Life After Life: Je, Wafu huwaita watu kifoni? Kuna walio hai huamua kuwafuata Wafu? Wapenzi mmoja akitangulia, mwenzake anafuata!

Mkuu Magallah, mwili ukiishafukiwa ardhini, unaoza na kugeuka kuwa mavumbi, kaburi ni ishara tuu, as just an rv ya kukutania, lakini roho zinakwenda kwenye ulimwengu wa roho, huko hakuna tena mass, distance wala time, kwa vile roho ni semu ya Mungu, then roho hizo ni omnipotent, omnipresent na omniscience.

Kitendo cha wamama wajawazito kwenda kaburini, vichanga vinamawasiliano na ulimwengu wa Roho, hivyo its just superstition tuu kuwa vikienda makaburini ndio vitaitwa, vinaweza kuitwa tuu vikiwa popote, ila kule kuona makundi ya watu wakilia, wakihuzunika, vinaweza kushawishika, kwa nini nije duniani kisha nije kuliza watu?, bora...
P.
Wewe bwana mayalla utakua Mtu wa system ya usalama au majeshi hilo neno "rv" ulilotumia hapo juu ni neno la kijeshi na kijasusi likimaanisha rendezvous mahali ambapo wanajeshi wanakutana wakiwa kwenye uwanja wa kivita au military mission kwa ajili ya kupeana brief.

Watu wa usalama wa taifa, wanajeshi ndio keyword yao hiyo rv.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi,
Kifo cha Ephraim Kibonde kimeibua simanzi kubwa kwa sababu katika uhai wake hakuwahi kuugua, amekufa ghafla, hivyo watu kubaki na maswali mengi.
Katika bandiko la Tribute to Kibonde, kuna mwana JF kaandika maneno haya kumhusu Kibonde.

Kufuatia kuyasoma hayo, nimeona nizungumze kitu kuhusu uhai, kifo na maisha baada ya kifo.

Uhai ni Nini na Kifo ni Nini?.
Mwili wa binadamu una sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni huu mwili wa nyama, ambao umeumbwa kwa mavumbi, na siku ukifa, kinachokufa ni mwili huu wa nyama, unazikwa kaburini, humo ndani unaoza na kurudi kuwa mavumbi. Sehemu ya pili ya mwili ni uhai, uhai hii ni pumzi Mungu aliyoipulizia kwenye ule udongo hivyo mwili kupata uhai. Hii ni Roho ya Mungu, the spiritual body, the astra body, mwili unapokufa, roho haifi, bali huacha mwili na kurudi kwa Mungu. Hivyo kifo ni kitendo cha roho kuacha mwili.

Jee Baada ya Kifo, hiyo Roho inakwenda Kuishi Wapi?.
Kama ulivyo mwili una sehemu mbili ya mwili wa nyama na mwili wa roho, vivyo hivyo dunia ina sehemu mbili, Ulimwengu wa Kidunia, the physical world, na Ulimwengu wa Roho, the Spiritual World, mtu akifa, roho ikiacha mwili, mwili unabaki kwenye ulimwengu wa dunia, unazikwa unaoza na kugeuka kuwa mavumbi, Roho inakwenda kwenye ulimwengu wa Roho kuendeleo kuishi milele, being mbinguni, peponi, kuzimu, toharani, au jehanum kwenye moto wa milele, hii subject nyingine lakini roho hazifi kwa sababu roho ni Mungu.

Jee Roho za Waliokufa Zinaweza Kuwaita Walio Hai?.
Jibu ni yes, ndio maana kwa baadhi ya mila, wamama wajawazito hawaruhusiwi kwenda makaburini, ili waliolala wasije wakaviita vichanga, na matokeo yake vikaitika na kupata still born.
Kwenye mahusiano kuna kitu kinaitwa Soul Mates, na hii ndio subject matter ya uzi wangu huu.

Mahusiano ya Mapenzi, ya Aina Mbili Kuna Mapenzi ya Mwili, na Mapenzi ya Roho ambayo Ndio Mapenzi ya Kweli.
Kama ulivyo mwili una mwili wa nyama, na mwili wa roho, vivyo hivyo kwenye mapenzi, kuna mapenzi ya mwili, physical love, na mapenzi ya Roho, spiritual love, emotional love.
Mapenzi ya physical love, ni yale mapenzi ya mambo ya mwilini, yanajumuisha mapenzi ya kutamani mwili na kufanya lile tendo la sex, sometimes ni needs, tamaa, infatuation, kila kiumbe mwenye viungo timilifu vya uzazi, anaweza kufanya physical love na kuridhika na tendo na kutoshelezeka, mechanically, lakini hakuna emotional na spiritual love, na hiki ndicho mara nyingi hufanyika kwenye biashara ya mapenzi, wale wadada wanaojiuza, hufanya physical love tuu kwa uhitaji wa pesa, lakini hakuna true love, emotional love wala spiritual love.

Mapenzi ya Kweli ni zaidi ya Sex, ni True love, Emotional na Spiritual.
Ili kupata mpenzi wa kweli na kufanya mapenzi ya kweli, yule mpenzi unaekutana nae lazima awe ndie soul mate wako uliyepangiwa ile siku unazaliwa. Yaani mtu uliyeumbiwa wewe kuwa parner wako wa maisha ya kimwili na kiroho, hivyo mkifanya sex, sio tuu mnafanya tendo, bali mnaunganika na kuwa mwili mmoja in spiritual body, na kutengeneza a special bond, hivyo mahusiano ya hivi, mmoja akitangulia, yule aliyebaki duniani hawezi kuishi muda mrefu, atamfuata tuu mwenzake, na mapenzi yao yataendelea kwenye the spiritual world kutokana na ile bond ambayo haiwezi kukatika.

