kiukweli uchunguzi wa kiimani nimeufuatiliasana kupitia dini mbalimbali zilizopo duniani, japo sisemi kuwa nimemalizaifuatayo ni baadhi ya vitu nilivyowahi kuvipitia:Historia ya biblia na aina tofauti zabiblia kuanzia ya wakatoliki, wa-orthodox, n.k ikiwemo madai kuwa imebadilishwa.Historia ya uislamu, mtume na maisha yake na madai ya yeye kuoa binti mdogo nawahyi, hadi kifo chake. Na waliouwepo na kipande quran kinachodaiwa kuliwa nambuzi n.k.nimeifuatilia sana na imani ya kiislamu namadhehebu yake kama shia, suni, sufi, agakhan, nk.Wanaoshuhudia dini walizoama mfano:Pia kuna mzungu mwislamu anaedaiwa nimtanzania alikuwa vatican akaacha anaitwa Abdul-Raheem Green. Anaeneza islamic propaganda(Dahwa), PastorDR. Hamis Paulo Hussein,&shekh Rashid Tahtashajara hawa walikuwa waislamu wameamiaukristo, wapo yu-tube) , freemasons, Illuminati, Skull and Bone,Satanic by Antony Lavey. DVDs za 'Thrive, Age of deceit-fallingangel and the new world order, The secrets of the secret service(2010), naVatican secret EXPosed by Jordan Maxwell, Zeitgeist, na Haunt,Video za Unidentified Foreing Object (UFO), Ancient Air craft and Spaceshipevidence, Ancient alliens (hapa ziponyingi tangu kipindi cha Adolf hitler hadi technolojia zinazoendelea inatolewamara nyingi kwenye History-DSTV channel), David Icke (mwingereza maarufu kwa mafundisho yake, hapo kabla aliwahi kuwamtangazaji wa mpira wa BBC kwenye miaka ya tisini anamuelezea binadamu kama anamijusi (Reptilia) akidai pia kuna uzao wa Reptilia((Illuminati blood lines) , Buddha (kiasi sana), Scientology, Mormon,Tagthatha(hii imani nadhani inasili kama korea na china hivi, chaajabu kiongozi wake anadai anajua mwisho wa dunia anapoambia ataje anakataaakidai itawachanganya watu.nikaona niwapige chini mara moja sikuendelea kusomazaidi. The Da Vince code,(hapa kuna mambo yayesu na maria magdalena na ule mchoro wa monalisa na nadharia za Plato kuhusu mungu. Meditation, kitu nilichopata kwenye meditation ni kwamba kama una diniyako, ukianza ku-meditate utakuwa unafuata dini na meditation lakini baadaeutaacha dini yako na kuendelea na meditation. Pia meditation inasaidia kukupaukweli ambao dini zote zimeshindwa kukupa. Watu niliokaa nao hawali nyama walaunyaji wa pombe na wanatumia vipande vya soya (vinavyotafunika kama nyama kamambadala wa nyama) hawaamini uchawi na wanaamini binadamu ana miili saba. Ninarafiki zangu ni waumini wazuri kwa hili. Na pia walinipa na hali ilivyoulimwenguni kwamba wazungu wengi sikuhizi hawaendi makanisani tena wanaaminikatika hii meditation zaidi. binafsi hivi vitabu vyote vinaweza kuku-disapoint kiimani.jambo kubwa nimetokea kuliamini kuwa kuna supernaturalpower katika ulimwengu tunaoishi,kuhusu uchamungu nimegundua kuwa:Dini kama dini haibadilishi asili ya mtuinachofanya ni kupunguza tena kidogo saana. Tabia ni kitu mtu anazaliwa nacho (inborn)na si kitu cha kujifanya kuishi. Kuna watu ni wapagani lakini wanaishi kamavile wameokoka na wacha mungu wakati huhuo kuna watu wameokoka na wanakwendakanisani au misikitini kila siku lakini wanaroho mbaya sana.kiasi kwamba unajiuliza hivi huyu kama angekuwa hajaokokaau haendi kusali angekuaje?. Na labda ndio maana katika ulimwengu wa leoutasikia mara padre kakamatwa amebaka, shekh kalawiti, mchungaji kafumaniwan.k.Pia kuhusu dini ni kwamba sio kila padre,Shekh, Mchungaji, anaweza kutoa jibu zuri kwa maandiko aliyosomea na hii ina maana kwamba ukimuuliza mmoja umjuae akishindwa kukupa jibuhaimaanishi wote hawawezi au dini hiyo sio ya kweli.nimeona video ya pastor chris akisema sigara, punyeto sio dhambi.ikawa very disapointing je wanaotetea ushoga sjui vp. pia kuna wale wanaoaminikatika mungu ukiachilia sababu za kimazingira kama kuzaliwa kwenye familiaza dini zao, pia huwa wanaamini kwa jinsi wanavyoona wananufaika nazo. Ni tatizokwasababu kuna dini nyingine zinaeneza uovu na ukatili kwa wananadamu wenginelakini kwakuwa wale perpetrator (wanaofanya uovu) wananufaika kimaslahi na hizodini wanaendelea kuhalalisha uovu wao kama sehemu ya kimungu au kiimani. Pia Tatizo la kukosa kuwa na kiasi la baadhi yawatu linapelekea kuhama dini na kuvurugikiwa na maisha kwasabau ya madhara ya kuzidisha.mfano watu walevi sana,malaya sana, wauaji sana, ikitokea matendo yao hayajawaletea mauti basimwishowe wanaweza kuishia kuacha wakidai wameokoka na kubadilikakabisa lakini ile nature yao ya asili huwa haiondoki hivyo wanakuwa