Life Experience: Jambo gani liliwahi kukutia aibu katika maisha?

Life Experience: Jambo gani liliwahi kukutia aibu katika maisha?

Good
 
ilitokea nimekuja dar kwa ndugu yangu aliepanga chumba maeneo ya uswahilini temeke,nyumba ilikua na vijana na mama mwenye watoto wa kike pale,sasa ilitokea siku moja usiku nimeenda kuoga mida ya usiku nikaona sio mbaya nitoe na haja kubwa kabisa,kumbe nimemaliza kujisaidia na maji nimemwaga yalikua machache,asubuh si ndo akaja mwenye zamu kufagia choo akaukatana nayo,kila akimwagia maji mzigo hausogei mbele ikabid aulize tu ni nan alikua wa mwisho si ndo nikatajwa mm..daaahh ilikua fedhea kwa watoto wa kike wale maana mama alikazia neno 'Alf yule kaka ni mwembamba ila ana mavi magumuuuuu' sikumsalimia mpk namaliza likizo naondoka
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji40][emoji40][emoji40]
 
Niliwahi kwenda migahawa koko maeneo flani ivi nikakuta contena la kunawia mikono wameweka pembeni na nyumba ya mtu alafu mgahawa wenyewe uko mbali kidogo mi niliponawa nikaingia nyumba iliyokuwa jirani nikidhani ndio mgahawa wenyewe kumbe nimeingia kwenye geto la Mmama flani ivi.

Sasa mda naingia alikuwa bize anakula alafu kageukia upande wapili wala hakusikia vishindo mda naingia kwa akili za kitoto nilipogumdua kuwa nimeingia kusipo nikapata akili ya kutoka kimyakimya tena...! Kumbe mda natoka ndani yule mama akashtuka nikajifanya kuchomoka mule ndani kwa haraka ndio akaniitia mwizi..mwizi...mwizi asee nikajifanya kukimbia nikaishia mikononi mwa wanainchi wenye hasira kali aisee sitakaa nisahau kilichonipata yaani kuna watu bongo hii hata ukiwa unatoa maelezo hawayazingatii wao ni kupiga tu na kutafta petroli.... Hadi leo nikikuta mwizi anapigwa huwa napenda kusikiliza maelezo yake kama yanaleta logic....Maana ningechomwa moto na sijawahi kuiba wala kutapeli cha mtu!
Hahahaha, nmecheka kwa sauti kubwa ndani ya Mwendokasi lililosheheni raia wa kutosha.
 
we boya sana yani unakata mikucha yako na nail cutter za mtu mwingine magonjwa yote haya.

mimi ilinikuta miaka kadhaa iliyopita ndio nimeajiriwa kwenye kampuni flani hapa dar.jioni nimekaa na mabosi zangu kupata wine kidogo na kujuana vizuri.tulikua tumeweka simu zetu mezani,bahati mbaya nikachukua simu ya bosi mmoja nikatia mfukoni nikijua ni yangu .mara kidogo jamaa akaanza kuulizi simu yake mimi nimetulia tu nikiamini iliyopo mfukoni ni yangu .Dah ilivyobipiwa ikaita kwangu halafu hata hawakunipa nafasi ya kujieleza zaidi ya kila mtu kutunza simu yake kwa umakini,nilijisikia fedheha haielezeki
Dah! Pole sana
 
Moja kwa moja niende katika mada.

Leo asubuhi kama kawaida yangu kuna mahali huwa naenda kunywa chai, ni mgahawa wa jamaa yangu mmoja wa karibu, nimekunywa chai, nilipomaliza nikaona kuna funguo juu ya meza, ambazo ninafahamu ni za jamaa yangu(Nimeshazitumia mara kadhaa kukatia kucha kwa maana zina nail cutter), nikatumia katika kukata kucha.