Je Utajuaje Mpenzi Uliyenae Kama Ndie Soul Mate Wako?.
Haya sasa ni mambo ya Roho, naomba nisiyazungumze hapa.

Roho za Wafu, Zinaweza Kuziita Roho za Walio Hai Au Walio Hai, Wakajipeleka Wenyewe Kifoni.
Watu walikufa ambao roho zao zinaishi kwenye ulimwengu wa Roho, wanaweza kuwaita watu wowote wenye strong bond nao, kutoka duniani na kuwafuata kifoni, wengi wa watu wanaitwa kwa namna hii, hufa ghafla. Wengi ni pale mmoja anapotangulia, mwingine hawezi ku recover hivyo ni ama ni yeye mwenyewe aliye hai anaona maisha bila ya mwenzake hayana maana, hivyo kutamani kumfuata, ama aliyekufa anamuita mwenza wake kifoni, hivyo mwenza kumfuata. Hii pia hutokea kwa identical twins kama wanaushi karibu, na twin mmoja akitangulia, kuna mila inafanywa ili kumkinga twin aliyebaki asimfuate.

Hivyo kama ni kweli Ephraim Kibonde alisema mke wake ni soul mate wake, usikute Ruge ndio alikuwa kila kitu kwa Ephraim Kibonde, hivyo baada ya kifo cha mke wake, Ephraim aliweza kuendelea kuishi kwa vile Ruge yupo, ilipotokea na Ruge amekufa, katika kuushughulikia msiba huo, roho ya Ruge na Roho ya Mke wa Kibonde, zikakutana na kumuita Ephraim kuwa sisi tuko huku, wewe huko unangoja nini?, hivyo Roho ya Ephraim, ikasikia sauti hizo, na yeye mwenyewe ku will, kuwa nitawafuata. Baada ya ku will kuwa uko tayari kuwafuata, powers of will hutafuta sababu yoyote ya kukuchomoa, kikawaida ikikosekana sababu yoyote, iwe ni ugonjwa wa ghafla, ajali, or majanga yoyote ya kuondoa roho, then mtu alikuwa ni mzima, analala usingizini, kesho yake haamki. Pamoja na uwepo wa hiyo bond, ili kumfuata aliyetangulia ni lazima will yako ikubali.

Hitimisho.
Kwa vile kwa sisi binadamu wote hapa duniani tuko safari tuu, kuelekea kwenye maisha ya milele, tusiwalilie waliotangulia na kuhuzunika saana kwa kuwakosa, tuhunike kibinaadamu, tulie kwa kiasi, maisha ni lazima yaendelee, bali tujiangalie sisi wenyewe, kwa nafsi zetu, jee tumejiandaa kuitika wito wakati siku yetu na saa yetu ikitakapofika?.

Kesheni mkiomba kwa maana hamjui siku wala saa.
RIP Ephraim Kibonde na Ruge Mutahaba na wengine wote waliotangulia, nyinyi mbele sisi tuko nyuma yenu, sote sisi ni wa Kwake na Kwake tutarejea.

Paskali
Rejea
Life after Death: What Happens after Death? - JamiiForums

Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, Wewe Unazo? - JamiiForums

"Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu za Kufanya Miujiza Ya Uponyaji kwa Imani!. -Kila Mtu Anazo! - JamiiForums

Life After Life: Regia Mtema (RIP) Amerejea Bungeni Kiaina? - JamiiForums

Ukweli + Uongo = Uongo.

Je, unatumia mamlaka gani kuthibitisha hilo?
Kwa wakristo, Biblia haijawahi kuzungumzia uongo wa kiasi hiki.
Ni Kweli binadamu ni muunganiko wa mwili (mavumbi) na pumzi itiayo uzima (roho).

Biblia ina uthibitisho wa kutosha na kupitiliza kuwa Aliyekufa hajui neno lolote.
Pumzi humrudia Mungu, ila ujue pumzi haiwezi kuwa nafsi hai bila Mwili (ambao tayari vimeshatenganishwa).
Ili hiyo pumzi iwe na uwezo wa kufanya lolote lazima iwe ndani ya mwili.
Zaidi ya hayo, mwenye uwezo wa kuamua kukuita leo na ukafa ni Mungu mwenyewe aliyekuumba. Over. Kasome biblia vizuri
 
