Portion 03.
....Ester alikaa pale ghetto kwa siku tano, kisha ndio akaenda kwao Iringa.
Alipoondoka nikapitia upande wa msg za namba zilizokuwa blocked , nikakuta matusi na lawama kibao kutoka kwa Madam. Nikaamua kumu-unblock kisha nikampigia, nikakuta Mimi pia kaniblock. Nikamtafuta kwa namba yangu nyingine, ila alivyojua ni Mimi akasema nisimpigie tena kisha akanikatia simu. Nikaendelea kumtafuta, ila akawa anaonesha kukereka:
Madam: "We mtoto kwani kuna kitu chako nilichochukua mbona umeniganda hivyo?"
Mimi: "Sio hivyo mama, unajua....."
Madam: "Koma kuniita mama, kwani baba ako ashawahi kukutambulisha kwangu?
Mimi: "Ila....."
Madam: "Alafu kuwa na adabu, nimesema unikome we mtoto"
Kwa ufupi kibarua kikawa kimeota nyasi.
Na Mimi nikadhamiria kumpiga chini Ester, sikuona haja ya kuendelea nae wakati najiona kabisa simuhitaji. Sikutaka kumwambia uamuzi wangu, nikamuacha ajiongeze mwenyewe kwa jinsi mambo yatakavyokuwa yanaenda.
Nikaamua kubadilisha namba ya simu, na sikumwambia Ester. Na sikuwahi kumtafuta tena tokea hiyo siku aliyoondoka.
******* ******* **
* ***
Muda wa kwenda chuo ulifika na Ester alichaguliwa kwenda chuo kile kile nilichokuwa naombea aende. Kwavile sikuwa na mawasiliano yake, sikuweza kujua mapema kama amepata chuo kile.
Inaonekana alinitafuta sana kwenye simu bila mafanikio. Alikuja Dar akafanya michakato yote ya udahili na alipomaliza akaamua kuja kule mtaani kwangu kunitafuta.
Kutokana na ugeni wake, alipata tabu sana kufika nilipokuwa naishi. Alijaribu kuniulizia, ila bahati mbaya kwake sikuwa nafahamika sana pale mtaani hivyo hawakuweza kunitambua. Mida ya jioni nikiwa narudi zangu ghetto mdogo mdogo, nikakutana uso kwa uso na Ester akiwa anabargain bei na boda boda ili aondoke maeneo yale.
Tukabaki tumetazamana tu. Kwa aibu nikajifanya kushtuka kwa furaha, nikamfata na kumwambia nilipoteza simu na sikuwa nimeishika kichwani namba yake ya simu. Uzuri nilikuwa nimebadilisha simu, hivyo uongo nilioutumia ulipata back up. Ila akaniuliza swali moja:
Ester: "Namba ya bibi siunayo?"
Mimi: "Ile notebook nimeitafuta ila sijaiona"
Akataka kunilaumu pale, ila nikamuomba twende nyumbani kwanza.
Ester akiwa mbele yangu, sikuwa na uwezo wa kumkataa kabisa. Nilikuwa najikuta nakuwa mpole mbele yake.
Tukiwa home Ester akaamua kunitolea uvivu:
Ester: "Hivi kwanini unanifanyia kama vile sina pa kwenda?. Huna hela, huna hupendo, hujali. Unadhani ni kitu gani kinanifanya niendelee kuwa na wewe?"
Kumjibu niliona ni kama ningezidi kumchochea. Nikabaki kimya tu, sikusema mengi zaidi ya kuomba msamaha.
Ester: "Najua kitendo cha Mimi kuwa mbali na wewe ndio kimefanya unakuwa na tabia hizi, ila sasa hatupo mbali mbali tena. Nakupa wiki mbili za kuweka mambo yako sawa, baada ya hapo ntakuja tuanze kuishi wote. Nisingependa kupata disappointment ya aina yoyote toka kwako"
Ile kauli aliitoa kama masihara tu, lakini baada ya wiki mbili naona mtu kaja na mizigo yake. Akajiozesha rasmi kwangu.