namatatizo hata wakisema wameokoka vipi. mfano mtu anajitetea alikuwamlevi sana akawa anapiga na kutukana na kujinyea hovyo lakini sasa ameacha na anashauri watuwaache pombe wawe kama yeye, ukimchunguza utamkua anamatatizo bado, . kwani mbona kuna watu wanakunywa pombe kila siku lakinihawamtukani mtu na hawana matatizo na mtu yoyote katika jamii?Vilevile uzoefu wangu unanionyesha walewatu ambao ni (extreme) wenye kutafuta perfection in most cases wanaishia kuwa disappointedin the end lakini hii naona inatokana na uhalisia kwamba hakuna mtu perfect perse. hata dini zetu zinamapungufu fulani. Sababu za uwezekano wa uwepo wa mungu duniani: kuna viumbe vimepita uwezo wakibinadamu ambayo wanasayansi wanaviita extraterestrial ambapo wanakiri kuvi-experiencekatika kazi zao za kitafiti especially Space na Archeology. Ambapo kunawatafiti wanaamini kuwa hawa extraterrestrial wanataka kuja tena duniani kuungana sisi na ndio chanzo cha maendeleo ya technologia duniani, wanasayansi wenginewanasema hawajui lengo lao. Mfano mwanasayansi mjerumani aliechukuliwa namarekani baada ya vita kuu ya pili na kuwa mkuu wa NASA alikiri kuwa ujuzi waowanasaidiwa na Alliens. Pia uchunguzi huu wa extrateresrial unahusisha vitabu vya dini kama Quran(gene, angel, , n.k.) na biblia (kuna satan, demon, angel, ).Pia ushahidi wa kimazingira mfano misrikuna pyramids(Giza) ambayo yapo pia sehemu nyingine duniani na kuna michoroya watu wenye maumbile ya ajabu ajabu kama vile sura ya kuku kiwiliwili chabinadamu, malaika wana mabawa, kwato, kucha kama za wanyama, n.k. Wataalamu wanasemamichoro hii haipo kama coincidence tu ila ni conceptual yakielezea uhalisia waviumbe ambao binadamu wa kale alikuwa akikutana nao miaka mingi iliyopita. Wanasayansikwa kutafuta majibu ya maswali yao wanahusisha na vitabu vya dini ili ku-linkideas. sayansi za kitabibu zinakiri kuwa Biblia ndio kitabu pekee cha kikongwe kuwepo na labda hapo ndipo panaponifanya nione haja ya kukiamini zaidi kulikovitabu vingine. Wanasayansi wamethibitisha kisayansi kuwepo kwa mapigo kumi ya misridhidi ya farao yalioandikwa kwenye biblia. . Vitu kama Safina ya Nuhu, msalaba wa yesualiosulibiwa, mji wa suleiman ni miongoni mwa mabaki ya vitu ambavyo vimepatikana vikiwa vimefukiwaardhini na wanasayansi wanaochimbua (archeologists) kule mashariki ya kati nakuthibitisha yale yaliyomo katika biblia yalitokea kweli.Quran inataja uwepo wa wakristo katikakitabu chao na inakiri uwepo wa yesu na kuzaliwa kwake, uwezo wake wa kuponyana kufufua wafu, yesu kutokuwa na dhambi na hata kuja kuhukumu ulimwengu wakatiwa kiama ambavyo ni vitu vinavyoshabiiana na biblia. Japo inakataa jambo moja kuula ukombozi wa mwanadamu kwa thamani ya damu yake yesu pale msalabani.Matukio katika biblia ni baadhi tu ya yanayonishawishi kusimamia imani;Pale wayahudi walipomkataa yesu inatokanana wao kuamini kitokacho kwa mungu kinautukufu na nguvu nyingi na kitatawaladunia watakuwa taifa kubwa, mwisho wa siku yesu akazaliwa kwenye zizi langombe, hata ningekuwa mimi kwa kutumia logic za kibinadamu ningekataa pia. .Pia najiuuliza ni kitu gani kilichowafanyawaisraeli watengeneze sanamu wa dhahabu wakati Musa aliwaambia anaenda mlimanikuleta amri za mungu. Sidhani kama waisraeli walikuwa mataahira/wa akili auwakaidi kivile binafsi naamini kuwa muda ambao Musa aliotumia kwenda na kurudiulikuwa mrefu katika kiwango ambacho binadamu yoyote asingeendelea kuamini tenakama kuna mungu anawaongoza hivyo walikata tamaa kama wanadamu. Na pengine sisituliopo leo tunakumbana na hali ileile iliowakuta wanawa-israel enzi hizo.Tujikumbuke kuwa hata maandiko yanasemakama muda usingalifupishwa hata watakatifu wangalipotoshwa.je hatuhisi kakata tamaa? hii inaonyesha nijinsi gani uwongo wa shetani ulivyomkuu hata wacha mungu wamekata tamaa nakuamua kuasi kama ambavyo waisraeli walikuwa wanamwasi mungu mara kwa mara.Pia maandiko yanasema shetani ni muongo nababa wa uongo. Nadhani watu wanaweza kuwa waongo lakini hawamfikii shetani yeyeni baba lao. Hivyo basi akiwa ndiye babawa uongo ni vigumu kwetu sisi kama wanadamu kuweza kuchora mstarikutenganisha kati ya kweli na uwongo. Lakini angekuwa mwongo mdogo tungewezakung'amua janja yake kirahisi nakumkataa. Njia pekee ni kusoma neno la mungunalo ni biblia tu. Nachoweza kusema, njia za mungu si njia za wanadamu namawazo yetu sio mawazo yake, ni kama vile mbingu ilivyo juu sana na ardhi.