Write your reply...
baba mdogo alifariki mwaka jana,akamuacha mke na watoto wa tatu na mimi nikiwa wa nne japokuwa sikuwa mtoto wa familia ile niliishi pale miaka kadhaa kwa sababu baba mdogo alikuwa ananifanyia mchongo fulani,lakini alifariki kabla hatujamaliza harakati zetu,r.i.p father
Mwezi mmoja baada ya kifo chake,nakumbuka siku ile mama mdogo aliniamsha mimi na akamuamsha na binti yake wa kwanza kwa kuwa sisi ndo tulikuwa wakubwa,wale wengine wawili walikuwa bado wadogo,nakumbuka ilikuwa alfajiri saa 11,ma mdogo alikuwa anatuhadithia ndoto aliyoota,alimuota marehemu baba mdogo ambaye ndo alikuwa mumewe akiwa na wenzake ambao ye mama mdogo hakuwatambua hao wengine,anasema amemuota akimuita kwa jina lake "----njoo,njoo,njoo"..ma mdogo akaenda akamshika mkono wakawa wanaondoka,ndipo ma mdogo akashtuka ghafla na kuja kutuamsha,
baada ya hapo ma mdogo alimuota marehemu mara kadhaa,sisi hatukujua kitu wakati huo tulimuaminisha ma mdogo kuwa zile zilikuwa ni ndoto tu pia aache kumuwaza mzee afanye maombi aendelee na shughuli zingine..zilipita wiki kadhaa,asubuhi moja ma mdogo hakuamka nilipigiwa simu nikiwa posta natafuta kazi na yule binti yake wa kwanza,nakumbuka nilirudi home fasta aisee ilikuwa siku mbaya sana kwangu kwani sikuwahi kuona mtu wangu wa karibu akiwa amefariki,kwa kuwa nilikuwa na kashule kidogo kichwani,sikuhangaika sana nikawakusanya madogo pembeni,nikawaambia mama kapata mshtuko kidogo atapona ngoja nimuite dokta tumpeleke hospitali..lakini ki-ukweli alikuwa keshafariki tayari

hivyo ktk hii dunia kuna mambo mengi tumefichwa..
 
Mkuu Losser Bad, kwanza ni kweli, aliyetuumba, na kutupa uhai, ndiye pekee mwenye mamlaka kuruhusu Roho iache mwili kwa kifo, mwili urudi kuwa mavumbi na Roho iende kwenye ulimwengu wa roho.

Hayo yote ni mipango na mamlaka ya Mungu, ila zaidi ya miili yetu kuwa na Roho wa Mungu, pia Mungu ametupa utashi, conscious ya kuamua, tumfuate yeye na kuzishika amri zake tuishi milele, au tumfuate shetani na mambo yake, tufe. Wazazi wetu wa mwanzo waliamua kutenda dhambi iliyotuumbia kifo, hivyo japo kifo ni kwa mapenzi ya Mungu, lakini kuna vifo vingi ni mipango ya mwovu shetani, japo anayetoa kibali sasa Roho iache mwili ni Mungu pekee.

Katika ule utashi, conscious Mungu aliotupa kuamua, ndani yake kuna powers za maamuzi zinaitwa "will Powers" ambazo ndicho kitu chenye nguvu kuliko kitu chochote duniani, hizo Will Powers, ni nguvu za Mungu zilizo ndani yetu na kila mtu anazo, nguvu hizi ndizo huamua hatima yetu, nikimaanisha sisi tuna nguvu za Kimungu ndani yetu, na shetani yupo kiturubuni tumuasi Mungu, kwa kutenda dhambi na kumfuata yeye. Mungu baada ya kutupa amri zake, pia ametupa utashi wa kuamua kumfuata yeye Mungu au kumfuata shetani, hivyo kuna baadhi ya matendo ya dhambi tunazotenda, yanasababisha vifo, japo Roho kutoka ni kazi ya Mungu.

Mfano ukiamua kumuua mtu kwa kumpiga risasi, huo ni ushetani, na kikawaida, risasi moja tuu inatosha kutoa roho ya mtu, lakini kama Mungu hajaruhusu Roho ile itoke, hata ukifanya ushetani mkubwa wa kumfyatulia mtu risasi 16, kama Mungu hajaruhusu Roho ile itoke, then mtu huyo atapona, na hata kama ingetokea akafa, huwezi kusema risasi zile ni mpango wa Mungu, no ni mpango wa shetani japo kibali cha Roho kutoka ni kazi ya Mungu

Hivyo kuna vifo vingi ni mipango ya shetani, ajali, maradhi, majanga, etc, na ndani ya vifo hivyo kuna vingine ni mtu mwenyewe ame will afe, kwa kukubali kuitwa na walio kifoni na yeye kukubali, hivyo ugonjwa, ajali, majanga ni kutafuta tuu sababu ya kuhalisha kifo ili tuu mtu uchomoke, lakini unaweza kuitwa kifoni, kwa kupitia will yako ukakataa kuitika, utaendelea kuishi

Watu walio karibu na wagonjwa mahututi, hufikia kipindi, mgonjwa anauona ulimwengu wa roho, anatamka kuwaona baadhi ya watu waliokufa zamani wanamfuata, atawataja kwa majina, kwa vile na nyinyi mko na mgonjwa wenu, na nyinyi hamuwaoni hao watu, basi mnamuona mgonjwa wenu kama anaona maluweluwe kisha mnanuona kama anaweweseka, kumbe ndio safari, kuitwa, kaitika, safari kimoja jumla

P.
Rejea

MAANA YA “ROHO”
Watu fulani hufikiri kwamba “roho” ni neno lingine linalomaanisha “nafsi.” Lakini, si kweli. “Roho” na “nafsi” ni vitu viwili tofauti.

"Mwili bila roho [pneuʹma] umekufa.” "Roho” inamaanisha kile ambacho huupa mwili uhai. Bila roho, mwili umekufa. Kwa hiyo, “roho” ni “nguvu” au kani ya uhai. "Roho” inarejelea nguvu isiyoonekana, inayotendesha viumbe vyote vilivyo hai.

