Life style yangu ilinipotezea mwanamke mzuri

Life style yangu ilinipotezea mwanamke mzuri

Attachments

  • IMG-20240813-WA0009.jpg
    IMG-20240813-WA0009.jpg
    366 KB · Views: 17
Portion 02:

.... Kipindi yupo kidato cha nne mwanzoni, kazi zikawa zimepungua sana kule. Maana ilikuwa ni msimu wa mvua. Sikuona haja ya kuendelea kuishi kule ikiwa sitengenezi hela.

Nikamtafuta mdau, nikamuuzia ghetto langu ili niondoke kule. Nikamwambia Ester kwamba nina mpango wa kuondoka pale kijijini. Aliumia tu, ila hakuwa na namna. Siku ambayo kesho yake nilikuwa natarajia kuondoka, Ester alikuja pale ghetto na tulishinda wote siku nzima.

Wakati anataka kuondoka, akaniambia:

Ester: "Nikuambie kitu?"

Mimi: "Niambie"

Ester: "Najua wewe kama mwanaume kuna vitu siwezi kukuzuia usifanye, kama uliweza kuvifanya hapa na Mimi nikiwepo, sidhani kama ukiwa mbali utajizuia. Ila ombi langu kwako ni moja tu"

Mimi: "Ombi gani?"

Ester: "Vyovyote itakavyokuwa, naomba usibadilishe namba ya simu. Na hata ikitokea imeshindikana ukabadilisha basi naomba unitafute kwenye hii namba ya bibi (akanipa note book ndogo ikiwa na namba ya simu)"

Mimi: "Sawa usijali"

Ester: "Unaniahidi?"

Mimi: "Ndio nakuahidi"

Ester alikuwa ananipenda sana,sijui hata alinipendea nini.

Ila nilifurahia kuondoka kule, nikijua sasa hiyo ndio nafasi ya Ester kunisahau. Kwavyovyote vile umbali ungetutenganisha tu. Alafu sio kwamba Ester alikuwa mbaya, hapana. Kiuhalisia kati ya wanawake ambao Nishawahi toka nao, kwenye top 3 yupo. Shida yangu kubwa akili yangu ilikuwa imeshikwa sana na wamama, kiasi kwamba mabinti niliona wananipotezea muda.

Ndio maana siku zote kabla ya kumuomba Mungu anifungulie milango ya neema, nilikuwa namuomba anitoe kwenye huu uraibu wa wamama. Niliamini nikiweza kuwaepuka, basi mengine yote yatakaa kwenye mstari.

***** ***** ***** ****** ****** ******

Nilivyotoka kule, moja kwa moja mpaka Dar. Nikarudisha harakati zangu pale.

Mara chache chache nilikuwa nawasiliana na Ester, japo mara zingine nilikuwa nazipotezea calls zake au text. Hii yote nikumfanya anitoe akilini mwake.

Mwanzoni alilalamika lalamika, mara zote nikawa namwambia kazi nyingi nakuwa busy. Hakuamini utetezi wangu, ila hakuacha kunitafuta.

Ester: "Hivi mbona unanifanyia hivi lakini?. Hunipendi tena?"

Mimi: "Sio kwamba sikupendi, ila naamini Mimi sio mtu sahihi kwako. Natamani upate mtu atakayeweza kukufanya uwe na furaha"

Ester: "Wewe ni mtu sahihi kwangu, na ukiamua niwe na furaha unaweza. Maana kila kitu kipo ndani ya uwezo wako"


Nikaishia kumuitikia tu.

Alimaliza form four, akachaguliwa kwenda advance shule moja ya wasichana inaitwa Igowole ipo kule kule Iringa. Nilimpongeza, nikamtumia hela kama zawadi, maisha yakaendelea.

Kipindi akiwa advance, Mimi nikawa na safari ya kuelekea mkoani Iringa. Maana ni kipindi ambacho nilikuwa nimeanza dili za mkaa na yule Mzee Dingi, hivyo nilimwambia Ester kuwa nitakuwa maeneo ya Usokami. Alivyosikia hivyo alifurahi sana:

Ester: "Kweli unakuja?"

