Life after Death: What happens after death?

Life after Death: What happens after death?

We kitimoto unajua ilmu ya roho allah aliyoizungumzia au unaleta ngonjera zako hapa zisizo na mashiko.
kweli kichaa ni taaluma! allah ndie aliyesema ilimu ya Roho hamkupewa unanikoromea mgen badala ya allah aliyesema! Mbona shobo? Na moja ya dalili ni hizi kwamc hamna ilimu ya Roho!; kuna hekima gani ukijamba unaachia swala na kukimbia kwenda kunawa na harfu ya ushuzi unaiacha msikitini ukijamba?...
 
wee g!; acha kupiga mikelele! allah amesha kwambia ilimu ya Roho hukupewa hau! Au unamuona allah muongo? Unatakiwa utulie uwe mdogo kama piriton! Wakati mambo ya Roho yakijadiliwa!

wewe umepewa elimi ya kiroho na mapadri wenzako na ndio mkaicheza ile michezo ya kiroho au sio hiyo ndio hoja uliyobaki nayo
 
mpaka saa hii sina idea kwamba naenda wapi....but nikishakufa ndio nitajua....kwa sasa ni mapema mno kwa mimi kufahamu hilo

the most prudent idea ni kukubali ukifa huendi popote thats is it na hiyo ndio fact iliyotuzunguka mpaka sasa unless mtu akitupa ushahidi otherwise... watu wote wanaokufa wanaoza basi inabaki mifupa sasa sijui hii courage ya kudhan ukifa may b unaenda mahali imetoka wapi!!! tuishi kwa fact zinazotuzunguka tuachane na illusion!!! since karne na karne watu wanakufa tu na hakuna hata mmoja aliyerud au kututhibitishia akifa anaenda mahal!!!
 
May be we are more afraid of living than we are of dying.. just saying..... this is some scary shit here
 
mi naona kila mtu atajua atakwenda wapi pale ATAKAPOKUFA...zaidi ya hapo hapo sasa tutakuwa tunachanganyana tu....tuwe na subira jamani kwani kifo chaja tutajua tu...lol.....
 
Ushauri wa bure kwa wote msioamini kwamba kuna maisha baada ya kufa: Ni heri muamini kwamba yapo
maisha baada ya na ya kuwa Mungu yupo kuwahukumu wanadamu,ili mtakapofika msimkute huyo Mungu,
kuliko kuamini kwamba hakuna maisha baada ya kufa then unakufa immediately unahukumiwa kwenda motoni.
Maana neno linasema mwanadamu amewekewa kufa mara moja na baada ya kufa tu ni hukumu - WAEBRANIA 9:27
Yesu ni njia kweli na uzima mtu haji kwa Baba ila kupitia kwa Yesu.Nawashauri kuwa mumpokee Yesu kwenye
maisha yenu mkiwa bado hai,kwani kuna maisha baada ya kufa either Mbinguni milele kwa waliompokea Yesu au
motoni milele kwa waliomkataa Yesu'

unacheza bahati nasibu? kwa nn uamini kitu usicho na ushahidi nacho? ni tamaa tu ya kutaka kuishi milele au!!!
 
Ikiwa tutaenda mbinguni mbona Mungu alipomuumba Mzazi wetu wa kwanza Adam na Hawa hawakuishi mbiguni? Na ikiwa tunamatumaini ya kuishi mbinguni kwanini tuonauomba ufalme wa mungu uje duniani?
Na hilo nalo neno!
 
nani anakumbuka chochote kilichotokea miezi kumi kabla hajazaliwa ambacho alikisikia alikiona yeye mwenyewe "live". kama hakuna, hiyo ndiyo hali anayokuwa nayo mtu akifa.

(1) UUMBAJI.
udongo + pumzi ya uhai = nafsi hai (mwanzo 2:7)

(2) KIFO
Nafsi hai - pumzi ya uhai = udongo. (mwanzo 3:19, zaburi 146:4, zaburi 104:29)

(3) MTU AKIFA ROHO HAIENDI MBIGUNI.
Biblia inasema hivi; mhubiri 9:4-6,10 & mhubiri 3:19-21

Kwa kuwa liko tumaini kwa yule aliyeambatana na wote walio hai; (maana ni afadhali mbwa aliye hai kuliko simba aliyekufa);
kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.

Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua.

Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili.

Wote huendea mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena.

Ni nani ajuaye kama roho ya binadamu huenda juu, na kama roho ya mnyama huenda chini?
Hivyo nikaona ya kwamba hakuna jema kupita mwanadamu kuzifurahia kazi zake; kwa sababu hili ni fungu lake; kwa maana ni nani atakayemrudisha tena ili ayaone yatakayomfuata baadaye.

