Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
umeandaliwa mnyoosho wa Milioni tano!Portion 14:
..... Nilifikiria kila mbinu ya kuchomoka pale nikakwama. Wazo la kuufungua ule mlango ili nikakabiliane na jamaa sikutaka hata kulifikiria. Ile gypsum kwenye ceiling board sijui fundi alitumia material gani, maana haikuwa na dalili za kuharibika japo niliipiga piga sana. Kitu pekee nilichomshukuru fundi, ni mbao alizotumia kwenye ule mlango, maana pamoja na mtani kujaribu kuuvunja, ila alikwama.
Akili ikanijia nimpigie yule Hoza jamaa yangu askari, lakini nikawa nasita. Kama aliweza kunichinjia baharini kwenye ule msala wa kwanza, sembuse sasa hivi? Ila baada ya kujishauri sana, nikaamua kumpigia. Jamaa kumuelezea mazingira niliyopo, akaniambia walikuwa na gari ya doria mitaa hiyo ila wameshaamsha. Nikamsisitiza arudi, nilivyoona anajifikiria, ikabidi niahidi kumlinda. Yani Mimi nipo kwenye hatari, lakini jamaa ndio kwanza anajaribu kunegotiate hela. Ikabidi nimwambie wageuze waje, nitawalinda.
Kweli wakarudi mpaka mitaa ile, nikamuelekeza hadi wakafika nilipokuwa. Waliingia mpaka ndani, wakamtaitisha jamaa na kumuweka kwenye gari. Kisha nikatoka mle ndani, wakaniambia nikakae kwenye gari na dereva. Kwavile niliwaambia kuna watu wengine wanakuja, basi wale askari wakashauriana wasogeze gari pembeni wawasubirie na hao. Wakati naenda kuingia ndani ya gari, mtani alikuwa ananiangalia jicho la kumaanisha nafasi yoyote atakayopata, ananiua.
Akiwa kakaa kule nyuma, akawa ananiambia "Mutani umenigongea demu wangu alafu umeniitia polisi?". Nilikuwa najisikia vibaya kinoma kwa namna alivyokuwa analalamika, ila sikuwa na namna, maana kama hao aliowaita wangenikuta pale ndani, kilio kingekuwa kwangu.
Tulisubiria pale, ila wale jamaa wengine hawakutokea. Tukahisi labda waliushtukia mchezo wakapotea. Ilinitoka laki tatu usiku ule kwa ajili ya wale askari.
Yule mtani wangu wakaamsha nae, alafu wakaniambia inabidi nifanye niwezavyo nihame haraka pale. Maana yule jamaa hawawezi kukaa nae sana, na akitoka sitokuwa salama.
***** ***** ****** *****
Palivyokucha ikabidi niombe ruhusa kazini kwamba naumwa, alaf nikaitumia siku nzima kuzunguka na madalali. Baada ya kuzunguka sana, hatimaye nikapata sehemu. Nyumba niliyopata ndio ile niliyosimulia story yake kipindi kile (Fumanizi la mama mwenye nyumba). Pale Kwa mtani ikabidi nitoke, nikaacha kodi ya miezi miwili.
Kiuhalisia sikuwahi fikiria habari za kufumaniwa, na sikuwahi imagine inakuwaje. Moja kati ya kumbukumbu mbaya niliyonayo, basi ni ile siku. Na lile tukio limekuwa likiniandama sana, maana miaka inaenda lakini yule jamaa hasira zake hazijawahi kupungua. Tokea ile siku nimejitahidi sana kutulia, lakini bado kashkash haziniishi. Wanasema Binadamu sio milima, ndivyo ilivyo kwangu na yule mtani wangu. Kuna siku nipo na crew yetu kwenye gari la ofisi, nikagumiana na mtani wangu wakati tunatoka kujaza mafuta. Jamaa aliacha alichokuwa anafanya, akaanzisha timbwili sio la kitoto. Jitihada za wenzangu ndio zilipoza Soo, nikatoka salama.
Lakini pia kile kitendo cha kuiona gari ya ofisi, akawa amejua ofisi ninayofanyia. Akawa ananilia radar sana, kuna siku alishawahi kunisubiria nje, alipoona sina dalili za kutoka. Akaja hadi mapokezi kuniulizia. Nikaitwa kwamba nina mgeni wangu kwenda namkuta ni yeye kasimama na HR pamoja na mdada mmoja ambae alikuwa ni mhudumu wa ofisi yetu. Sikujiuliza mara mbili, nikatoka speed eneo lile. Namsikia HR anauliza "We Analyse mbona unamkimbia mgeni wako?". Wala sikutaka kumsikiliza au kupunguza mwendo. Japo wanasema hutakiwi kumkaidi mwajiri wako ila wawe wanaangalia na mazingira. Unajua kwa akili za mtani wangu, pale pale ofisini angeweza kunidhalilisha. So niliona ni bora nipate aibu ya kumkimbia mgeni, kuliko kupigwa mbele ya HR.