Nilipomaliza kukata kucha nilipigiwa simu, nikasogea pembeni kuzungumza na simu, nikazungumza na simu kwa muda mrefu, hivyo sikuona umuhimu wa kurudi pale tena maana nimemaliza kunywa chai, kumbe wakati huo nimesahau funguo zile nimeziweka mfukoni, nilipofika nyumbani nimeendelea na shughuli zangu bila kuelewa chochote wala kukumbuka, nimekuja kupigiwa simu na binti kuwa kumbe zile funguo zinahitajika, ndio nikakumbuka kujisachi najikuta na funguo kuwa ninazo mfukoni, na kumbe si za jamaa yangu, kumpigia simu anasema si zake kweli, ni za binti anayefanya kazi hapo mgahawani, ni kwamba zimefanana, tukio hili limeniachia fedheha na aibu kubwa maana moja kwa moja nimeonekana kama nilikuwa nina hila mbaya, na hakuna yoyote ninayeweza kumueleza akaniamini, imebaki kuniuma mwenyewe rohoni, maana ningehusishwa na wizi.


Katika maisha kuna mambo ambayo yanatukuta kwa bahati mbaya bila sisi kutarajia, hayo mambo huwa yanapelekea aibu na fedheha ambayo haistahili kwa kweli, na hata haielezeki kwa mtu kirahisi.

Kama na wewe una kisa chochote tupe hapa tupate funzo kidogo.
kuhusu suala la fedheha na aibu nishazioga sana,,,,,,siku moja nikiwa advance miaka hiyo tulipewa adhabu na makamu mkuu wa shule,tuliambiwa tupalilie bustani za mboga mboga shuleni kutwa nzima,ilipofika mida ya saa saba yule mzee ikabid aje bustanini kutusimamia,alikuja na kiredio kidogo huku anasikiliza DW,kipindi hicho ishu ya escrow ilikuwa very hot na DW ndo walikuwa wanaichambua siku hiyo,yule dingi alitusimamia bhna,taarifa ilipoisha mzee akachomeka headphones kwny redio,akaweka maskioni fresh,sasa sisi tukajua anasikiliza kwa headphones kumbe redio kaizima,aiseeee kuona vile tukajua hawez kusikia maongez yetu,mm nikaanza kumsema,nikawaambia washikaji,,,,, mnajua haya mazee yalisoma kwa shida sana,sasa yanataka hizo shida na sisi wanafunzi wao yanalazimisha tuzpitie,usenge tu huu,wana wakacheka,mwingine akasapot,akatukana kinoma,tukacheka sana ticha yupo kimya,baada ya kazi tukashangaa ticha anatoa headphones na kutuambia tumsikilize,akasema ww buffet na Fulani na Fulani kama nyie ni wanaume rudien maneno mliyoyasema yote,aiseeeee hatukuadhibiwa kwa hilo ila binafsi nliona noma balaa asee
 
Bro wangu ameoa sasa.Alikuwa na demu lake lina msambwanda kinyama.Basi lilivyosikia jamaa anaoa alienda kumfanyia fujo home wote tulikuwepo.Likaanza kubwatuka kuwa jamaa kamla ndogo miaka mingi kwa nini amuoi yeye.Tuliona noma sana.Washua wananiuliza kweli?Nikawaambia mkamuulize bro.Noma sana.
Bro kweli au wewe mwenyewe
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kuna siku ndo nimetoka kireport kazini kama siku mbili 3 hivi nmebaki ofisini mwenyewe si nikaachia hewa chafu pale mara paap Boss huyu hapa ofisi inanuka balaa hakika nilipata fedhehea ya kufa mtu
 
Kilindi nipo chuo nilikuwa naingia masomo ya jioni baada ya job, sasa kutokana na ule uchovu wa kazi mara nyingi kipindi cha lecture siku nyingine nasinzia kutokana na uchovu
Siku moja buana tecture anaendelea na kumetulia tuli mm na kale kausingizi si nikaachia Ushuzi tena ule wa puuuuuu.....[emoji23] i.
Ile nashtuka tu darasa lote wanacheka balaa aisee usingizi uliishia palepale na ile aibu sitokuja kuisahau na kibaya zaidi pembeni nilikuwa nimekaa na demu wangu
 
Kitambo flani nilikuwa na mpenzi mmoja matata sana na uzuri tulikaa mtaa mmoja ila yeye aliajiriwa shirika binafsi na ni karibu na ofisini kwangu.

