hata insta na fb kuna pages nyingi ultu za madini ya kila aina. Umemfollow mwijaku, unategemea nini?

Hayo uliyosema jf yapo tena ni mengi mno, Kama uzushi basi humu ndio sehemu yake. Kama utoto humu ndio sehemu yake pia, Kama ni vijembe Kama ulivyosema twitter humu napo ni mahala pake
Tena vijembe vya Jf kila siku kuwasakama walimu, nakubaliana na wewe mkuu
 
Watu wengi wakiwa nje ya JF hawapendi kujionyesha kua wanaijua JF.

Ila ukweli ni kwamba wanaijua JF vizuri sana.

sio kila anayekwambia kua haijui JF basi ni kweli kua haijui.
Na Mimi ni miongoni mwao wiki mbili zilizopita Kuna jamaa yangu sana alipitia changamoto tukiwa tumekutana tunaongea na kushauriana aliniambia alipita jf kusoma experience za watu na kuchukua ushauri.
Kilichonifurahisha zaidi ni kuona baadhi ya comments ameziscreenshot na yangu ikiwemo kati ya ambazo zimekua msaada sana kwake.

Nikamuuliza jf ndio nini akanijibu na kuisifia sana japo sidhani Kama anayo account humu.
 
Back
Top Bottom