MTU ALIE KWENYE KOMA, AU ALIEZIMIA HUWA KWENYE NUSU MAUTI.

mtafute mtu aliwahi kuwa mahututi au aliewahi kuzimia muulize kama anakumbuka kuona chochote au kusikia chochote.

mshahara wa dhambi ni mauti. roho inayotenda dhambi itakufa.
yesu alipokufa hakwenda mbinguni hadi alipofufuka na kupaa..

waliokufa wamelala wanasubiri kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 1wathesalonike 4:13-15

Umeeleza vizuri sana mkuu, na kifungu ulichotoa kwa hakika kiliandikwa na mtu aliyekwishaanza kujitambua! Lakini hapo chini kwenye njano naona ukanipoteza tena, kwa maana hiyo wenye dhambi ndiyo wataonja umauti halafu wasio na dhambi hawataonja umauti? au kuna kitu sijaelewa mkuu?
 
Ushauri wa bure kwa wote msioamini kwamba kuna maisha baada ya kufa: Ni heri muamini kwamba yapo
maisha baada ya na ya kuwa Mungu yupo kuwahukumu wanadamu,ili mtakapofika msimkute huyo Mungu,
kuliko kuamini kwamba hakuna maisha baada ya kufa then unakufa immediately unahukumiwa kwenda motoni.
Maana neno linasema mwanadamu amewekewa kufa mara moja na baada ya kufa tu ni hukumu - WAEBRANIA 9:27
Yesu ni njia kweli na uzima mtu haji kwa Baba ila kupitia kwa Yesu.Nawashauri kuwa mumpokee Yesu kwenye
maisha yenu mkiwa bado hai,kwani kuna maisha baada ya kufa either Mbinguni milele kwa waliompokea Yesu au
motoni milele kwa waliomkataa Yesu'

Aisee! Kuna mambo mawili nimeyaona ktk hoja zako!

Moja rudi ukaisome Hiyo waebrania tena uone ina maana gani na km Bado utakua hauielewi rudi uniulize nikufafanulie!
Kutokana na waebrania haina maana ya kifo Cha mwandamu!

Na pili ktk Biblia kuna mtu anaitwa Razaro! Nenda ukasoma kisa chake kisha uje hapa Tujadili!

Napenda niseme Hakuna maisha baada ya kifo! Wafu wamekufa na Hawajui chochote na hawako sehemu yoyote Zaidi ya Kua mizoga kaburuni!

Hii ndio kauli halisi ya shetani alipomwambia Hawa bustanini Kua ukila tunda hautokufa utakua km Mungu na Leo tena mnatuambia kuna maisha baada ya kifo?
 
Umeeleza vizuri sana mkuu, na kifungu ulichotoa kwa hakika kiliandikwa na mtu aliyekwishaanza kujitambua! Lakini hapo chini kwenye njano naona ukanipoteza tena, kwa maana hiyo wenye dhambi ndiyo wataonja umauti halafu wasio na dhambi hawataonja umauti? au kuna kitu sijaelewa mkuu?

Mkuu Nimeona nijaribu kujibu niwezavyo,

Nirudi Eden Mungu alimwambia Adam Kua wakila lile tunda la mti Wa uzima watakufa! Na walipokula hawakufa hapohapo na baada ya laana Ndo tunaona mtoto Wa Adamu " Abel" anauawa/kufa! Kwa Hiyo hapo ile kauli ya Mungu ikaanza kutimia!

Ukisema mshara Wa dhambi ni mauti haina maana Kua usipotenda dhambi Kamwe hautokufa! Hilo fungu linazungumzia kifo kile Cha pili Cha milele na Kwa maana Hiyo mtu asipotenda dhambi ajapokufa ataishi! Hii nayo inaonesha ule ufufuo ujao Kua ukiwa Just utaishi milele!
Shida kubwa ni mauti ile ya pili maana ukiwa mdhambi ndio milele hautoonekana na ukiwa Mwenye haki basi utaishi milele! Hichi kifo Cha sasa Hakina shida Kwasababu kuna ufufuo ila shida ni kwamba mauti yatakukuta Vipi? Mdhambi Au Mwenye haki? Na pia niweke wazi hapa Hiyo siku atakaporudi Mwana Wa Adamu kuna binadamu wengine watakutwa hai.
Na katika Hao wenye haki hawatoonja mauti na watanyakuliwa kwenda mbinguni na waliokufa katika haki watafufuliwa kwanza na kuunganana Hawa kwenda mbiguni! Wenye dhambi watakaokutwa duniani watakufa na shetani atafungwa miaka 1000 na Dunia kubaki ukiwa na mizoga ya maiti ikiwa imetapakaa! Then shetani atafunguliwa na Hao wadhambi watafufuliwa na kuteketezwa. Na dhambi kutokomezwa
Then Dunia itafanywa mpya na walio kwenye haki watarudia kuja kuishi hapa Dunia!