Japo hiyo siku nilifanikiwa kumtoroka, lakini aliendelea kunisumbua saa na route za ofisini plus vitisho vingi. Jamaa sijui alipewa nini na yule mwanamke aisee, maana hakuwa mke wake, na hakuwa na mpango wa kumuoa. Ilifikia hatua hadi nikawa sina raha na ile kazi tena, na hivi ilikuwa ni ya mkataba tu, nikaamua kupiga chini.
Kuacha kazi ni rahisi kuliko kupata kazi. Nilisota sana benchi, nikawa natumia akiba niliyokuwa nayo. Hela ikawa inatoka nyingi, inaingia kidogo. Kiufupi life likarudi kuwa tight.
Matukio yaliyofatia hapa, ndio kama nilivyosimulia kwenye fumanizi la Mama mwenye nyumba. Pale napo nilihama baada ya kukutana na Mwahija. Japo sikudumu nae muda mrefu, maana Dar alikuwa kaja kutembea tu. Alivyoondoka kuna kipindi nilimfata hadi kwao, yani nilifunga safari toka Dar mpaka Manyara. Yaliyotokea huko ndio yalifanya tukapotezeana mazima, japo nilitamani tungeendelea.
Huku mjini Dar, katika harakati za kuendelea kutafuta michongo ndio nikaja kukutana na Mzee Dingi. Na yeye akaniunganisha na timu yake, yaliyotokea hapo baadhi mnayafahamu maana niliyaelezea kwenye story iliyopita. (Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee)
Hapa nitaelezea yale ambayo kule sikuyaandika.
Unajua baada ya Mzee Kesho Yetu (Mzee KY) kutuachia msala alafu yeye kutembea na hela zote, kwa upande wangu niliamua kumfatilia maana nilikuwa vibaya sana kiuchumi. Japo nilimpata, ila alinikataa. Nikawa sina msaada, nilirudi kijijini kwa wazee kupumzisha akili, ila baada ya muda nikarudi tena mjini.
Maisha yalisonga, misala yote ikawa imepoa hadi nikaanza kusahau.
Kuna ndugu yetu mmoja binti yake alikuwa anaolewa. Sasa Mama yangu akawa ananiambia mara kwa mara nikaudhurie vikao, ila sikuwa naenda. Sasa kuna siku ya jumamosi usiku akanipigia simu na kunisisitizia kuwa kesho yake jumapili nifanye niwezavyo niende kwenye kikao cha hiyo send off. Nikamkubalia kama kawaida, ila sikuwa na mpango wa kwenda.
Ilivyofika kesho yake, mpaka mida ya saa nane sikuwa na ratiba yenye kueleweka, na ghetto panaboa. Nikaona ngoja niende tu kwenye hicho kikao walau nikafahamiane na ndugu zangu. Kikao kilikuwa kinafanyikia maeneo ya DDC kule survey. Wakati kikao kinaendelea, mwenyekiti akawaambia wajumbe kuwa kwenye kikao kilichopita walikubaliana MC aliyependekezwa nae audhurie kikaoni ili wamuone, lakini pia wajadiliane kuhusu gharama zake. Wakampigia simu huyo MC maana muda wote alikuwa amekaa kwenye gari yake. Huyo MC mwenyewe alivyofika, najikuta nipo uso kwa uso na Mzee KY. Moyo ukalia Pa!. Huyu Mzee ni lini ameanza kazi ya u-MC?
Na yeye alivyoniona, nikaona ameshtuka kidogo, lakini akajikausha. Mwenyekiti akamtambulisha kuwa huyu ndio MC fulani. Kisha MC akaambiwa aelezee package zake na gharama. Mzee KY akaanza kujielezea pale, alikuwa na utulivu wa hali ya juu sana kana kwamba kila kitu kipo sawa. Ule utulivu wake hata kwenye mazingira magumu kama yale ndio huwa unanipa wakati mgumu. Inakuwaje hana wasiwasi?.
Wakati yeye anaendelea kujinadi, nikaingia Instagram kulitafuta jina lake kama ambavyo mwenyekiti alimtambulisha. Nikamuona!. Jamaa anafollowers wakutosha, account imeshiba japo haina matukio mengi. Picha ikanijia hii kazi ya u-MC itakuwa ni zuga tu, au labda hana muda mrefu tokea ainze. Lakini mbona followers ni wengi kiasi hiki?. Akili ikaniambia huyu anaweza akawa kazini, lakini mbona yuko pale?. Au kuna mtu anamlenga hapa?