Mimi: "Ndio. Ungekuwa na nafasi tungeonana"

Ester: "Basi tukutane Mafinga, nitaomba ruhusa ya kwenda hospital"

Mimi: "Hivyo inawezekana kupata ruhusa?"

Ester: "Ndio. Wengi wanaendaga sana. Na Mimi nitaomba ruhusa"

Basi tukaweka mipango yetu hivyo. Na kweli alifanikiwa kupewa ruhusa. Mimi nilifika Mafinga usiku, yeye akaja Kesho yake asubuhi. Tulishinda wote mpaka kwenye mida ya saa nane ndio akaondoka.

Wakati tukiwa kituoni anasubiria gari ijae arudi shule, akaniambia:

Ester: "Siku sio nyingi tutakuwa wote huko Dar mpenzi"

Mimi: "Mnahamia Dar?"

Ester: "Hapana, ila chuo nitasomea Dar"

Mimi: "Jitahidi ufaulu vizuri, ndio utaweza kuwa na nafasi ya kuchagua usomee wapi chuo"

Ester: "Najua nitafaulu tu"

Tuliongea ongea pale, mpaka gari ikajaa kisha wakaondoka. Na Mimi nikaendelea na safari yangu kuelekea kijijini kucheki mkaa.

Nikiwa kule, mashine ikawa inawasha sana. Na wakati wa kukojoa kuna maumivu fulani nayapata. Ile hali ilivyozidi, ikabidi niende hospitali. Pale ndio nikaambiwa nina gono. Hii ndio ilikuwa mara ya kwanza nakutana na huu ugonjwa.

Nikataka kusema Ester kaniambukiza? Ila haraka sana akili yangu ikanikatalia. Maana dalili za kuwashwa nilikuwa nazo tokea nikiwa ndani ya bus naelekea Mafinga. Hii inaonesha ugonjwa nimesafiri nao. Hapo ndio nikamkumbuka Halima, maana ni yeye ndio wiki iliyoisha yote nilikuwa nae. Kivyovyote vile huu mzigo nimeutoa kwake.

Issue ikaja, kama Mimi ninao, basi lazima na Ester nimempa. Kama natumia dawa, basi na yeye inabidi atumie dawa. Ila nitamwambiaje?? Ikabidi zile zile dawa nilizopewa Mimi pale hospital, nimnunulie na Ester. Ila nitampaje dawa wakati haumwi? Na hajaniambia kama anaumwa, nikimtumia dawa lazima aniulize nimejuaje.

Ikabidi nitulie mpaka aniambie. Ila nikawa namjulia hali mara kwa mara ili kujua maendeleo yake. Hazikupita siku nyingi, akaniambia kuwa anatokwa na uchafu mwingi ukeni. Pale pale nikamwambia nitamtumia dawa. Nikaziagiza kwa gari. Alivyozipata akaanza kuzitumia. Hakunihoji chochote, kwamba Mimi sio daktari nawezaje kumuagizia dawa? Alipata nafuu na kupona kabisa.

Siku moja kwenye mazungumzo, nikamuuliza aliwezaje kumeza dawa bila hata kuhoji? Akanijibu "Mimi ni mkeo, naamini huwezi kunidhuru."

Nikabaki kimya kwa muda. Mara zote amekuwa akiniita Mimi mume wake, ila kwa upande wangu sikuwahi kumchukulia hivyo. Sikutaka kuendelea na hiyo mada.


********** * **** ******

Hatimae akamaliza kidato cha sita na katika waliochaguliwa kwenda jeshini jina lake lilikuwepo. Akaniuliza kama nipo tayari endapo ataamua kuja kuishi na mimi kwa ile miezi mitatu badala ya kwenda jeshini. Nikamkatalia na kumpa sababu nyingi za yeye kwenda jeshini. Mwisho wa siku akakubaliana na mtazamo wangu.

Ila ukweli ni kwamba sababu zote nilizompa hazikuwa ndio dhumuni halisi la kumtaka aende jeshini. Ambacho sikutaka ni yeye kuja ninapoishi, maana kipindi naishi Dar ghetto palikuwa na jam kama la kwenye ATM ifikapo mwisho wa mwezi. Sikupenda Ester anione vile.