Binti akawa na tabia akitoka kazini kwake anakuja kunipitia tunakwenda home na gari ya ofisi (serikalini) kwangu. Ambapo ilikuwa ni kawaida coz watu wengi walifanya hivyo hata kwa watoto wao washule pia witumia fursa hiyo kwa kupanda gari za hapo ofisini kurahisisha usafiri.

Mara chache sana Bosi alikuwa anapanda gari za Utawala coz yeye alikuwa na VX lake!! Na gari za utawala zilikuwa cruiser mkonge sita na zilikuwa zinabeba watumishi kwa idara. Idara yangu tulikuwa watatu so gari ilikuwa na nafasi kibao tu.

Kumbe katika hizo mara chache Boss akamuona binti wangu na akamuelewa ila pa kumpatia hana!! So, akawa anabanana nasi kwenye gari ya wasaka tonge na hataki kukaa siti ya mbele ambayo tulikuwa tunamuachia kwa heshima yake (sisi tukajua Boss anapenda sana gari ya idara yetu 😂😂😂 kumbe ana yake)!

Kitendo cha kukaa siti za nyuma na wavuja jasho akafanikiwa kupata contact za binti wangu mrembo na akawa anaimbisha mi bila kujua! Bahati mbaya sana, binti akampa cha mbavu Boss kubwa!!

Bosi akajawa na hasira, akaona njia ya pili baada ya ile ya kwanza kufeli ili kumpata Binti ni kunidhalilisha mbele ya binti ili kunishushia status!

Siku hiyo sina hili wala lile, muda wa kutoka umefika nikasogea garini na mrembo wangu. Kuna staff mwenzangu akachelewa kuja garini dereva akawa anapiga honi asikie aje.

Dereva alipoona jamaa haji akaamua kushuka amfuate ofisini! Lilikuwa kosa kubwa sana!! Aliibuka Boss from nowhere akaanza kunitukana kwanini napiga honi nasumbua na pia si kazi yangu kufanya hivyo!!

Alinitukana sana japo nilijitahidi kumwelewesha kuwa dereva ndiyo kapiga honi hakunielewa! Na kesi zikawa zinahama, zinatoka kwenye honi zinakwenda ofisini zinarudi zinakwenda mtaani zinarudi zinakwenda kwenye umalaya zinarudi huuuuh!!

Dereva akimwambia ni mimi nilipiga honi mkuu, anahamisha kesi inakuja madai ya umalaya mradi matusi na dharau zimtoke!! Niliyakoga siku hiyo sitasahu kabisa!! Dereva akitaka kutoa gari anamwambia ondoa gari langu na wewe nikuonyeshe!!

Nilikaa kimya, nachezea nokia ya tochi zile toleo la kwanza kabisa!! Ilikuwa ndiyo simu hot kabisa kabisa wakati huo!!

Aliporidhika akaondoka zake, garini hakuna mtu aliongea mpaka tunashuka!! Staff zote walitoka nje kuona kunani huko parking!!

Baadae ndiyo Binti ananiambia inawezekana kaamua kufanya hivyo sababu anamtaka kimapenzi, na sms zake akanionyesha!! Pia baada ya kutukana sana akamtumia Binti msg "si ndiyo kibwana chako unachoringia, haya ana nini sasa"

Hii kesi hii kwangu haijaisha kabisa!! Kuna siku akajitusua nikafuma kabrasha analipa vibarua hela ndogo kuliko iliyopitishwa na bodi na kuna allowance alikuwa analipa kidogo kuliko iliyopitishwa kwenye bajeti na bodi kisha inayobaki anapiga!

Nikanyofoa karatasi piga kopi nikamchoma macho makavuu huku anaona!! Kidogo avuliwe ukuu wake kama si kuhonga sana na baada ya hapo nikatafuta ajira kwingine nikasepa!!