********* ********* ********** *********
Mwanzoni iliniwia vigumu sana kuzoea uwepo wake. Maana ni kama alikuwa ananibana. Nikawa nashindwa kujiachia kwenye baadhi ya vitu. Ratiba zangu za kazi akawa anazijua, hivyo kukawa na ugumu kumuongopea mara kwa mara ili kulala nje.
Lakini pamoja na yote hayo, kuna mabadiliko fulani makubwa aliyaleta pale nyumbani. Nilianza kutumia hela kwa mpangilio, pia nilikuwa nakula vizuri tofauti na nilivyokuwa naishi mwenyewe. Hakuwa na kero nyingi, hivyo uwepo wake ulinipunguzia baadhi ya stress, maana nilijikuta nafurahia uwepo wake.
Nikajikuta naanza kumpa uzito ambao yeye alikuwa ananipa. Nikaanza kumuangalia kwa namna ya tofauti. Namna ambayo sikuwahi kumuangalia hapo kabla.
Kitu kingine, alikuwa na akili tofauti na wanawake wengi wa rika lake
Sometimes mishe zangu zilikuwa tight, angeweza kutumia boom lake kuboost baadhi ya mahitaji pale ghetto. Lakini nilichompendea zaidi ni kwamba alikuwa na uwezo wa kutumia hela vizuri.
Kuna siku moja tukiwa ghetto akaibua mada:
Ester: "Kuna jambo moja nimekuwa nikilifikiria kwa muda sasa"
Mimi: "Jambo gani?"
Ester: "Nataka tuanze kufanya biashara"
Mimi: "Biashara? Biashara gani?"
Ester: "Ya vipodozi"
Mimi: "Mmh kwa ratiba zetu zilivyo tutaweza?"
Ester: "Tunaweza sana, hata hivyo hatuhitaji muda mwingi"
Mimi: "Kivipi?"
Ester: "Nimeshaifatilia kwa muda kiasi, wewe nisaidie mtaji tu"
Mimi: "Mtajie kiasi gani?"
Ester: "Laki mbili inatosha kuanzia"
Mimi: "Kwavile umeiona ile laki mbili kwenye droo, ghafla umekuja na wazo linalohitaji laki mbili. Na laki mbili inawezaje kutosha kila kitu?"
Ester: "Sasa hela inakaa kwenye droo badala ya tuitumie kutafuta hela zingine. Mimi hiyo hiyo inanitosha kuanzia"
Tulijadili jadili, mwisho wa siku nikakubali kumpatia ile hela.
Mpaka kufikia kipindi iki nilikuwa na wivu sana kwa Ester kuliko kawaida. Moyo wangu ulisharidhia uwepo wake. Lakini pamoja na hayo sikuacha movements zangu na mashangazi. Sana sana nilijikuta nakuwa makini sana ili asijue.
Ester akaanza biashara yake ya vipodozi. Akawa anapost sana mitandaoni habari za vipodozi, ila hakuwa na duka wala frame. Ukihitaji anaenda kununua kkoo kisha anakupatia.
Mtaji wake ukakua kiasi kwamba ile laki mbili akairudisha kwenye droo, maana ndio ilikuwa hela yetu ya dharura. Mahitaji yake madogo madogo kama vile nauli za kwenda chuo, saluni nk alikuwa anauwezo wa kuyamudu mwenyewe. Sometimes nikikwama, alikuwa ananiboost kusimamia mahitaji ya home, hasa kipindi ambacho nakuwa nimesafiri.
Nilimchagulia kile chuo ili iwe rahisi kuchukuliwa na wanaume wengine, ila yeye baada ya kufika pale akaona fursa ambayo ikawa inatufanya maisha yetu yaende vizuri.
Kuna siku tukiwa kwenye story za hapa na pale akaniambia:
Ester: "Kodi hii itakapoisha, tuhamie sehemu nyingine"
Mimi: "Kwanini tuhame?"