Sijui nimeeleweka?
 
Ni kama umenipoteza kidogo mkuu, navyoelewa biblia inafundisha kuwa baadaye watu wote watafufuliwa, kisha wengine wataenda mbinguni na wengine motoni ambako wataunguzwa milele bila "kufa" tena!
 
Ni kama umenipoteza kidogo mkuu, navyoelewa biblia inafundisha kuwa baadaye watu wote watafufuliwa, kisha wengine wataenda mbinguni na wengine motoni ambako wataunguzwa milele bila "kufa" tena!

Mkuu nilihisi hoja haijatimia nikafanya kuhariri Hiyo post! Hebu pitia tena uisome kuna majibu ya hapo ulipopotea!
 
Ni kama umenipoteza kidogo mkuu, navyoelewa biblia inafundisha kuwa baadaye watu wote watafufuliwa, kisha wengine wataenda mbinguni na wengine motoni ambako wataunguzwa milele bila "kufa" tena!

Alafu Mkuu kuna kitu nilisahau kidogo, wakati Wa hukumu ni sasa Yani Tuko ktk huku iwe jema Au baya! Tunaesabiwa haki na atakapokuja Mwana Wa Adam ni kumlipa mtu ujira wake Kutokana na matendo yake!
Na ndio maana ukifa hesabu yako inakua imeishia hapo! Hakuna mtu atakaeweza kukuombea usamehewe dhambi Au upate heri wakati mauti yakiwa tayari yamekukuta!
 
Knowledge yetu ya maisha is limited to the ordinary life. Ukikubali kujua zaidi ya unachojua, na ukiwa tayari kujua, mwalimu atakuja na kukufunulia yale usiyoyajua kuhusu maisha. Mwalimu huyo atakupeleka kwenye 'enlightment' ya kujua deeper Into life, before life na after life.

Siku ambayo mwalimu atakuja ni wakati ukiwa tayari 'when the student is ready, the teacher will apear'.

Bada sijafikia kiwango cha kumpata mwalimu, lakini kwa mujibu wa maandiko ya wafuasi wa jumuiya ya 'Rosae Crusis' Msalaba wenye uaridi linalotiririsha matone ya damu wanaamini, kuna maisha kabla ya haya na kuna maisha baada ya haya. Yaani 'life before life' na 'life after life'.

Wafuasi wa Rosae Crusis wanaitwa ma 'rosecrusians'. Hawa jamaa wanauwezo wa kufanya kila kitu, uwezo wa kuwepo mahali popote in a split of second, uwezo wa kuwa invicible na uwezo wa kutenda miujiza.

Kwenye maandiko yao, wanadai Jesus Crist was a rosecrusian. Kuna uwezekano hawa wahubiri wanaofanya miujiza ni marosecrusians.

Wao wanaamini kuna 'Supreme Being', call him what you may, be God, Allah, Budha, Brahma, Bahai,etc. Uli kumfikia lazima upitie mbingu 7 waziitazo Eternities. Katika safari yako, utazaliwa, utakufa, utaliwa, utakufa na kuendelea hivyo hivyo mpaka ufike kwenye 7th Eternity.

Ukufanikiwa kuwa enlighterned, you have the control of death. Yaani unashinda kifo na unaishi milele, ila lazima ubadilishe body from time to time kwa sababu mwili unachakaa mapema.

Mwandishi Linda Goodmans kwenye kitabu chake cha 'Star Signs'
Anasema, you have the control over death na kuna watu aliwajua toka akiwa mdogo, na wanaishi mpaka kesho na umri usio hesabika.

Linda anasema, kwa vile watu huishi takriban miaka 100, ukiweza kuyashinda mauti, unafikia muda wale wote wa rika lako wamekufa mpaka unaona noma, its time to change body, unakubali kufa, wanazika mwili, huku in actual fact, umehama mwili na kuchukua mwili mpya na kuishi maisha mapya mahali papya au hata pale pale kama mtu mwingine.