Nafsi na roho hutofautiana. Mwili unahitaji roho kama vile redio inavyohitaji umeme ili kufanya kazi. Kwa mfano, unapotia betri katika redio na kuiwasha, nguvu zilizo katika betri huiwezesha redio kufanya kazi. Hata hivyo, redio haiwezi kufanya kazi bila betri. Hali kadhalika, redio ambayo imeondolewa kwenye umeme haiwezi kufanya kazi. Vivyo hivyo, roho ni nguvu ambayo hutendesha mwili wetu. Kama umeme, roho haiwezi kuhisi wala kufikiri. Ni nguvu isiyo na utu. Lakini bila roho au kani ya uhai, “tunakata pumzi na kurudi kwenye udongo,” kama mtunga-zaburi alivyosema.

Andiko la Mhubiri 12:7 linasema hivi linapozungumzia kifo cha mwanadamu: “Mavumbi [mwili wake] huirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho yenyewe humrudia Mungu wa kweli aliyeitoa.” Roho au kani ya uhai inapoondoka mwilini, mwili hufa na kurudi ulipotoka, yaani, kwenye udongo. Vivyo hivyo, nguvu ya uhai hurudi ilipotoka, yaani, kwa Mungu. Hiyo haimaanishi kwamba nguvu ya uhai huenda mbinguni kihalisi. Badala yake, inamaanisha kwamba mtu akifa, tumaini lolote la kuishi tena linamtegemea Mungu. Ni kana kwamba uhai wake uko mikononi mwa Mungu. Ni kupitia nguvu za Mungu tu ndipo roho au nguvu ya uhai inaweza kurudishwa ili mtu aweze kuishi tena.
 
Write your reply...
baba mdogo alifariki mwaka jana,akamuacha mke na watoto wa tatu na mimi nikiwa wa nne japokuwa sikuwa mtoto wa familia ile niliishi pale miaka kadhaa kwa sababu baba mdogo alikuwa ananifanyia mchongo fulani,lakini alifariki kabla hatujamaliza harakati zetu,r.i.p father
Mwezi mmoja baada ya kifo chake,nakumbuka siku ile mama mdogo aliniamsha mimi na akamuamsha na binti yake wa kwanza kwa kuwa sisi ndo tulikuwa wakubwa,wale wengine wawili walikuwa bado wadogo,nakumbuka ilikuwa alfajiri saa 11,ma mdogo alikuwa anatuhadithia ndoto aliyoota,alimuota marehemu baba mdogo ambaye ndo alikuwa mumewe akiwa na wenzake ambao ye mama mdogo hakuwatambua hao wengine,anasema amemuota akimuita kwa jina lake "----njoo,njoo,njoo"..ma mdogo akaenda akamshika mkono wakawa wanaondoka,ndipo ma mdogo akashtuka ghafla na kuja kutuamsha,
baada ya hapo ma mdogo alimuota marehemu mara kadhaa,sisi hatukujua kitu wakati huo tulimuaminisha ma mdogo kuwa zile zilikuwa ni ndoto tu pia aache kumuwaza mzee afanye maombi aendelee na shughuli zingine..zilipita wiki kadhaa,asubuhi moja ma mdogo hakuamka nilipigiwa simu nikiwa posta natafuta kazi na yule binti yake wa kwanza,nakumbuka nilirudi home fasta aisee ilikuwa siku mbaya sana kwangu kwani sikuwahi kuona mtu wangu wa karibu akiwa amefariki,kwa kuwa nilikuwa na kashule kidogo kichwani,sikuhangaika sana nikawakusanya madogo pembeni,nikawaambia mama kapata mshtuko kidogo atapona ngoja nimuite dokta tumpeleke hospitali..lakini ki-ukweli alikuwa keshafariki tayari

hivyo ktk hii dunia kuna mambo mengi tumefichwa..
Mkuu Massachusetts, kwanza pole sana kwa masahibu yaliyokuta. Kilichomtokea mama yako mdogo, RIP Ma mdogo, RIP, Ba mdogo, ni uthibitisho wa haya nikiyo yaandika. Wenzetu wazungu wanayajua haya siku nyingi, ukikumbwa na majanga ya kumpoteza mwenza ambaye ni soul mate, unahitaji ushauri nasaha, counselling session, toka kwa professionals ili kwanza, ui accept ile hali, uikubali ile hali kuwa mwenzako ametangulia na pili uweze kuibreak ile the invicible cord inayo wa bind together ikatike, Roho ya marehemu ipumzike kwa amani katika ulimwengu wa roho na kuacha kuwatokea ndotoni wenzi wao walio hai na kuwaita wawajoin kifoni.

Tatizo kubwa linalo waathiri wajane na wagane, ni upweke unaosababishwa na denials ya kuto accept kuwa mwenza ametangulia, hivyo kujikuta watu wanaishi na marehemu bila kujijua. The best way around ni acceptance, na kukubali life has to go on, hivyo to break the bond na mwenza aliyetangulia

Wazungu walipokuja Africa, walitukuta na mila na tamaduni zetu za kudeal na mambo haya, baadhi ya mila zilikuwa nzuri na baadhi zilikuwa mbaya, wao wakaziponda mila zetu zote na kuziita ni za kishenzi. Moja ya mila hizi ni caretakers kwa wajane na wagane. Mke aliyefiwa alikuwa anarithiwa faster, na mume anaoa tena hivyo to cut the ties na marehemu.