Kabla hajaenda aliomba anitumie documents zake za shule ambazo angekuja kuzihitaji kwenye kuapply chuo na mkopo. Nikamwambia azitume kwenye email yangu, akafanya hivyo.

Wakati wa kwenda jeshini ulipowadia aliomba sana apitie Dar ninapoishi alafu ndio aende huko jeshini. Nikamkataa kwa mara nyingine, maana kama angekuja ungekuwa msala mwingine. Hakuwa na namna akaenda jeshini bila sisi kuonana. Niliamini akiwa jeshini lazima atakutana na mtu ambae atamfanya aachane na Mimi, hivyo yeye kwenda jeshini kwangu niliona ni ahueni.

Matokeo yalipotoka alifaulu vizuri tu, na kipindi cha kuapply vyuo kilipoanza akaniomba nimuombee maana taarifa zake nilikuwa nazo:

Mimi: "Nitajie kozi unazopenda kusoma pamoja na vyuo ili nikufanyie hiyo application"

Ester: "Chagua vyuo vyovyote vya hapo Dar. Kozi weka zinazoendana na tulivyoongeaga Kipindi kile"

Kuna chuo kimoja pale Dar wao kwa mwaka wanaweza wakawa na mabash hata 10. Yani hata wakiambiwa wameletewa mkuu wa chuo mpya, basi wataandaa bash. Niliona kile chuo ndio kitamfaa Ester, maana kivyovyote vijana wa pale hawawezi kumuacha salama. Niliamini atakuwa na furaha sana endapo atakuwa na mtu mwingine tofauti na Mimi. Sikujiona kama namfaa kabisa.

***** ***** ***** ***** ****** ****** *****

Akiwa jeshini, tuliendelea na mawasiliano kama kawaida. Wakati wanakaribia kuhitimu, akaniambia kuwa kabla ya kwenda kwao atapitia Dar kwangu akae siku kadhaa maana amenimiss.

Kipindi ananiambia hivyo, tayari nilikuwa ninaplan ya kwenda Bagamoyo na madam Nuru. Kama Ester anakuja, basi natakiwa kuhairisha hiyo safari. Na endapo nikihairisha basi nijiandae na msala toka kwa huyu shangazi.

Sikuwa na namna, ikabidi nimkatae tena Ester kwamba kuna kazi naifanya ambayo inanifanya niwe mbali na ghetto kwa muda mrefu sasa.

Ester: "Sasa nina zawadi zako ambazo sitaki kwenda nazo nyumbani. Inabidi nikupe, itakuwaje?"

Mimi: "Hapo sijui inakuwaje. Ni zawadi gani?"

Ester: "Wewe jua ni zawadi tu. Kuna rafiki zangu huku ni wakazi wa Dar, nitaongea nao nione kama kuna ninayeweza kumpa akuletee"

Mimi: "Okay sawa"

Siku ya wao kurudi ilipofika, akaniambia kuna mtu amempa. Hivyo akifika Dar atanipigia.

Na kweli, kuna muda namba ngeni ikanicheki. Kuongea nae nakuta ni mdada ambae ni rafiki wa Ester. Akaniambia yeye anakaa maeneo magomeni, hivyo akifika tukutane pale River side anikabidhi mzigo wangu kisha aendelee na safari yake. Tukakubaliana akikaribia anijulishe ili nianze kusogea.

Kweli alifanya hivyo. Nikasogea mdogo mdogo mpaka River side. Nafika pale, nakutana na Ester akiwa na rafiki yake.

Ester: "Mimi ndio zawadi yenyewe baby, najua umechukia ila ndio nishafika tayari"

Sio siri nilimind kuliko alivyofikiria. Ila sikuwa na namna, Nikaondoka nae mpaka maskani. Ujio wake ulifanya safari ya Bagamoyo ifie hewani, maana siku tatu mbele ndio nilikuwa natarajia kusafiri.

Niliplan siku ikifika kumuongopea Ester kuwa naondoka kikazi, lakini kumbe alipekuwa simu yangu na kuona Chatting zetu alafu akakausha. Siku moja kabla ya siku ya safari, ilikuwa mida ya usiku baada ya kumaliza kula akaniambia kwamba anajua sababu ya Mimi kukataa asije kwangu wakati anatoka jeshini. Kiufupi alinieleza vyote alivyosoma kwenye simu.

