How do we live after physical death?
Mwenyewe umesema Physical death, kifo cha mwili. Anza kujiuliza wewe ni mwili au mwenye mwili, kama ni mwili basi waamini wanaosema tunarudi mavumbini kwa sababu mwili ni chakula na vinywaji tunavyokula ambavyo vinatoka ardhini, lakini kama sio mwili ni mwenye mwili basi kitu ambacho kikojuu ya mwili au ndani ya mwili ambocho ndio kina siri ya kifo cha mwili hivyo ni kazi yako kutafuta kujua wewe ni nani? ukoje, unakufa? unahitaji mwili kwa nini? Kwa maana kwa nini unaishi?
Amani mrimbo, nadhani unakumbuka mambo mengi sana, uliyoyafanya ukiwa mdogo mpaka sasa, mtu mzee amepitia mabadiliko mengi sana, sasa ukiona ubadilikaji ina maana wewe hauko ndani ya mabadiliko kuweza kuona kitu kinabadilika lazima uwe nje ya mabadiliko hayo. Ukweli wakati miili ina badilika (inakua) sisi tunaiona na tunatunza kumbukumbu, hatubadiliki. Upo, Ulikuwepo na utaendelea kuwepo,kama vile nguo unavaa ikichafuka unaivua unavaa nyingine ndio miili pia sijui umeshasikia kitu kinaitwa re-incanation , miili imetoka mavumbini lakini sisa ni uhai, hai haifi, haichoki, haichomeki. Badala ya kuhaika kutafuta kumjua mungu binadamu anapaswa kwanza kujijua yeye, harafu kwa kutumia nafsi yake ndio atamjua mungu, lakini wengi hatuanzi hivyo, tunakimbilia majibu rahisi. Ama kwa kuambiwa na kusoma kwenye vitabu. Majibu yote pamoja na swali lako yanapatika ndani nafsi yetu, ni nafsi ilikuwepo kabla ya kuzaliwa, pia itakuwepo wakati wa kifo, sasa kwani tusiitafute na kuijua tungali hai?
Tukiweza kujijua (yaani kujua nafsi zetu), tutaweza kujua tumetoka wapi,tunakwenda wapi na wasiwasi wa nini tulipaswa kufanya katika maisha yetu vitaondoka na kuanzia hapo tutakuwa huru daima.
Kwa kutokufanya hivyo tunakuwa watumwa wa kutaka kuendelea kuishi yaani waoga wa kifo kama vile tukiishi muda mrefu tutalizika kuwa sasa imetosha. Muulize kikongwe wa miika 90 kama amelozika na maisha,utamkuata anataka kuisha kama kijana mdogo licha ya kwamba mwili wake umechoka na kila kiungo kinauma, hawezi kufanya mambo mengi alizowea kuyafanya alipokuwa kijana.
Kuna kitu binadamu anakitafuta lakini hakijui ndio maana hata akiwa tajiri kiasi gani haliziki. Kifo kinakuwa kama ndio mweisho wa juhidi zake kutafuta hicho, lakini fact kwamba tutakufa huwa ni mwanzo mzuri kwa kujua kwanini tunaishi wakati lazima tutakufa.
Asante