Kuna kitu nimekisisitiza kwenye hili, ni will power na acceptance ya aliyebaki kukubali kuitwa, kuitikia ndipo sababu ya justifying kifo hufuata, be ugonjwa, ajali or just usingizini.

On the other way around, pia there are some strange ways, the dead wana help out hao watoto wao yatima walio waacha kwa kutoa mafanikio ya ajabu kwa ndugu waliobakia ili wasishindwe, huku hao watoto wakipata akili za ghafla za kufanya vizuri shuleni hadi walimu wanashangaa. Au wajane wanapata mafanikio ya ajabu baada ya kufiwa, hii nayo ni mada ya kujitegemea.
P.
 
Imani ni ujinga, ili uamini lazima ukubali kuwa mjinga

Mada yako imeanza kujengwa na jambo ambalo we mwenyewe mtoa mada sidhani kama una uhakika nalo, unaposema
Wanabodi,
Kifo cha Ephraim Kibonde kimeibua simanzi kubwa kwa sababu katika uhai wake hakuwahi kuugua, amekufa ghafla, hivyo watu kubaki na maswali mengi.
Katika bandiko la Tribute to Kibonde, kuna mwana JF kaandika maneno haya kumhusu Kibonde."
Kweli kibonde katika maisha yake hajawahi kuugua? Amekufa ghafla au ameugua ghafla? Maana kama kahangaikiwa hospitali siku tatu utasemaje amekufa ghafla?
Jamaa ugonjwa wa moyo ndo umempeleka na sio kwamba umeanza siku hiyo wewe utasemaje hajawahi kuugua?
Kama umeanza na jambo la kufikirika basi yote katika maandishi yako hayana uhalali, uhalali wake umeharibiwa na mfano huu ulioutoa
 
MAANA YA “ROHO”
Watu fulani hufikiri kwamba “roho” ni neno lingine linalomaanisha “nafsi.” Lakini, si kweli. “Roho” na “nafsi” ni vitu viwili tofauti.

"Mwili bila roho [pneuʹma] umekufa.” "Roho” inamaanisha kile ambacho huupa mwili uhai. Bila roho, mwili umekufa. Kwa hiyo, “roho” ni “nguvu” au kani ya uhai. "Roho” inarejelea nguvu isiyoonekana, inayotendesha viumbe vyote vilivyo hai.

Nafsi na roho hutofautiana. Mwili unahitaji roho kama vile redio inavyohitaji umeme ili kufanya kazi. Kwa mfano, unapotia betri katika redio na kuiwasha, nguvu zilizo katika betri huiwezesha redio kufanya kazi. Hata hivyo, redio haiwezi kufanya kazi bila betri. Hali kadhalika, redio ambayo imeondolewa kwenye umeme haiwezi kufanya kazi. Vivyo hivyo, roho ni nguvu ambayo hutendesha mwili wetu. Kama umeme, roho haiwezi kuhisi wala kufikiri. Ni nguvu isiyo na utu. Lakini bila roho au kani ya uhai, “tunakata pumzi na kurudi kwenye udongo,” kama mtunga-zaburi alivyosema.

Andiko la Mhubiri 12:7 linasema hivi linapozungumzia kifo cha mwanadamu: “Mavumbi [mwili wake] huirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho yenyewe humrudia Mungu wa kweli aliyeitoa.” Roho au kani ya uhai inapoondoka mwilini, mwili hufa na kurudi ulipotoka, yaani, kwenye udongo. Vivyo hivyo, nguvu ya uhai hurudi ilipotoka, yaani, kwa Mungu. Hiyo haimaanishi kwamba nguvu ya uhai huenda mbinguni kihalisi. Badala yake, inamaanisha kwamba mtu akifa, tumaini lolote la kuishi tena linamtegemea Mungu. Ni kana kwamba uhai wake uko mikononi mwa Mungu. Ni kupitia nguvu za Mungu tu ndipo roho au nguvu ya uhai inaweza kurudishwa ili mtu aweze kuishi tena.
Naunga mkono hoja, kuwa Roho ni kama battery ndio yenye kuchaji mwili. Mwili bila Roho ni just an empy shells, lakini Roho is not just a charger, it has power of life force, ndio uhai, and there is duality, kwa kuwepo miili miili miili, the physical body ndio huu mwili wa nyama umeumbwa kwa mavumbi, na mavumbini utarudi, na kuna spiritual body ambayo haifi na ndio hiyo itakayo fufuka siku ya mwisho ya ufufuko wa miili, usidhani ni ule mwili wa mavumbi ndio utajikusanya tena na kufufuliwa, ukiisha kufa, the physical body is nothing, ndio maana wenzetu waelewa, wanafanya creamation tuu, haya ya kuzikana kwenye majeneza mazuri, makaburi mazuri hadi kujengea, ni kwa ajili tuu ya ku please nafsi zetu sisi tuliobaki

Kwenye hiyo duality haianzi kwenye mwili wala haiishi kwenye mwili, inaanzia kwa Mungu Mwenyewe, kuna Mungu na Shetani, almost everything God can do, shetani can do, except kuumba uhai na kuutoa, hivyo the concept of the God is Power, nguvu za Mungu, the Powers of light, hizi ni nguvu za mema yote duniani na shetani pia ana command the powers of darkness, ni nguvu za giza , ndizo nguvu za uovu wote, tena shetani ni very tricky, mara nyingi huji disguised as Angels or God, hivyo kuna wengi wana mwabudu shetani bila kujijua wakidhani ndio Mungu, wanafanya miujiza kwa jina lake, wanapata mafanikio makubwa ya dunia hii, mali na utajiri, huku wakihubiri neno la Mungu kupitia vitabu vitakatifu lakini sio Mungu.