Akaniambia kama nitaondoka na kwenda na yule mwanamke, basi sitokaa nimuone tena kwenye maisha yangu. Maana Ile nidharau ya kiwango cha juu sana, kumuacha yeye ndani na kwenda kwa mwanamke mwingine.

Japo sikuwa na mipango yoyote ya future na Ester, ila iliniwia vigumu kuondoka na kumuacha pale ghetto, hasa baada ya kuwa ameshaujua ukweli. Kiufupi hii ilikuwa ni nafasi nzuri ya Mimi kuvunja mahusiano yetu, maana kama ningeondoka ni wazi pasingebaki chochote kati yetu. Ila sijui kwanini, nikajikuta moyo wangu unakuwa mzito.

Nikamuomba msamaha na kuahidi siondoki tena, nitabaki na yeye. Akachukua simu yangu na kumblock Madam Nuru. Hakujua kama ameblock mtaji wangu.

Kati ya mashangazi yote ambayo nishawahi kuwa nayo, hakuna aliyenifanya nikala bata kama huyu Madam. Sometime akiwa na ziara za kiofisi, alikuwa ananitanguliza Mimi huko anakoenda. Hakuwa mgumu kwenye kutoa hela. Kitendo cha Ester kuamua kumblock, ni sawa na kumblock boss wangu. Nikajua pale kibarua kimeshaota nyasi, ila sikuwa na namna.

Maana kama nisingekubali ablockiwe, Ester alikuwa tayari kuondoka usiku ule ule. Hakuwa mwenyeji Dar, hakuwa na ndugu wa karibu pia. Sikuwa na uhakika angeenda wapi.

Ila ningejua timbwili ambalo lingefatia, basi ningefikiria mara mbili kuhusu kumblock Madam
 
Portion 04.

.....Siku ya jumamosi mapema kabisa akarudi home na mizigo yake. Kisha akaenda kkoo kufata vipodozi kwa ajili ya wateja wake. Mchana akakuta tayari nimeshapika, tukala kisha mambo mengine yakaendelea. Siku ikawa nzuri kwetu.

Tulikaa kama mwezi hivi kila kitu kipo sawa. Nilikuwa najitahidi sana ku-handle mambo yangu yasije kuleta tafrani tena. Sikutaka kumdisappoint tena Ester. Lakini kuna watu wana nyota za kuharibia wenzao tu. Kuna shangazi mmoja nilikuwa nae anaitwa Tina. Huyu shangazi alikuwa anapenda sex kana kwamba ndio yupo kwenye balehe. Mashangazi wengine wote ukipiga goli zako mbili, wanalidhika. Lakini sio kwa Tina. Mpaka kuna time nikahisi labda ana mapepo. Mfano mnaweza mkawa mmetoka kusex sasa mnaenda out kurefresh, ikitokea hata akaona kavideo clip kenye viasharia vya mapenzi, atakwambia turudi ndani kidogo. Hapo jua mnaenda kusex.

Alafu huwa hajali mazingira, iwe parking, ndani ya gari au sehemu ya Cinema. Imagine ukumbi wa cinema uliokuwaga pale Tazara, tulipiga show kipindi movie inaendelea. Nakumbuka tulivyoingia ukumbini, akachagua viti vya nyuma kabisa kwenye kona. Nikawa nishajua nini kinafatia.

Sasa hiyo siku nipo zangu ghetto na Ester, Tina akapiga simu. Sikuipokea.

Akapiga tena, nikakausha. Ester akaniuliza mbona hupokei? Nikamjibu achana nae, ni msumbufu tu

Ester: "Anakusumbua na nini?"

Mimi: "Mpotezee tu asikuumize kichwa"

Ester: "Tayari ameshaniumiza kichwa, ndio maana nataka kujua. Why anapiga mfululizo hivi kama anakudai?"

Mimi: "Hatopiga tena , maana anajua huu ni muda wa kupumzika".

Ester akakubali kuachana nae, hazikupita dakika tano simu ikaita tena mpigaji bado akiwa ni Tina.