Kulikuwa na daftari la mahudhurio kwenye kile kikao, ikabidi niliombe. Nikapitia majina yote. Kati ya tuliokuwepo, kuna wamama watatu umri wao kidogo umeenda. Nilikadiria wanaweza kuwa kati ya late 50's au early 60's. Akili ikaniambia kama Mzee KY michezo yake ni ile ile ya kudeal na wastaafu, basi hao ndio itakuwa target yake. Kwavile majina tulikuwa tunaandika kulingana na tulivyokaa, nikawa nimeyajua majina ya wale wamama.
Nikayaandika kwenye msg alafu nikamtumia Bi Mkubwa kumuuliza kama anawajua. Mama akanipigia simu:
Mama: "Nawafahamu ndio, wamefanyaje?"
Analyse: "Tupo nao kwenye kikao hapa, najaribu kuangalia nani anaweza kunisaidia kwenye maswala ya kazi"
Mama: "Ulivyokuwa hutaki kwenda kwenye hicho kikao, ungewaona saa ngapi sasa?"
Analyse: "Ndio nishakuja sasa Mama"
Mama: "Hapo hakuna anayeweza kukusaidia, labda kidogo huyo (......) Maana alikuwa na kazi nzuri kweli, ila nadhani atakuwa ameshastaafu au anaelekea kustaafu"
Analyse: "Basi sawa Mama"
Nilivyokata simu, nikawa nishamjua ninayemtaka. Mzee KY nae baada ya kumaliza sera zake, wakajadiliana gharama alafu wakamruhusu aondoke, watamjulisha. Akaaga na kuondoka.
Kikao kilivyoisha, nikamfata yule Mama nakuongea nae. Nilimsalimia nikajitambulisha Mimi ni mtoto wa fulani, hapo ndio akanichangamkia. Nikajifanya naomba connection pale, na kwenye story ndio nikathibitisha kuwa amestaafu mwaka mmoja uliopita, maana aliniambia "Mbona mimi nimeshastaafu tayari, nasubiria mafao tu".
Akili ikaniambia huyu ndio target ya Mzee KY.
Nikamfata mwenyekiti, akanipatia namba ya MC alafu nikaondoka zangu home. Mida ya saa tatu kama na nusu hivi, nikampigia simu Mzee KY. Alivyopokea tu, kabla hata sijajitambulisha akaniwahi:
Mzee KY: "Hapa nilikuwa nasubiria simu yako, nilijua lazima ungenipigia"
Analyse: "Kama ulichukua namba yangu, kwanini hukunipigia sasa?"
Mzee KY: "Namba yako nichukue ya nini sasa?. Sikia, kesho saa kumi jioni tukutane pale pale tulipokuwa leo, usichelewe Aposto"
Alaf akakata simu.
Nikaanza kujiuliza, hivi kama hakuchukua namba yangu pale, ameitoa wapi? Au amejuaje kama ni Mimi?. Akili ikaniambia hii namba yake ni bosheni kwa ajili ya huu mchongo wake, ni watu wa kwenye kikao tu ndio wanaijua. Na kwavile wale hawakuwa na mpango wa kumpigia maana alishaelewana nao bei tayari, hivyo mtu pekee angeweza kupiga alibakia kuwa Mimi.
Nikaamua kulala.
Asubuhi niliendelea na mishe zangu, mida ya jioni nikawa eneo la tukio. Uzuri wote hatukuchelewa.
Mzee KY: "Aposto umekuwa kama luba sasa, umeniganda kuliko nilivyotarajia"
Analyse: "Sijakuganda, ni mazingira ndio yanatukutanisha"
Mzee KY: "Niambie unataka nini?"
Analyse: "Safari hii siwezi kukubali umtapeli mtu mwingine"
Mzee KY: "Ukishaona nimeanza kuonekana hadharani, basi ujue hakuna kinachoweza kulizuia ilo dili kutokea"
Analyse: "Nakuahidi ili halitotokea"
Mzee KY: "Ukiwa mwanaume usiweke ahadi ambazo huwezi kuzitimiza"
Analyse: "Nakuahidi hii nitaitimiza"
Mzee KY: "Nakuomba usiingilie ili jambo, litakugharimu pakubwa sana"
Analyse: "Nishakutana na mengi, huna cha kunitisha. Pia nitahakikisha ile tenda ya kuwa MC pia unaikosa"
Mzee KY: "Kilichonipeleka pale, kimeshakamilika. Sikwenda kwa ajili ya kuomba u-MC"
Analyse: "Kumbe ulifata nini pale?"