Duality hii pia iko kwenye Roho ni ya Mungu, ndani ya Roho kuna nafsi, conscious ambayo tumepewa utashi wa kuamua kuchagua tumfuate Mungu au shetani, hivyo kabla hujafikia uamuzi wowote ndani ya nafsi yako, (wengine wanasema ndani ya moyo wako), kuna sauti mbili, the soft one and the noisy one. The soft one ndio sauti ya Mungu ndani yetu, na the noisy one ni sauti ya shetani.

Hata baada ya kiama pia kuna duality ya mbingu mpya na dunia mpya.

Hii duality ina exist in almost everything kuanzia hasi na chanya, Wachina wana Ying na Yang, male na female, tajiri na masikini, mbingu na ardhi etc

P
 
Imani ni ujinga, ili uamini lazima ukubali kuwa mjinga

Mada yako imeanza kujengwa na jambo ambalo we mwenyewe mtoa mada sidhani kama una uhakika nalo, unaposema
Wanabodi,
Kifo cha Ephraim Kibonde kimeibua simanzi kubwa kwa sababu katika uhai wake hakuwahi kuugua, amekufa ghafla, hivyo watu kubaki na maswali mengi.
Katika bandiko la Tribute to Kibonde, kuna mwana JF kaandika maneno haya kumhusu Kibonde."
Kweli kibonde katika maisha yake hajawahi kuugua? Amekufa ghafla au ameugua ghafla? Maana kama kahangaikiwa hospitali siku tatu utasemaje amekufa ghafla?
Jamaa ugonjwa wa moyo ndo umempeleka na sio kwamba umeanza siku hiyo wewe utasemaje hajawahi kuugua?
Kama umeanza na jambo la kufikirika basi yote katika maandishi yako hayana uhalali, uhalali wake umeharibiwa na mfano huu ulioutoa
Mkuu Mnyikungu, kwanza uko very right kuita imani ni ujinga, kwasababu ujinga ni ile hali ya kutojua, hata wale wasio amini uwepo wa Mungu, atheists, wanatuona ni wajinga, sisi wote tunaoamini Mungu. Hivyo kwa jambo usililolujua kuliona ni ujinga ni haki yako. Hata Galilei Galileo, baada ya kugundua telescope, na kuangalia kivuli cha dunia siku ya kupatwa kwa jua, na mwezi, akatoa andiko kuwa dunia, mwezi na jua, zote ni duara. Kwanza alionekana mjinga, kisha akahukumiwa kifo kwa kunyongwa kwa kosa la kumkosoa Mungu, wakiamini Mungu aliumba dunia ni bapa. Hivyo you're very right kwako imani ni ujinga.

Pili haya mambo ninayo yazungumzia katika bandiko hili, sio mambo ya dunia hii au ulimwengu huu wa physical world, mimi hapa nazungumzia ulimwengu wa Roho. Huu ni ulinwengu mengine wa hypothetical existence, ambao ni only kwa watu deep thinkers tuu ndio wanaweza nielewa, sisi wengine wetu wenye vichwa panzi, kwao huu utakuwa ni ujinga tuu, hivyo ninakuelewa sana unapoita imani ni ujinga.

Best wa Ephraim Kibonde, Gadner G Habash ndie aliyethibitisha kuwa tangu wamefahamiana na Ephraim Kibonde, hajawahi kuwa ni mtu wa kuumwa umwa. Lakini baada ya kifo cha mkewe, kwanza ile nyumba yao ikawa haikaliki, ilikuja kuwa a haunted house, jee unajua haunted house ni nini?. Akasema Ephraim Kibonde alilazimika kuhama na kuacha kila kitu, na kurejea kuishi kwa wazazi.

Baada ya msiba wa Boss Ruge, sote tulimshuhudia Kibonde akiendesha shughuli, hadi mazishi.

Dr. Issac Maro ndio akikuwa na Kibonde hadi saa yake ya mwisho, ila akipohojiwa, alisema Ephraim Kibonde hakuwahi kumaliza msiba wa mkewe, means ku accept, na Dr. Maro akasisitiza Kibonde alihitaji counseling.

Mimi ninachosema kwenye bandiko hili, kuna kuitwa, ukiitwa ukiisha itika na kukubali kwenda kumfuata, that is done, kitakacho fuata ni sahabu tuu za kuondokea ndizo zinatafutwa iwe ni kwa ugonjwa, ajali au sababu yoyote kuhalalisha mtu kuchomoka, na ikikosekana kabisa sababu yoyote, then mtu anachomokea usingizini, alikuwa mzima kabisa, haumwi chochote, na asubuhi mtu anakutwa alichomoka usingizini.

RIP Ephraim Samson Kibonde

Mkuu unayejiita mwenye akili kubwa, kuna tofauti sana kufananisha na Alivyoandika Galileo na hivi vyakwako, Galileo aliandika vitu ambavyo haviko kwenye dhahania vinathibitishika, wewe umeandika vitu ambavyo ni imani tu kuthibitisha uhalisia wake haiwezekani zaidi ya porojo nyingi.

