Life After Life: Je, Wafu huwaita watu kifoni? Kuna walio hai huamua kuwafuata Wafu? Wapenzi mmoja akitangulia, mwenzake anafuata!

Life After Life: Je, Wafu huwaita watu kifoni? Kuna walio hai huamua kuwafuata Wafu? Wapenzi mmoja akitangulia, mwenzake anafuata!

Pascal Mayalla, kwanini mwenzi mmoja akitangulia na kisha mwenzie kumfuata, Huko waliko wasiwaite watoto wao pia wawafuate na badala yake wanawaacha hapa duniani wakiteseka na kuhangaika bila msaada wowote?
Na pia kwanini huyo mwenzi wake alichelewa kumuita mpaka mwaka unaisha ndio anamuita inamaana muda wote huo alikua anafanya nini?

Sent using unknown device
 
"Yaani mtu uliyeumbiwa wewe kuwa parner wako wa maisha ya kimwili na kiroho, hivyo mkifanya sex, sio tuu mnafanya tendo, bali mnaunganika na kuwa mwili mmoja in spiritual body, hivyo mahusiano ya hivi, mmoja akitangulia, yule aliyebaki duniani hawezi kuishi muda mrefu, atamfuata tuu mwenzake, na mapenzi yao yataendelea kwenye the spiritual world."


Hatari sana... ndiyo maana vifo vya ghafla nje nje... ngoja nikae kimya...


Cc: mahondaw
Bibi kidude mume wake alikufa mwaka gani?

Sent using unknown device
 
Ninacho fahamu mimi ni kua katika imani za kishirikina (Uganga) kuna dawa hua wanachanja kama ni mume akianza kufa basi soon mke anafuata.
I mean mganga anamchanja mke wake dawa au mtu aliyemuhitaji yeye kama wanapendana sana kisah mmoja atakae anza kufa basi mwingine anafuata. Nimelishuhudia hili kwa macho..
Kuna ndugu angu sijui kama walikubaliana na mkewe ila nadhani alimpa mke akiwa hajui.. alimchanja then 2013 akafariki alipokufa tu mkewake akaanza kuumwa HHeavily. Mapepo yanampanda yanasema yanmtaka amfuate mume wake maana wametoka nae mabali so kwann amuache aende peke ake!! Ndugu zake tunapigania uhai mpaka leo kuvunja dawa nguvu. Mpaka leo yuko hoi ila kadhoofu mno..

Angalieni sana viapo vyenu mnavyojiwekea mkiwatembelea waganga. It will Haunting you
Kwa kuongezea hapo ni kwa mfano wa Mzee Kingunge alipokufa mkewe haikupita miezi mingi mumewe alimfuata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
OK "Duality"

Pia, Existence - inexistence
Life - death

Mzunguko [emoji676]

1= Inexistence
2= Existence
3= Life / living
4= Death
5= Inexistence

Wakati sijazaliwa sikuwa popote, kinyume chake nikawepo nilipozaliwa.

Vilevile, napotaka kuwasha moto wa mshumaa kiuhalisia moto haupo hadi nitakapowasha moto. Nitakapozima, moto na mwanga wake hupotea. Sasa moto na mwanga huenda wapi?

Naweza fananisha, binadam kuanza kufanyizwa tumboni mwa mwanamke ni kama uwepo wa mshumaa. Kuzaliwa ni kuwashwa kwa mshumaa, ambapo moto wa mshumaa ndio roho. Mshumaa unapozimwa au unapozima hakuna moto tena ( hakuna roho - uhai - tena). Kama moto, roho haina makazi tena. Kwa maana iliyowazi roho ya binadamu ni pumzi yake.

Mtu akifa, uhai wake unakoma. Kifo ni kinyume cha uhai. Kwa hiyo, mtu akifa haendelei kuishi mahali pengine, hisia na mawazo yake hupotea.Tukifa hatuwezi kuona, kusikia, wala kufikiri.

Swali : Wanyama pia wana roho, je wakifa roho zao huenda wapi?
Kama zinakuwa sehemu, zinafanya nini?