Mzee KY: "Ilo halikuhusu"
Nikabaki namuangalia tu. Akasimama:
Mzee KY: "Sikia Aposto, jizuie kufanya jambo lolote la kipumbavu. Mimi ni mpumbavu kuliko unavyoweza kufikiria "
Hakusubiria niongee kitu, akaondoka.
Sikujiuliza mara mbili nilivyoona ameshaingiza gari yake barabarani, nikaita boda boda, nikamfungia tela. Nilimfata mdogo mdogo, mpaka alivyo paki kwenye car wash maeneo ya magomeni. Nikamlipa yule boda, kisha nikajibana sehemu kusikilizia.
Akaacha gari pale, nadhani kwa ajili ya kuosha. Akaita bolt, akaondoka eneo lile. Na Mimi nikaita tena bodaboda, nikaendelea kumfatilia.
Kufika Morocco, wakavuka yale mataa kama wanaelekea Kawe. Ila walivyofika maeneo ya Zantel, wakakunja kushoto. Nikaendelea kuwafatilia hadi maeneo ya karibia na Kairuki, wakaenda kupaki mitaa ya nyuma kwenye nyumba moja nzuri nzuri imezungukwa na maua nje. Akaachana na ile bolt akaingia ndani, na Mimi nikamlipa bodaboda, nikaamua kuyasoma mazingira.
Kwa namna mazingira ya pale alipoingilia, ilionesha ni kama ametumia geti la nyuma. Akili ikaniambia atakuwa mwenyeji sana kwenye hii nyumba, hapa ndio patakuwa nyumbani kwake. Kwa jinsi palivyokuwa tulivu, nikaogopa kuzunguka zunguka sana maeneo yale, maana unaweza jikuta unaitiwa mwizi. Nikaamua kukaa sehemu pembeni kidogo na ile nyumba.
Lengo ilikuwa nikumuacha atulie kwanza huko ndani, ili nitakapoenda kumkurupua nimkute na familia yake, maana ingekuwa rahisi kumdhibiti. Nilikaa pale mpaka mida ya saa kumi na mbili kama na nusu hivi. Baada ya hapo nikasogea upande wa mbele mwa ile nyumba, nikagonga kengele. Geti likafunguliwa, nikataka kujielezea kwa mlinzi ila akaniambia wewe pita tu, utawakuta ndani. Kimoyo moyo nikajisemea "This is good, inabidi niongee nae huko huko ndani"
Nikapiga hatua mpaka sebleni, nakuta kuna furniture za Bei ghari sana, na utulivu uliokuwepo pale sebleni ulikuwa mkubwa sana. Wakati najiuliza kama nikae au la, akaja dada mmoja mkali sana kiasi kwamba nikajikuta natoa macho.
Dada: "Karibu boss"
Analyse: "Asante, samahani kuna mtu namuulizia"
Dada: "Wewe ndio Aposto?"
Nikashangaa yeye kuniuliza vile, lakini kabla sijasema chochote akaendelea:
Dada: "Kuna ujumbe wako hapa"
Analyse: "Ujumbe wangu? Toka wapi?"
Akanipa kikaratasi. Nikakipokea na kukisoma:
"Chagua package, ufanyiwe massage. Punguza nyege Aposto"
Nikabaki nimeshangaa, maana sikuelewa. Nikageuka kumwangalia yule dada, naye akaniuliza:
"Unataka massage ya aina gani?"
Analyse: "Massage? Kwani hapa ni sehemu ya massage?"
Hakunijibu kitu akanioneshea kibango upande wa kushoto kwangu ndipo nikatambua ile ni sehemu ya Massage. Pia ndio nikaweza kusoma hata t-shirt yake ilionesha hayo majina.
Analyse: "Mbona nje sijaona bango lolote?"
Dada: "Bango letu pale nje linafanyiwa marekebisho, tunabadilisha muonekano wake. Ila kama unalitaka, kesho litakuwepo"
Nikajikuta napatwa na hasira.
Analyse: "Sasa Mimi bango la nini?. Aliyeniachia huu ujumbe yuko wapi?"
Dada: "Aliondoka muda mfupi baada ya kuingia hapa. Akasema kuna mgeni wake utafika, ndio akaniachia huu ujumbe"
Nikageuka nakuanza kuondoka.