Kibonde kukimbia nyumba yake si sababu ya kufanya mimi niamini andiko hili, hapo ukisoma vizuri maandiko yako haya ulipomnukuu Dr Isack Maro utagundua kibonde alikuwa Mhanga mkubwa wa msongo wa mawazo, huo ni ugonjwa ambao umeuthibitisha mwenyewe, pili ni kawaida kabisa mtu asipokubaliana na kuamini kama mwenza wake kafa huwa hawezi kudumu muda mrefu, hiyo huwapata wanandoa wengi tu ambao hushindwa kurwjerea kwenye maisha ya kawaida na kusahau juu ya vifo vya wenza wao.hivyo bado nasisitiza kibonde hakufa ghafla.

ukimsikiliza gadna basi kawaulize kanisa katoliki kwanini hawakuchukua kitabu cha Tomaso kukiingiza kwenye bilblia ilhali naye aliandika, waliogopa habari za mihemko ambazo huwa zinatia chumvi kwenye mambo mengi.

Mwisho unayoyaandika yapo sana lakini mfano wako hauendani, kuna mazingira mawili yanaweza kutokea kuna kuitwa unakokusema wewe na kuna kuitwa kunakotokana na kula yamini na mwenza wako ama rafiki yako. Hapa wakati wa msiba wa Kingunge wengi waliisema sana hii kuwa huenda alikula yamini na mkewe.
 
Naona tunazunguka tuu na kurudi kule kule, nimesema ukiisha itwa ukakubali kuitika, then kinachofuatia ni kutafutwa sababu ili kuhalalisha, you can just call them what you may, be it usongo wa mawazo, yamini, ugonjwa etc, lakini the bottom line is safari, you go to follow.

Unaodhani yamini ni nini?. Katika bandiko hili nimeeleza mtu unaweza kuitwa, au usiitwe bali wewe mwenyewe ukaamua kujipeleka, hii hutokea zaidi kwa wazee waliozeeka pamoja, mmoja akitangulia, mengine anaona life has no meaning to him/her, mengine huita watoto wake wote na kuwaaga, kisha huondoka peacefully akiwa usingizini.

Nakubaliana na wewe kuna vitu ni dhana tuu, havina any scientific evidence or proof of existence ikiwemo uwepo wa Mungu, mbingu, peponi na motoni, ni imani tuu, hivyo nakuomba imani za watu usiite ni ujinga.

Sijui ulikuwa na umri gani wakati wa mihadhara yao kashfa, lakini chanzo ni muhubiri kuwa "Yesu sii Mungu", kwenye kadhia ya Mwembechai, mimi ndio nilikuwa reporter on line of fire.

Kuita imani ya mwenzio ni ujinga, umekusababishia kuitwa una akili za kichwa panzi, naona umenirudia kwa neno "unayejiita mwenye akili kubwa", in reality sijajiita popote kuwa mimi ni akili kubwa, nimesema haya mambo ya life after life ni mambo makubwa ya hypothetical situation tuu yanayohitaji viwango fulani vya comprehension, ukiwa ni mwenzangu na mimi, sisi wa type ya vichwa panzi, tutaona ni ujinga tuu.

Naomba tuufunge mjadala kwa kukubaliana kutokubaliana kuhusu causative agents ya chanzo cha safari yake, lakini the facts remain the same, mmoja ametangulia, mwingine akamfuata, they've gone, let their souls rest in peace.
P.
 
Naunga mkono hoja, kuwa Roho ni kama battery ndio yenye kuchaji mwili. Mwili bila Roho ni just an empy shells, lakini Roho is not just a charger, it has power of life force, ndio uhai, and there is duality, kwa kuwepo miili miili miili, the physical body ndio huu mwili wa nyama umeumbwa kwa mavumbi, na mavumbini utarudi, na kuna spiritual body ambayo haifi na ndio hiyo itakayo fufuka siku ya mwisho ya ufufuko wa miili, usidhani ni ule mwili wa mavumbi ndio utajikusanya tena na kufufuliwa, ukiisha kufa, the physical body is nothing, ndio maana wenzetu waelewa, wanafanya creamation tuu, haya ya kuzikana kwenye majeneza mazuri, makaburi mazuri hadi kujengea, ni kwa ajili tuu ya ku please nafsi zetu sisi tuliobaki

Kwenye hiyo duality haianzi kwenye mwili wala haiishi kwenye mwili, inaanzia kwa Mungu Mwenyewe, kuna Mungu na Shetani, almost everything God can do, shetani can do, except kuumba uhai na kuutoa, hivyo the concept of the God is Power, nguvu za Mungu, the Powers of light, hizi ni nguvu za mema yote duniani na shetani pia ana command the powers of darkness, ni nguvu za giza , ndizo nguvu za uovu wote, tena shetani ni very tricky, mara nyingi huji disguised as Angels or God, hivyo kuna wengi wana mwabudu shetani bila kujijua wakidhani ndio Mungu, wanafanya miujiza kwa jina lake, wanapata mafanikio makubwa ya dunia hii, mali na utajiri, huku wakihubiri neno la Mungu kupitia vitabu vitakatifu lakini sio Mungu.