Maana mbili za roho

1. ROHO ~ nomino

: Pumzi, inayopelekea uhai wa binadamu.

2. ROHO ~ nomino

: Viumbe visivyoonekana Mf. Malaika,Mapepo,Jini,Shetani.
Ambao wapo mamilioni. Huwa havina miili maalumu ila vina uwezo wa kujivika miili ya nyama au kutumia mwili wa nyama.
Mkuu hapo kwenye malaika ndio huwa sielewi kabisa... Mungu muweza wa yote anawezaje kuwa na wasaidizi? Mfano muslim wanadai kila binadamu amezungukwa na malaika wawili.. mmoja anarekodi matendo mabaya na mwengine anarekodi matendo mazuri..... alafu kuna yule anaetoa roho..... why this??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana ulichoandika kina ukweli kwa asilimia fulani nimewahi kujadili hii topic na watu before,pengine ndio maana baada ya mke wa Kingunge kutangulia mzee mzima Ngombale mwiru akasema hataaa ntakufata,sasa sjui Kambarage ye kaamua kumkaushia mke wake.
 
Wanabodi,
Kifo cha Ephraim Kibonde kimeibua simanzi kubwa kwa sababu katika uhai wake hakuwahi kuugua, amekufa ghafla, hivyo watu kubaki na maswali mengi.
Katika bandiko la Tribute to Kibonde, kuna mwana JF kaandika maneno haya kumhusu Kibonde.


Kufuatia kuyasoma hayo, nimeona nizungumze kitu kuhusu uhai, kifo na maisha baada ya kifo.

Uhai ni Nini na Kifo ni Nini?.
Mwili wa binadamu una sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni huu mwili wa nyama, ambao umeumbwa kwa mavumbi, na siku ukifa, kinachokufa ni mwili huu wa nyama, unazikwa kaburini, humo ndani unaoza na kurudi kuwa mavumbi. Sehemu ya pili ya mwili ni uhai, uhai hii ni pumzi Mungu aliyoipulizia kwenye ule udongo hivyo mwili kupata uhai. Hii ni Roho ya Mungu, the spiritual body, the astra body, mwili unapokufa, roho haifi, bali huacha mwili na kurudi kwa Mungu. Hivyo kifo ni kitendo cha roho kuacha mwili.

Jee Baada ya Kifo, hiyo Roho inakwenda Kuishi Wapi?.
Kama ulivyo mwili una sehemu mbili ya mwili wa nyama na mwili wa roho, vivyo hivyo dunia ina sehemu mbili, Ulimwengu wa Kidunia, the physical world, na Ulimwengu wa Roho, the Spiritual World, mtu akifa, roho ikiacha mwili, mwili unabaki kwenye ulimwengu wa dunia, unazikwa unaoza na kugeuka kuwa mavumbi, Roho inakwenda kwenye ulimwengu wa Roho kuendeleo kuishi milele, being mbinguni, peponi, kuzimu, toharani, au jehanum kwenye moto wa milele, hii subject nyingine lakini roho hazifi kwa sababu roho ni Mungu.

Jee Roho za Waliokufa Zinaweza Kuwaita Walio Hai?.
Jibu ni yes, ndio maana kwa baadhi ya mila, wamama wajawazito hawaruhusiwi kwenda makaburini, ili waliolala wasije wakaviita vichanga, na matokeo yake vikaitika na kupata still born.
Kwenye mahusiano kuna kitu kinaitwa Soul Mates, na hii ndio subject matter ya uzi wangu huu.

Mahusiano ya Mapenzi, ya Aina Mbili Kuna Mapenzi ya Mwili, na Mapenzi ya Roho ambayo Ndio Mapenzi ya Kweli.
Kama ulivyo mwili una mwili wa nyama, na mwili wa roho, vivyo hivyo kwenye mapenzi, kuna mapenzi ya mwili, physical love, na mapenzi ya Roho, spiritual love, emotional love.
Mapenzi ya physical love, ni yale mapenzi ya mambo ya mwilini, yanajumuisha mapenzi ya kutamani mwili na kufanya lile tendo la sex, sometimes ni needs, tamaa, infatuation, kila kiumbe mwenye viungo timilifu vya uzazi, anaweza kufanya physical love na kuridhika na tendo na kutoshelezeka, mechanically, lakini hakuna emotional na spiritual love, na hiki ndicho mara nyingi hufanyika kwenye biashara ya mapenzi, wale wadada wanaojiuza, hufanya physical love tuu kwa uhitaji wa pesa, lakini hakuna true love, emotional love wala spiritual love.