Ester: "Hapa padogo, siunaonaga rafiki zako wakija wanashindwa hata kuingia ndani"
Mimi: "Sio lazima waingie ndani"
Ester: "Kinachowaletaga hapa ni kucheza hii PS4 hapa, hivyo ni lazima waingie ndani. Kama tukiwa na vyumba viwili, Mimi nitakuwa nakaa zangu chumbani nyie mnaendelea na mambo yenu sebleni"
Nikamkubalia wazo lake. Na ikawa hivyo.
Maisha yaliendelea kuwa poa sana kati yetu mpaka akaingia mwaka wa tatu.
Mpaka kufikia hapo, tayari mama yake alikuwa ananifahamu. Na wote tulikubaliana akimaliza chuo tuanze mipango ya kurasimisha mahusiano yetu.
Wakati akiwa mwaka wa tatu mwanzoni, kuna siku akafuma picha kwenye gallery ya simu yangu. Picha ambazo hazikuwa nzuri. Zile picha ziliibua ugomvi mkubwa kati yetu. Nilijaribu sana kujitetea na kumuomba msamaha, ila kutokana na record yangu, ikawa ngumu yeye kunielewa.
Akaondoka pale home.
Jioni akanitumia msg kwamba atalala hostel na pia anafanya mpango wa kupata nafasi hostel, hayupo tayari kuendelea kuishi na mimi pale home.
Kesho yake akaja kuchukua nguo, akasema atakuwa anabebwa na rafiki yake pale hostel. Nilijaribu kumbembeleza tena, ila bado hakutaka kunielewa. Akawa amehamia hostel.
Baada ya kama wiki nikaamini hasira zake zitakuwa zimepoa, nikaamua kumfata hostel ili tukaongee. Alikubali tuonane, na nilijitahidi sana kumbembeleza
Ester: "Unajua nakupenda sana na tulipotoka ni mbali, nisingependa kuona tunaishia hivi. Lakini ukweli ni kwamba haupendeki, na nimevumilia sana hata visivyovumilika".
Nilitamani kujitetea lakini nikakosa utetezi maana makosa ni mengi, na mara zote nimekuwa mtu wa kuomba msamaha tu.
Sikujua ni kitu gani niseme, ila sikuwa tayari kuachana na Ester.
Mimi: "Sijui hata niseme kitu gani unielewe ila kama kuna adhabu yoyote unayoona nastahili, wewe nipe. Ila plz sipo tayari kuona haya mahusiano yanavunjika"
Ester: "Kila ambacho umekuwa unafanya kinaonesha kwamba huyataki haya mahusiano. Ni Mimi tu ndio niliamua kujifanya kipofu".
Mimi: "Lakini....."
Ester: "Hebu nisikilize vizuri. Nipo tayari kukusamehe endapo utanihitaji kufanya hivyo. Ila kaa ukijua huu ndio utakuwa msamaha wa mwisho".
Nikamuomba msamaha, tukaweka mambo sawa. Nikamuomba achukue vitu vyake turudi home kule, akagoma:
Ester: "Acha Mimi kwanza nibaki hapa, wewe nenda kaweke mambo sawa, jumamosi ndio nitarudi"
Mimi: "Sina mambo yoyote ya kuweka sawa, sijawa sawa tangia umeondoka hivyo ninachohitaji ni wewe kurudi nyumbani Mama"
Ester: "Nakujua vizuri, na ninamaanisha ninaposema kwamba hakuna msamaha wako nitakaoukubali tena baada ya hii leo, kwahiyo fanya ninachokuambia"
Sikutaka kuendelea kumbishia asije akakwazika tukaanza upya. Ikabidi nimkubalie, nikarudi home peke yangu. Walau nilikuwa na matumaini kwamba we are okay now.
Kwani nilichukua muda basi? Haukupita muda mrefu, nikajipiga tena risasi ya mguu. Hapo ndio ikawa mwanzo wa mwisho wetu, kama masihara Ester aliamua kuondoka mazima.
***** ***** ****** ****** *******
Some next portion hapa:
Life style yangu ilinipotezea mwanamke mzuri