Ester akaniambia ili awe na amani basi anaomba aongee nae yeye. Wakati anaichukua simu ili apokee, ikakata. Pale pale ikaingia msg:

"Pokea simu basi, mbona unakuwa hivyo"

Ester akaamua kuchati nae, akijifanya ni Mimi:

Ester: "Unataka nini? Kwani situlikuwa wote leo?"

Tina nae akajaa akahisi anachat na Mimi kweli, maana kabla sijarudi ghetto nilikuwa kwake.

Tina: "Sawa, ila nina nyege mwenzio. Niambie nikufate wapi basi"

Ester: "Mimi nimechoka nahitaji kupumzika"

Tina: "Usinifanyie hivyo bhana. Basi hatufanyi, nakuja unisugue kisimi tu nitaridhika"

Hii msg ikamuondolea uvumilivu Ester, akaamua kumpigia simu. Walitukanana sana pale mpaka alipotosheka, akakata simu. Msala ukanirudia kwangu.

Ester hakuongea kitu chochote na Mimi, akaomba tulale.

Tukalala.

Hata palivyokucha hakutaka kabisa kuliongelea lile jambo. Akawa anaenda chuo na kurudi kama kawaida, ila baada ya wiki akakusanya nguo zake zote na kuniambia anaondoka na hatokaa arudi tena. Kwamba it is over kati yetu.

Mimi: "Usitumie hasira, tuongee kwanza"

Ester: "Tuongee nini kipya sasa? Nimeamua kwa moyo mmoja kukupa uhuru unaoutaka"

Mimi: "Huo uhuru ndio siutaki, ndio maana nataka kuishi na wewe. Naomba usiondoke hapa nyumbani"

Ester: "Naondoka kwenye maisha yako, hivyo hata hapa sistahili kuendelea kubaki"

Mimi: "Ukiondoka nitapata wakati mgumu sana, bila uwepo wako akili yangu itastack sana"

Ester: "Ita mwingine aje muishi wote, huwezi kosa mtu. Kama unapigiwa simu mpaka usiku wa manane, hatokataa ukimwambia aje hapa"

Mimi: "Hivi ni kweli umedhamiria?"

Ester: "Haya maisha ya ushindani na kuvumilia siyawezi tena. Naondoka ili uwe huru kuwasugua vizuri. Sitaki ujibane bane tena, sawa kaka msugua visimi?"

Kama masihara, Ester akawa ameondoka pale home.

***** ***** ***** ***** ***** ******

Tokea siku ile nikawa na kazi ya kumbembeleza Ester anisamehe, ila hakutaka kunielewa. Mpaka anamaliza mtihani wa mwisho, bado hakuwa amenisamehe.

Alivyomalizana na mitihani, tukakaa chini ili kujadili tena swala letu. Ila msimamo wake bado ulikuwa ni ule ule.

Ester: "Wewe ni mwanaume mzuri sana, ni mpole, mcheshi, unajali, una huruma na akili. Ila bahati mbaya kwetu ni kwamba tumekutana wakati usio sahihi. Pengine utakayekutana nae akili yako ikiwa imetulia, atafurahia sana mahusiano na wewe, ila kwa Mimi nimeshindwa"

Mimi: "Najua nimekudisappoint sana, ila nipe nafasi ya kukuonesha kwamba nabadilika. Nitakuwa vile unavyowish niwe"

Ester: "Mimi nadhani nimeshachoka tayari, hata huo muda tena wa kukupa sina. Yani kwako nahisi nilikosea njia,hakuna kitu kinachoniuma kuona watu ninaocompete nao kila siku ni wamama. Heri wangekuwa rika langu, ningesema pengine kuna sehemu siko vizuri hivyo unanitafutia mbadala. Ila wamama wamama wamama. Yawezekana ukawa una mapepo ila hujijui, hebu anza kwenda kanisani. Ikiwezekana okoka"

Mimi: "Kama nikiokoka itaweza kurudisha mahusiano yetu, nitafanya hivyo kipenzi".

Ester: "Mimi na wewe tumeshamalizana, nenda kaombewe, jirekebishe ili utengeneze mazingira mazuri kwa utakayekuja kuwa nae".