Dada: "Mbona unaondoka bila huduma Boss, maana alisema bill juu yake"
Kipindi yule dada ananiambia habari za massage, Mimi kichwani nawaza mwendo wa kutoka kule mpaka kufika makumbusho stand. Nikamjibu huku natoka:
Analyse: "Fanya mwenyewe hiyo massage"
Kisha nikatoka pale nikiwa na hasira sana. Kwanza ameniingiza gharama ya zile route za bodaboda, pili amenigandisha pale nje kumbe ameshaondoka. Nikajaribu kumpigia simu, hakupatikana. Nikalazimika kutembea hadi Makumbusho stand, ila njiani niliendelea kumpigia, lakini bado hakupatikana. Mpaka nafika home, bado hapatikani.
Wazo likanijia niingie Instagram kwenye account yake. Nikatengeneza account nyingine chap, alaf nikaingia kwenye page yake nakuanza kuandika shit kwenye comments. Nilikuwa naandika chochote kinachonijia, kuanzia deals alizoshawahi kuzifanya mpaka hii ya sasa. Haikuchukua muda, akafunga comments. Nikabaki na hasira nisijue cha kufanya. Nikachukua line yangu ya magumashi, nikaiweka kwenye simu na kumtumia ujumbe yule Mama mstaafu.
Kwenye msg nikampa ABC kuhusu Mzee KY, na kwamba anajiandaa kumtapeli. Msg ilivyokuwa delivery, nikatoa line kwenye simu. Nikaenda zangu kuoga walau nipoze hasira, maana nilikuwa nimefura sio mchezo. Nilivyorudisha line yangu ya kawaida kwenye simu, haikuchukua muda Mzee KY akanipigia simu:
Mzee KY: "Hivi unajua Aposto wewe ni m$enge tofauti na nilivyofikiria"
Analyse: "Utajua mwenyewe, ila safari hii ni bampa to bampa na wewe"
Mzee KY: "Hiyo bampa to pamba unayoitaka na Mimi, utaweza?"
Analyse: "Nadhani Mzee unaniangalia kwa uoga sana. Imefika hatua sasa natakiwa kukuonesha kwamba sikuletwa mjini bali nilikuja mwenyewe kwa hustle zangu"
Mzee KY: "Hizo hustle zilizokuleta mjini Mimi zimenikuta, maana nimezaliwa hapa. Na ndio hustle hizo hizo nitakufukuzisha nazo kwenye ili Jiji"
Analyse: "Hakuna mwenye uwezo wa kunifukuza kwenye ili Jiji. I'm here to stay grandpa"
Mzee KY: "Aposto ondoka , rudi haraka ulipokuwa"
Analyse: "Kwa umri wako ndio unatakiwa kuhama Jiji, Mimi ndio kwanza nimefika"
Mzee KY: "Ili dili lazima litafanikiwa. Na kabla halijakamilika nakuahidi nitatenga kiasi cha fedha kwa ajili yako Aposto"
Nilivyosikia habari za hela, kidogo jazba ikashuka. Maana nilikuwa nimepigika sana.
Analyse: "Naona umeanza kupata ufahamu Mzee, hivi ndio vitu vya kuongea. Umeniandalia kiasi gani?"
Mzee KY: "Wewe unapendekeza kiasi gani?"
Analyse: "Milioni 5 sio mbaya"
Mzee KY: "Million 5 sio mbaya! Okay sawa"
Analyse: "Niitarajie lini hiyo hela?"
Mzee KY: "Siku sio nyingi Aposto"
Hakusubiri jibu, kakata simu. Sikumjali maana najua alimind, nikabaki natafakari pale kuhusu hiyo Milioni 5. Kitu ambacho Mimi sikuelewa, kumbe alivyosema atatenga kiasi cha fedha kwa ajili yangu, hakumaanisha atanipatia hiyo hela. Alimaanisha atatenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kuninyoosha. Na pindi nilipopendekeza Milioni 5, kumbe nilikuwa nimejichagulia mnyoosho wa Milioni 5.
Na kweli alininyoosha sana yule Mzee, hakuna rangi niliyoacha kuona pale mjini.
Asikwambie mtu, million 5 ni hela nyingi sana. Inategemea unaifanyia nini....
alikufanya ukarudisha mpira kwa kipa!Yule Mzee alinifanya nikaondoka Dar bila kupenda.
ni ipi hiyoRatiba yetu inajulikana mkuu
Dah!...noma sana..... kweli majuto ni mjukuu...Akili ikaniambia huyo Mogadishu ambaye anasisitiziwa kuja, kama akifika basi shughuli imeisha, maana ilo jina haliwezi kuwa la balozi au mwenyekiti wa serikali ya mtaa.