Ila bado nikikumbuka naona kama kanidhalilisha jana hivi!! Bado namuwinda, nilimuotea mwanae kwenye harakati flani hivi nikamtosa then nikamwambia kamsalimie baba yako!
Pole sana mkuu. Haya majanga yanayofanana kama ya kwako yanatupata wengi huku makazini hasa ukikuta vibosi visivyojielewa. Ila ulikosea kuhukumu mtoto kwa kosa la baba yake. Hii ni sawa na magaidi, wanakosana na watawala au watu fulani, wanakuja kulipua wananchi au watu wengine wasio na hatia nao.
 
Pole sana mkuu. Haya majanga yanayofanana kama ya kwako yanatupata wengi huku makazini hasa ukikuta vibosi visivyojielewa. Ila ulikosea kuhukumu mtoto kwa kosa la baba yake. Hii ni sawa na magaidi, wanakosana na watawala au watu fulani, wanakuja kulipua wananchi au watu wengine wasio na hatia nao.

Ni pale wamekosa Adamu na Hawa adhabu tunakula sie, tuna uhusiano gani na kosa lao!!?

Basi huo ni mwendelezo wake, jifunze kuishi vyema adhabu/laana hudondokea hata kizazi chako kisichohusika
 
Ni pale wamekosa Adamu na Hawa adhabu tunakula sie, tuna uhusiano gani na kosa lao!!?

Basi huo ni mwendelezo wake, jifunze kuishi vyema adhabu/laana hudondokea hata kizazi chako kisichohusika
Huko sahihi kabisa mkuu. Kuna aina ya dhambi/laana zinaridhishwa kwa vizazi na vizazi lakini siyo kila dhambi/laana. Kuna makosa watu tunafanya inabidi adhabu apatiwe yule yule mtenda kosa/dhambi. Kama si hivyo yaani ikiwa kila kosa langu lazima na mke, baba, mama, watoto wangu nao wahusike hii jamii itakuwa ngumu haitakalika kabisa na kila sehemu itakuwa ni vita isiyoisha. Imagine, mfano baba kaiba sehemu halafu hukumu inatolewa kwa familia yaani yeye baba, mama, watoto, na hata ukoo kama ilivyokuwa huko Mara. Mara wanakatana mapanga familia au ukoo mzima hadi vitoto vinavyo nyonya bado, hii si sawa mkuu. Pia utakubali kuwa hata mimi na wewe pia siyo malaika, hivyo kuna watu tunawakosea. Sasa na wao wakiamishia hasira zao kwa familia na koo zetu kweli itapendeza?

Hivyo sikatai na sishabikii hule upuuzi aliyokufanyia huyo jamaa. Ila kwa kosa kama alilo kufanyia huyo limbukeni unaona kabisa anayesitahili kuadhibiwa ni yeye. Watoto wake unawaonea bure maskini.

.
 
Binamu yangu wa kike aliniingia chumban kwangu bila kubisha hodi kanikuta nimesimamia kucha (nyeto) daaah nilijisikia vibaya nikaapa naacha nyeto lakn wap mpaka saiz ni active member wa chama chetu
Aibu aisee mzee sura yako uliiegesha wapi baada ya tukio?
 
ilitokea nimekuja dar kwa ndugu yangu aliepanga chumba maeneo ya uswahilini temeke,nyumba ilikua na vijana na mama mwenye watoto wa kike pale,sasa ilitokea siku moja usiku nimeenda kuoga mida ya usiku nikaona sio mbaya nitoe na haja kubwa kabisa,kumbe nimemaliza kujisaidia na maji nimemwaga yalikua machache,asubuh si ndo akaja mwenye zamu kufagia choo akaukatana nayo,kila akimwagia maji mzigo hausogei mbele ikabid aulize tu ni nan alikua wa mwisho si ndo nikatajwa mm..daaahh ilikua fedhea kwa watoto wa kike wale maana mama alikazia neno 'Alf yule kaka ni mwembamba ila ana mavi magumuuuuu' sikumsalimia mpk namaliza likizo naondoka
hahahaaa asee umenichekesha sana
 
Back
Top Bottom