Mimi kwa kiasi fulani nakubaliana nao, tatizo ili ukubaliwe kuwa mmoja wao, lazima ukubali kula kiapo cha usiri na kufanyiwa initiations na hapo ndipo palipo nishinda nikaamua kukubali kuishi maisha haya ya kawaida na knowledge haba. Haya machache nimeyasoma kwa wizi toka vitabu vya muumini viitwavyo 'monograms'. Mambo ya 'de-javu' ni vitu vya ukweli, only vivid of life before life.

life before life hata kitabu cha momorns kinaeleza hvyo,life after life pia kinaeleza kua kuna mbingu nyngi sana na kabla ya kuja duniani sis tulikua miungu na hata tukifa tunarudi kua miungu na kila mtu anapewa sayari yake awe mungu kwa watu wa huko na hata mungu wetu hapo kabla alikua binadam kwenye sayar nyngne kisha akawa mungu,shart ili uwe mungu unatakiwa kuobey mungu wako wa sasa km alivofanya mungu wetu,aliobei mungu wake,je unataman kua mungu,soma vitabu vya nabii joseph smith.
 
Mkuu Nimeona nijaribu kujibu niwezavyo,

Nirudi Eden Mungu alimwambia Adam Kua wakila lile tunda la mti Wa uzima watakufa! Na walipokula hawakufa hapohapo na baada ya laana Ndo tunaona mtoto Wa Adamu " Abel" anauawa/kufa! Kwa Hiyo hapo ile kauli ya Mungu ikaanza kutimia!

Ukisema mshara Wa dhambi ni mauti haina maana Kua usipotenda dhambi Kamwe hautokufa! Hilo fungu linazungumzia kifo kile Cha pili Cha milele na Kwa maana Hiyo mtu asipotenda dhambi ajapokufa ataishi! Hii nayo inaonesha ule ufufuo ujao Kua ukiwa Just utaishi milele!
Shida kubwa ni mauti ile ya pili maana ukiwa mdhambi ndio milele hautoonekana na ukiwa Mwenye haki basi utaishi milele! Hichi kifo Cha sasa Hakina shida Kwasababu kuna ufufuo ila shida ni kwamba mauti yatakukuta Vipi? Mdhambi Au Mwenye haki? Na pia niweke wazi hapa Hiyo siku atakaporudi Mwana Wa Adamu kuna binadamu wengine watakutwa hai.
Na katika Hao wenye haki hawatoonja mauti na watanyakuliwa kwenda mbinguni na waliokufa katika haki watafufuliwa kwanza na kuunganana Hawa kwenda mbiguni! Wenye dhambi watakaokutwa duniani watakufa na shetani atafungwa miaka 1000 na Dunia kubaki ukiwa na mizoga ya maiti ikiwa imetapakaa! Then shetani atafunguliwa na Hao wadhambi watafufuliwa na kuteketezwa. Na dhambi kutokomezwa
Then Dunia itafanywa mpya na walio kwenye haki watarudia kuja kuishi hapa Dunia!

Sijui nimeeleweka?

vp kuhusu wale watakuwa katika sayari nyingine mfano mass au mwezini hawatakufa atakapokuja mwana wa adamu hapa duniani?.
 
vp kuhusu wale watakuwa katika sayari nyingine mfano mass au mwezini hawatakufa atakapokuja mwana wa adamu hapa duniani?.

Aisee! Unazungumzia kiumbe binadamu Au? Km ni kiumbe binadamu popote pale Mungu atamfikia kumlipa ujira wake!

Kumbuka kisa Cha Yona aliemkimbia Mungu na kwenda kujificha! Lkn akiwa ndani ya bahari akatupwa majini na akamezwa na samaki na kupelekwa Ninawi ambako Mungu alikua amekusudia Yona Ende!

Huwezi kujificha mbele za USO Wa Mungu!
 
Lakini hapo chini kwenye njano naona ukanipoteza tena, kwa maana hiyo wenye dhambi ndiyo wataonja umauti halafu wasio na dhambi hawataonja umauti? au kuna kitu sijaelewa mkuu?

Hapo pia yupo sawa kwani hakuna binadamu ambaye ni masfi wote tunatenda dhambi na tuliridhi dhambi ile ya adamu ndiyo maana tuna kufa.
 
Hapo pia yupo sawa kwani hakuna binadamu ambaye ni masfi wote tunatenda dhambi na tuliridhi dhambi ile ya adamu ndiyo maana tuna kufa.

Mnazidi kunichanganya wakubwa, naona kama mistari ya biblia inakinzana!
 
Back
Top Bottom