Life Experience: Jambo gani liliwahi kukutia aibu katika maisha?

Hahaha
 
Duuh pole sana mkuu

uliponaje huo msala?
 
Hiyo ilinitokea miaka kama sita iliyopita, Sikh hiyo nimeenda ukweni kwa Mara ya kwanza kabisa, sasa lile wenge la kuonana na babamkwe( Wakati tunafika hakuwepo,alipiga simu yupo njiani anakuja) Basi nikawa naenda chooni kukojoa.

Ile nafika chooni nakuta kuna mzigo haujasukumwa, duh palepale nikaghairi kujisaidia ile nafungua mlango nitoke uso kwa uso na babamkwe,

A see hata domo lilikuwa zito maana lazima angejua ni Mimi ndiyo nimesababisha, ile anaingia naskia anafyonya. Acha kabisaaa.
 
U made my day, sio kwa kucheka huku mpk watu wananishangaaa[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Dah. Thanks for the laugh.
 
Nakumbuka 2010 nimetoka tbr nameenda biharamulo kwa bibi yangu, sasa usiku nimelala kitanda cha peke angu mkojo ukanibana haswaa kutoka nje naogopa maana ni giza sana yaan full migomba, basi nikajikaza mara usingizi ukanipitia kuja kushtuka alfajiri godoro limeloa plus nguo zangu, aisee niliona aibu ikabidi niamke mapema nikafua mashuka yote na saa moja asubuh nilipanda gari kuelekea muleba kupunguza stress kwa mama mkubwa, nadhan bibi alielewa sema alinikaushia tu
 
Nakumbuka miaka ya nyuma tulitoka kwenye kwaya jamaa mmoja akawa amekula vyakula vingi kwa kuchanganya wakati tukiwa safarini jamaa akabanwa na haja kubwa akaomba gari isimame ili ajisaidie,jamaa alikuwa amepiga bonge ya suti mbaya zaidi alikuwa mwalimu wa kwaya,,mzee baba alivyorudi akarudi amechafua koti la suti kwa pembeni na kinyesi bila yeye kujua,watu ilikuwa ni kucheka tuu [emoji23].nikamwambia jamaa umechafua koti yeye hakujua kama ni uchafu gani akashika ile kushika watu wakacheka gari zime jamaa akakunguta mkono ule mzigo ukiangukia kichwani nikikumbuka hiyo siku nachekaga wenyewe tuu.[emoji23]
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Jitahidi kunywa maji na kula matunda mkuu [emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…