Duality hii pia iko kwenye Roho ni ya Mungu, ndani ya Roho kuna nafsi, conscious ambayo tumepewa utashi wa kuamua kuchagua tumfuate Mungu au shetani, hivyo kabla hujafikia uamuzi wowote ndani ya nafsi yako, (wengine wanasema ndani ya moyo wako), kuna sauti mbili, the soft one and the noisy one. The soft one ndio sauti ya Mungu ndani yetu, na the noisy one ni sauti ya shetani.

Hata baada ya kiama pia kuna duality ya mbingu mpya na dunia mpya.

Hii duality ina exist in almost everything kuanzia hasi na chanya, Wachina wana Ying na Yang, male na female, tajiri na masikini, mbingu na ardhi etc

P

OK "Duality"

Pia, Existence - inexistence
Life - death

Mzunguko ⤵

1= Inexistence
2= Existence
3= Life / living
4= Death
5= Inexistence

Wakati sijazaliwa sikuwa popote, kinyume chake nikawepo nilipozaliwa.

Vilevile, napotaka kuwasha moto wa mshumaa kiuhalisia moto haupo hadi nitakapowasha moto. Nitakapozima, moto na mwanga wake hupotea. Sasa moto na mwanga huenda wapi?

Naweza fananisha, binadam kuanza kufanyizwa tumboni mwa mwanamke ni kama uwepo wa mshumaa. Kuzaliwa ni kuwashwa kwa mshumaa, ambapo moto wa mshumaa ndio roho. Mshumaa unapozimwa au unapozima hakuna moto tena ( hakuna roho - uhai - tena). Kama moto, roho haina makazi tena. Kwa maana iliyowazi roho ya binadamu ni pumzi yake.

Mtu akifa, uhai wake unakoma. Kifo ni kinyume cha uhai. Kwa hiyo, mtu akifa haendelei kuishi mahali pengine, hisia na mawazo yake hupotea.Tukifa hatuwezi kuona, kusikia, wala kufikiri.

Swali : Wanyama pia wana roho, je wakifa roho zao huenda wapi?
Kama zinakuwa sehemu, zinafanya nini?

Maana mbili za roho

1. ROHO ~ nomino

: Pumzi, inayopelekea uhai wa binadamu.

2. ROHO ~ nomino

: Viumbe visivyoonekana Mf. Malaika,Mapepo,Jini,Shetani.
Ambao wapo mamilioni. Huwa havina miili maalumu ila vina uwezo wa kujivika miili ya nyama au kutumia mwili wa nyama.
 
Naona tunazunguka tuu na kurudi kule kule, nimesema ukiisha itwa ukakubali kuitika, then kinachofuatia ni kutafutwa sababu ili kuhalalisha, you can just call them what you may, be it usongo wa mawazo, yamini, ugonjwa etc, lakini the bottom line is safari, you go to follow.

Unaodhani yamini ni nini?. Katika bandiko hili nimeeleza mtu unaweza kuitwa, au usiitwe bali wewe mwenyewe ukaamua kujipeleka, hii hutokea zaidi kwa wazee waliozeeka pamoja, mmoja akitangulia, mengine anaona life has no meaning to him/her, mengine huita watoto wake wote na kuwaaga, kisha huondoka peacefully akiwa usingizini.

Nakubaliana na wewe kuna vitu ni dhana tuu, havina any scientific evidence or proof of existence ikiwemo uwepo wa Mungu, mbingu, peponi na motoni, ni imani tuu, hivyo nakuomba imani za watu usiite ni ujinga.

Sijui ulikuwa na umri gani wakati wa mihadhara yao kashfa, lakini chanzo ni muhubiri kuwa "Yesu sii Mungu", kwenye kadhia ya Mwembechai, mimi ndio nilikuwa reporter on line of fire.

Kuita imani ya mwenzio ni ujinga, umekusababishia kuitwa una akili za kichwa panzi, naona umenirudia kwa neno "unayejiita mwenye akili kubwa", in reality sijajiita popote kuwa mimi ni akili kubwa, nimesema haya mambo ya life after life ni mambo makubwa ya hypothetical situation tuu yanayohitaji viwango fulani vya comprehension, ukiwa ni mwenzangu na mimi, sisi wa type ya vichwa panzi, tutaona ni ujinga tuu.

Naomba tuufunge mjadala kwa kukubaliana kutokubaliana kuhusu causative agents ya chanzo cha safari yake, lakini the facts remain the same, mmoja ametangulia, mwingine akamfuata, they've gone, let their souls rest in peace.
P.
Haya bwana, tuufunge tu mjadala.....maana tumeanza kuonyesha uvichwa panzi wetu kwa kuanza kukashfiana.....
 
Ni kweli kabisa mtu anapokufa mwili ndio unabaki na Roho ndo inatoka kwenda kuvalishwa mwili mwingine maalumu kwaajili ya kusubiri parapanda ya mwisho na hapo Kuhani Mkuu Yesu Kristo ndipo atakapo toa hukumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unataka tuseme watu wasichopenda kusikia
Mkuu Gama, personal health status za watu ni very personal affairs, sisi tunazungumza kile tunachoona, kuona ni kuamini. Alikuwa ok tulimshuhudia akiwa very active tangu Karimjee hadi makaburini, hivyo the next day ukiambia he is no more, its a shocking news na ni ghafla.
Please let his soul rest in peace.
P
 
Back
Top Bottom