Kipindi chote cha hayo mazungumzo, nilikuwa nikimwangalia Ester, naona kabisa anamaanisha. Maana alikuwa anaongea kwa utulivu sana, hapayuki, hana jazba wala hasira. Mbaya zaidi sina cha kufanya kumshawishi.

Kikao chetu kikaishia hivyo, Ester wangu anapeperuka huku namuona. Akachukua vitu vyake vilivyokuwa vimebaki pale ghetto, akaenda Tanga kwa mama ake.

Kipindi iki ndio niliandamwa na matatizo kadha wa kadha. Hapa ndio nilianza kutafutwa na polisi au kulala kituoni kila baada ya siku mbili. Mzee KY alikuwa ananiandama na pia kuna jamaa wakikurya nae aliamua kunikosesha amani.

Ester ambae ndio alikuwa mtu wangu karibu mwenye kunipa moyo kwenye nyakati kama hizi, nae ndio hivyo alishaamua kunipiga chini.

Sikuwa na mtu wa kuongea nae.

Kuna siku mama yake Ester akawa amenipigia simu, katika maongezi ya hapa na pale akawa analaumu simtafuti tena siku hizi. Nikamwambia ndani ya ile wiki nina safari ya Tanga, nitaenda kuwatembelea. Akasema atafurahia sana, pia atapata nafasi ya kusuluhisha matatizo yangu na Ester. Nilivyosikia kauli ile, nikapata nguvu.

Ester alivyopata habari kwamba natarajia kwenda kwao, akanipigia simu:

Ester: "Mambo, nasikia umemwambia Mama kuwa utakuja"

Mimi: "Alhamisi hii nitakuwa Tanga mjini, nikimaliza shughuli zangu nitakuja kuwatembelea jumamosi au jumapili"

Ester: "Unakuja kufanya nini wakati tumeshaachana? Kwanini usiniache nikawa na amani lakini?"

Mimi: "Bado sijayakatia tamaa mahusiano yetu, natamani tuyape nafasi nyingine

Ester: "Hakuna namna naweza badili mawazo yangu. Mama yangu anakupenda sana, aliumia nilipomwambia tumeachana. Nisingependa aumie tena ukija maana sitobadili msimamo wangu "

Mimi: "Familia yako tayari inanikubali, niruhusu nirekebishe nilipokosea, kila kitu kitakuwa sawa. Najua kati yetu bado kuna upendo mkubwa sana, tusikubali kuupoteza. Mimi ni mumeo Ester"

Ester: "Upendo pekee sio sababu ya watu kuoana, Mimi na wewe tumekuwa pamoja kwa zaidi ya miaka sita. Nimevumilia sana nikiamini pengine wewe ndio mume wangu, ila ukweli ni kwamba haujawahi kunichukulia kwa namna hiyo. Mimi sio aina ya mwanamke unayetamani kujenga nae maisha. Nimekubali kujitoa, niache niendelee na maisha mengine. Mimi na wewe hatuwezi kuwa pamoja"

Mimi: "Tukiamua kwa pamoja, hakuna kitakachoshindika
na. Niruhusu nije kwenu tuongee"

Ester: "Hapa tutabishana mpaka kesho, ila hatuwezi kuelewana. Sawa njoo".

Kauli hii ilileta furaha sana kwangu, niliona nimepata ushindi nusu. Nikajipanga kwenda kuhakikisha nasolve huu msala. Ukweli ni kwamba sikuwa na ratiba za kwenda Tanga wiki hiyo, ila niliwaambia vile ili wasione nimelazimisha kwenda bali imetokea tu.

Kauli ya mwisho ya Ester kuniambia niende ilinipa matumaini sana nikiamini mahusiano yetu yanaenda kufufuliwa upya. Ila nilipofika kule ndio ikawa wazi kwangu kwamba hakuna namna ninayoweza kumrudisha Ester tena.

Alikuwa ananijua kuliko nilivyojijua Mimi mwenyewe, na aliposema mahusiano yetu hayawezi kuendelea haikuwa sababu ya hasira bali alidhamiria maana aliona vitu ambavyo Mimi sikuwa naviona.

Alikuwa anajua anachokiongea.

** ** ** *** ******

Soma next portion hapa: Life style yangu ilinipotezea mwanamke mzuri
 
Back
Top Bottom