Life Experience: Jambo gani liliwahi kukutia aibu katika maisha?

Life Experience: Jambo gani liliwahi kukutia aibu katika maisha?

Hahaha
Bro wangu ameoa sasa.Alikuwa na demu lake lina msambwanda kinyama.Basi lilivyosikia jamaa anaoa alienda kumfanyia fujo home wote tulikuwepo.Likaanza kubwatuka kuwa jamaa kamla ndogo miaka mingi kwa nini amuoi yeye.Tuliona noma sana.Washua wananiuliza kweli?Nikawaambia mkamuulize bro.Noma sana.
 
Niliwahi kwenda migahawa koko maeneo flani ivi nikakuta contena la kunawia mikono wameweka pembeni na nyumba ya mtu alafu mgahawa wenyewe uko mbali kidogo mi niliponawa nikaingia nyumba iliyokuwa jirani nikidhani ndio mgahawa wenyewe kumbe nimeingia kwenye geto la Mmama flani ivi.

Sasa mda naingia alikuwa bize anakula alafu kageukia upande wapili wala hakusikia vishindo mda naingia kwa akili za kitoto nilipogumdua kuwa nimeingia kusipo nikapata akili ya kutoka kimyakimya tena...! Kumbe mda natoka ndani yule mama akashtuka nikajifanya kuchomoka mule ndani kwa haraka ndio akaniitia mwizi..mwizi...mwizi asee nikajifanya kukimbia nikaishia mikononi mwa wanainchi wenye hasira kali aisee sitakaa nisahau kilichonipata yaani kuna watu bongo hii hata ukiwa unatoa maelezo hawayazingatii wao ni kupiga tu na kutafta petroli.... Hadi leo nikikuta mwizi anapigwa huwa napenda kusikiliza maelezo yake kama yanaleta logic....Maana ningechomwa moto na sijawahi kuiba wala kutapeli cha mtu!
Duuh pole sana mkuu

uliponaje huo msala?
 
Hiyo ilinitokea miaka kama sita iliyopita, Sikh hiyo nimeenda ukweni kwa Mara ya kwanza kabisa, sasa lile wenge la kuonana na babamkwe( Wakati tunafika hakuwepo,alipiga simu yupo njiani anakuja) Basi nikawa naenda chooni kukojoa.

Ile nafika chooni nakuta kuna mzigo haujasukumwa, duh palepale nikaghairi kujisaidia ile nafungua mlango nitoke uso kwa uso na babamkwe,

A see hata domo lilikuwa zito maana lazima angejua ni Mimi ndiyo nimesababisha, ile anaingia naskia anafyonya. Acha kabisaaa.
 
ilitokea nimekuja dar kwa ndugu yangu aliepanga chumba maeneo ya uswahilini temeke,nyumba ilikua na vijana na mama mwenye watoto wa kike pale,sasa ilitokea siku moja usiku nimeenda kuoga mida ya usiku nikaona sio mbaya nitoe na haja kubwa kabisa,kumbe nimemaliza kujisaidia na maji nimemwaga yalikua machache,asubuh si ndo akaja mwenye zamu kufagia choo akaukatana nayo,kila akimwagia maji mzigo hausogei mbele ikabid aulize tu ni nan alikua wa mwisho si ndo nikatajwa mm..daaahh ilikua fedhea kwa watoto wa kike wale maana mama alikazia neno 'Alf yule kaka ni mwembamba ila ana mavi magumuuuuu' sikumsalimia mpk namaliza likizo naondoka
U made my day, sio kwa kucheka huku mpk watu wananishangaaa[emoji23][emoji23][emoji23]
 
we boya sana yani unakata mikucha yako na nail cutter za mtu mwingine magonjwa yote haya.

mimi ilinikuta miaka kadhaa iliyopita ndio nimeajiriwa kwenye kampuni flani hapa dar.jioni nimekaa na mabosi zangu kupata wine kidogo na kujuana vizuri.tulikua tumeweka simu zetu mezani,bahati mbaya nikachukua simu ya bosi mmoja nikatia mfukoni nikijua ni yangu .mara kidogo jamaa akaanza kuulizi simu yake mimi nimetulia tu nikiamini iliyopo mfukoni ni yangu .Dah ilivyobipiwa ikaita kwangu halafu hata hawakunipa nafasi ya kujieleza zaidi ya kila mtu kutunza simu yake kwa umakini,nilijisikia fedheha haielezeki
Dah. Thanks for the laugh.
 
Nakumbuka 2010 nimetoka tbr nameenda biharamulo kwa bibi yangu, sasa usiku nimelala kitanda cha peke angu mkojo ukanibana haswaa kutoka nje naogopa maana ni giza sana yaan full migomba, basi nikajikaza mara usingizi ukanipitia kuja kushtuka alfajiri godoro limeloa plus nguo zangu, aisee niliona aibu ikabidi niamke mapema nikafua mashuka yote na saa moja asubuh nilipanda gari kuelekea muleba kupunguza stress kwa mama mkubwa, nadhan bibi alielewa sema alinikaushia tu
 
Nakumbuka miaka ya nyuma tulitoka kwenye kwaya jamaa mmoja akawa amekula vyakula vingi kwa kuchanganya wakati tukiwa safarini jamaa akabanwa na haja kubwa akaomba gari isimame ili ajisaidie,jamaa alikuwa amepiga bonge ya suti mbaya zaidi alikuwa mwalimu wa kwaya,,mzee baba alivyorudi akarudi amechafua koti la suti kwa pembeni na kinyesi bila yeye kujua,watu ilikuwa ni kucheka tuu [emoji23].nikamwambia jamaa umechafua koti yeye hakujua kama ni uchafu gani akashika ile kushika watu wakacheka gari zime jamaa akakunguta mkono ule mzigo ukiangukia kichwani nikikumbuka hiyo siku nachekaga wenyewe tuu.[emoji23]
 
ilitokea nimekuja dar kwa ndugu yangu aliepanga chumba maeneo ya uswahilini temeke,nyumba ilikua na vijana na mama mwenye watoto wa kike pale,sasa ilitokea siku moja usiku nimeenda kuoga mida ya usiku nikaona sio mbaya nitoe na haja kubwa kabisa,kumbe nimemaliza kujisaidia na maji nimemwaga yalikua machache,asubuh si ndo akaja mwenye zamu kufagia choo akaukatana nayo,kila akimwagia maji mzigo hausogei mbele ikabid aulize tu ni nan alikua wa mwisho si ndo nikatajwa mm..daaahh ilikua fedhea kwa watoto wa kike wale maana mama alikazia neno 'Alf yule kaka ni mwembamba ila ana mavi magumuuuuu' sikumsalimia mpk namaliza likizo naondoka
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Jitahidi kunywa maji na kula matunda mkuu [emoji23][emoji23]

Back
Top Bottom