Mapenzi ya Kweli ni zaidi ya Sex, ni True love, Emotional na Spiritual.
Ili kupata mpenzi wa kweli na kufanya mapenzi ya kweli, yule mpenzi unaekutana nae lazima awe ndie soul mate wako uliyepangiwa ile siku unazaliwa. Yaani mtu uliyeumbiwa wewe kuwa parner wako wa maisha ya kimwili na kiroho, hivyo mkifanya sex, sio tuu mnafanya tendo, bali mnaunganika na kuwa mwili mmoja in spiritual body, na kutengeneza a special bond, hivyo mahusiano ya hivi, mmoja akitangulia, yule aliyebaki duniani hawezi kuishi muda mrefu, atamfuata tuu mwenzake, na mapenzi yao yataendelea kwenye the spiritual world kutokana na ile bond ambayo haiwezi kukatika.

Je Utajuaje Mpenzi Uliyenae Kama Ndie Soul Mate Wako?.
Haya sasa ni mambo ya Roho, naomba nisiyazungumze hapa.

Roho za Wafu, Zinaweza Kuziita Roho za Walio Hai Au Walio Hai, Wakajipeleka Wenyewe Kifoni.
Watu walikufa ambao roho zao zinaishi kwenye ulimwengu wa Roho, wanaweza kuwaita watu wowote wenye strong bond nao, kutoka duniani na kuwafuata kifoni, wengi wa watu wanaitwa kwa namna hii, hufa ghafla. Wengi ni pale mmoja anapotangulia, mwingine hawezi ku recover hivyo ni ama ni yeye mwenyewe aliye hai anaona maisha bila ya mwenzake hayana maana, hivyo kutamani kumfuata, ama aliyekufa anamuita mwenza wake kifoni, hivyo mwenza kumfuata. Hii pia hutokea kwa identical twins kama wanaushi karibu, na twin mmoja akitangulia, kuna mila inafanywa ili kumkinga twin aliyebaki asimfuate.

Hivyo kama ni kweli Ephraim Kibonde alisema mke wake ni soul mate wake, usikute Ruge ndio alikuwa kila kitu kwa Ephraim Kibonde, hivyo baada ya kifo cha mke wake, Ephraim aliweza kuendelea kuishi kwa vile Ruge yupo, ilipotokea na Ruge amekufa, katika kuushughulikia msiba huo, roho ya Ruge na Roho ya Mke wa Kibonde, zikakutana na kumuita Ephraim kuwa sisi tuko huku, wewe huko unangoja nini?, hivyo Roho ya Ephraim, ikasikia sauti hizo, na yeye mwenyewe ku will, kuwa nitawafuata. Baada ya ku will kuwa uko tayari kuwafuata, powers of will hutafuta sababu yoyote ya kukuchomoa, kikawaida ikikosekana sababu yoyote, iwe ni ugonjwa wa ghafla, ajali, or majanga yoyote ya kuondoa roho, then mtu alikuwa ni mzima, analala usingizini, kesho yake haamki. Pamoja na uwepo wa hiyo bond, ili kumfuata aliyetangulia ni lazima will yako ikubali.

Hitimisho.
Kwa vile kwa sisi binadamu wote hapa duniani tuko safari tuu, kuelekea kwenye maisha ya milele, tusiwalilie waliotangulia na kuhuzunika saana kwa kuwakosa, tuhunike kibinaadamu, tulie kwa kiasi, maisha ni lazima yaendelee, bali tujiangalie sisi wenyewe, kwa nafsi zetu, jee tumejiandaa kuitika wito wakati siku yetu na saa yetu ikitakapofika?.

