Life After Life: Je, Wafu huwaita watu kifoni? Kuna walio hai huamua kuwafuata Wafu? Wapenzi mmoja akitangulia, mwenzake anafuata!

Pascal Mayalla, kwanini mwenzi mmoja akitangulia na kisha mwenzie kumfuata, Huko waliko wasiwaite watoto wao pia wawafuate na badala yake wanawaacha hapa duniani wakiteseka na kuhangaika bila msaada wowote?
Na pia kwanini huyo mwenzi wake alichelewa kumuita mpaka mwaka unaisha ndio anamuita inamaana muda wote huo alikua anafanya nini?

Sent using unknown device
 
Bibi kidude mume wake alikufa mwaka gani?

Sent using unknown device
 
Kwa kuongezea hapo ni kwa mfano wa Mzee Kingunge alipokufa mkewe haikupita miezi mingi mumewe alimfuata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hapo kwenye malaika ndio huwa sielewi kabisa... Mungu muweza wa yote anawezaje kuwa na wasaidizi? Mfano muslim wanadai kila binadamu amezungukwa na malaika wawili.. mmoja anarekodi matendo mabaya na mwengine anarekodi matendo mazuri..... alafu kuna yule anaetoa roho..... why this??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana ulichoandika kina ukweli kwa asilimia fulani nimewahi kujadili hii topic na watu before,pengine ndio maana baada ya mke wa Kingunge kutangulia mzee mzima Ngombale mwiru akasema hataaa ntakufata,sasa sjui Kambarage ye kaamua kumkaushia mke wake.
 
Paschal Bwana leo nimecheka sana
Wafu unawazuia kwa Maombi, Mama yangu alikuwa best friend wangu, amefariki namuota kila week lakini haji kuniambia njoo huku nilipo ananiambia "SIJAFA NIPO HAI"
Maombi yanasaidia kufukuza Miroho ya kuchukua binadamu wengine kabla ya wakati wa Mungu kukuondoa Duniani
ingekuwa ni hivyo umeandika mimi ningeshakufa muda sana lakini mpaka leo nadunda na Mama yangu hajawahi kuniambia njoo huku.

Biblia unayoibeba Kila j2 kwenda Kanisani inasema, ". HAKUNA SHIRIKA KATI YA WAFU NA WALIO HAI"
Ukiweza kusimama huo msitari kwenye maombi WAFU hutowaona tena, roho yako itakuwa na Amani siku zote
Au sio Pastor Ekuweme Mung Chris ?

Cc: 50thebe joanah moneytalk lara 1 Smart911
 

Honey Money Penny maisha ya kimwili (physical) yanaanzia rohoni (spiritual). Ni somo gumu kidogo linalotaka ustahimilivu kulisoma, kulichambua na kulitafakari. Mfano rahisi ni ile nyota ya mashariki waliyoaiona mamajusi zama zile. Waliona mfalme katika roho. Tunajua Herode alifanya nini.

Yusuph mwana wa Jacob alipokuwa Misri aliishi kwenye ulimwengu wa roho. Uthibitisho ni uwezo wake kufasiri ndoto. Ndoto ni lango la maisha ya kiroho yanayotokea katika mwili (physical world)

Inapotokea unaota unawasiliana na watu waliofariki, ima unawafahamu ila lah, sio rahisi kuhitimisha maana ya ndoto husika. Maana ndoto sio jambo la kubeza. Ndiposa wanasema "Dream come true!"
 
Mama Mercy alikuwa soul mate wa mzee Mengi, ila binadamu ni wabishi sana.
Daisy Llilies, hapa tunazungumzia hypothetical situation please usitaje majina ya watu ili usije kuwa hurt wafiwa, maana sisi Waafrika unakuta mtu ana soul mates, hivyo soul mate mmoja akamuita na kuitikia, hivyo kumfuata, soul mate mmoja na kumuacha soul mate mwingine, hivyo huyo soul mate aliyebakia naye anaweza kuitwa kwenda kuendeleza threesome.

Haya mambo ya soul mate ni very hard to comprehend.

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…