Tukio lingine ninalo likumbuka ilikua miaka ya nyuma kidogo, nmemaliza kidato cha nne pale nasubiri kwenda A level,hivyo nikasafiri kwenda Moshi kwa ajili ya likizo hiyo ndefu.... Basi bwana,pale mtaani kukawa na sherehe za kipaimara cjui ubarikio sikumbuki vizuri ambae mdogo ake jamaa angu ndo alikua muhusika so nikaalikwa na huyu mshkaji wangu,ukafika muda wa msosi na utaratibu ni kupanga foleni,yule jamaa angu akawa na mishe mishe hivyo na mimi ikanibidi nipange foleni,imefika zamu yangu basi kuna mama wa kipare alikua ana "save" msosi pale,alinifananisha akaniwakia "kaka umeshachukua chakula pisha wenzio nao wapate kama hujashiba utaongeza mwishoni"...aisee nilijisikia vibaya,kwanza watu wengi,alafu mimi ni mgeni pale tena "kutoka Dar" sa kadri nilivyokua nakataa ndio yule mama anapaza sauti na kuzua taharuki pale,ilibidi niondoke kitendo kilichoaminisha kweli nlikua narudia,nilidhalilika sana na roho iliniuma sana japo yule jamaa angu aliniomba radhi haikusaidia... nilijifungua ndani muda wote na nikahama na mtaa kabisa nikaenda kuishi Moshi mjini kutoka NewLand[emoji24][emoji24]