Kesheni mkiomba kwa maana hamjui siku wala saa.
RIP Ephraim Kibonde na Ruge Mutahaba na wengine wote waliotangulia, nyinyi mbele sisi tuko nyuma yenu, sote sisi ni wa Kwake na Kwake tutarejea.

Paskali
Rejea
Life after Death: What Happens after Death? - JamiiForums

Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, Wewe Unazo? - JamiiForums

"Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu za Kufanya Miujiza Ya Uponyaji kwa Imani!. -Kila Mtu Anazo! - JamiiForums

Life After Life: Regia Mtema (RIP) Amerejea Bungeni Kiaina? - JamiiForums
Paschal Bwana leo nimecheka sana
Wafu unawazuia kwa Maombi, Mama yangu alikuwa best friend wangu, amefariki namuota kila week lakini haji kuniambia njoo huku nilipo ananiambia "SIJAFA NIPO HAI"
Maombi yanasaidia kufukuza Miroho ya kuchukua binadamu wengine kabla ya wakati wa Mungu kukuondoa Duniani
ingekuwa ni hivyo umeandika mimi ningeshakufa muda sana lakini mpaka leo nadunda na Mama yangu hajawahi kuniambia njoo huku.

Biblia unayoibeba Kila j2 kwenda Kanisani inasema, ". HAKUNA SHIRIKA KATI YA WAFU NA WALIO HAI"
Ukiweza kusimama huo msitari kwenye maombi WAFU hutowaona tena, roho yako itakuwa na Amani siku zote
Au sio Pastor Ekuweme Mung Chris ?

Cc: 50thebe joanah moneytalk lara 1 Smart911
 
Paschal Bwana leo nimecheka sana
Wafu unawazuia kwa Maombi, Mama yangu alikuwa best friend wangu, amefariki namuota kila week lakini haji kuniambia njoo huku nilipo ananiambia "SIJAFA NIPO HAI"
Maombi yanasaidia kufukuza Miroho ya kuchukua binadamu wengine kabla ya wakati wa Mungu kukuondoa Duniani
ingekuwa ni hivyo umeandika mimi ningeshakufa muda sana lakini mpaka leo nadunda na Mama yangu hajawahi kuniambia njoo huku.

Biblia unayoibeba Kila j2 kwenda Kanisani inasema, ". HAKUNA SHIRIKA KATI YA WAFU NA WALIO HAI"
Ukiweza kusimama huo msitari kwenye maombi WAFU hutowaona tena, roho yako itakuwa na Amani siku zote
Au sio Pastor Ekuweme Mung Chris ?

Cc: 50thebe joanah moneytalk lara 1 Smart911

Honey Money Penny maisha ya kimwili (physical) yanaanzia rohoni (spiritual). Ni somo gumu kidogo linalotaka ustahimilivu kulisoma, kulichambua na kulitafakari. Mfano rahisi ni ile nyota ya mashariki waliyoaiona mamajusi zama zile. Waliona mfalme katika roho. Tunajua Herode alifanya nini.

Yusuph mwana wa Jacob alipokuwa Misri aliishi kwenye ulimwengu wa roho. Uthibitisho ni uwezo wake kufasiri ndoto. Ndoto ni lango la maisha ya kiroho yanayotokea katika mwili (physical world)

Inapotokea unaota unawasiliana na watu waliofariki, ima unawafahamu ila lah, sio rahisi kuhitimisha maana ya ndoto husika. Maana ndoto sio jambo la kubeza. Ndiposa wanasema "Dream come true!"
 
Mama Mercy alikuwa soul mate wa mzee Mengi, ila binadamu ni wabishi sana.
Daisy Llilies, hapa tunazungumzia hypothetical situation please usitaje majina ya watu ili usije kuwa hurt wafiwa, maana sisi Waafrika unakuta mtu ana soul mates, hivyo soul mate mmoja akamuita na kuitikia, hivyo kumfuata, soul mate mmoja na kumuacha soul mate mwingine, hivyo huyo soul mate aliyebakia naye anaweza kuitwa kwenda kuendeleza threesome.

Haya mambo ya soul mate ni very hard to comprehend.

P
 
Back
Top Bottom