Portion 15.
.... Hazikupita hata siku nyingi, nikaanza kuziona dalili za ile hela niliyotengewa.
Nilikamatwa na polisi mida ya jioni siku ya jumapili nikiwa natoka uwanjani kuangalia mpira. Ilikuwa ni mida ya saa 12 hiv, sina ili wala lile, gari ya doria ikapaki mbele yangu. Sikuwa na wasiwasi wowote, ila nikashangaa nashikwa na kupakiwa ndani ya gari. Nikajaribu kuhoji, nikaishia kupigwa kofi, nikatulia.
Nilikaa kituoni mpaka jumanne nilivyokuja kutolewa na jamaa zangu niliowacheki. Ikanitoka elfu 50, japo niliachiwa ila bado sikuwa najua kosa langu. Nikachukulia simple tu. Hazikupita hata siku tatu, nikashikwa tena na polisi. Yani ndani ya miezi miwili, niliingia pale buguruni na Tabata kama mara 5 au 6. Na zote lazima hela initoke. Hii mara ya sita, ndio kuna afande wakati natoka akanichana; "Mdogo wangu, fanya mpango umalizane na yule Mzee vinginevyo kila wiki utakuwa unahudhuria hapa kituoni"
Nikajaribu kumuuliza ni Mzee gani huyo?. Ila hakutaka kuendelea kuongelea ilo swala. Baada ya kufikiria sana, akili ikaniambia atakuwa Mzee KY tu, hakuna mwingine. Nilijikuta napatwa na hasira sana. Nikajaribu kumtafuta kwenye simu, lakini hakupatikana.
Hazikupita siku mbili tokea niachiwe, nikashikwa tena. Yani ni kama vile wale askari waliambiwa kila wakinishika kuna hela wanapewa. Na kwanza sijui hata walikuwa wananipataje wale jamaa.
Walivyonishika safari hii, nikajaribu kuwapa hela ili nisifike kituoni ila wakagoma hela ndogo. Nilishazoea kila wakinishika nawaachia 20 au 30, sasa siku hiyo wakagoma kabisa kupokea 30. Mpaka tunakaribia kituoni, bado wamegoma. Walipoona kweli sina nyingine, wakaamua kuipokea kisha wakaniambia nishuke.
Wakati nimeshashuka, nikamuona Mtani wangu alikuwa anatokea upande kilipo kituo cha polisi anakuja kwangu. Tukakutanisha macho, akili ikaniambia nikimbie ila nikaipinga, maana yule jamaa kwa akili zake anaweza akaniitia mwizi. Bila kupenda ikabidi nirudi ndani ya lile gari la polisi. Wale askari wakaanza kucheka. Mtani baada ya kuona nimeingia ndani ya gari, akaamua kuondoka maana askari walikuwa wanamtolea macho waone atafanya nini.
Alivyoondoka nikataka kushuka, askari wakagoma mpaka nitoe hela. Nikajaribu kuwaambia si nimewapa 30 muda sio mrefu?. Wakaniambia ile iliisha niliposhuka, ila baada ya kuingia tena kwenye gari yao, natakiwa kulipia tena maana mle sio sehemu ya kujificha. Nilikuwa na elfu 5 ikabidi niwape hiyo.
Kushoto yupo Mzee KY, kulia yupo Mtani. Nilikuwa naishi kwa wasiwasi na stress sana kile kipindi. Hapo ndio nikaanzisha utaratibu wa kuwa naenda kushinda beach. Naenda zangu misele kutafuta michongo, alafu mida ya mchana naenda zangu beach kushangaa shangaa warembo na kupoteza muda. Nikichoka beach hii, naenda nyingine ilimradi nipoteze muda.
Niliendelea na hiyo ratiba mpaka siku ile nilivyokutana na Evervess pale Rongoni (sorry hii ndio story iliyoondelewa jukwaani)
Ile siku nilivyoachana na Evervess pale beach, siku kadhaa mbele nilishikwa tena na polisi. Nilivyoachiwa, wakati nipo ghetto mida ya jioni nikapigiwa simu na namba ngeni. Kuipokea ndio nagundua ni Evervess.
Evervess: "Dogo niaje?"
Analyse: "Fresh broh, niaje?"
Evervess: "Sasa sikia, kuna mchongo nataka nikuunganishe. Upo tayari kusafiri safiri mikoani?"
Analyse: "Niko tayari, nipe maelekezo"
Akanielekeza sehemu ya kwenda na mtu wa kwenda kuonana nae. Nilivyofika pale, ikawa ni ofisi ambayo inahusisha kusafiri sana, nikaulizwa lini nitaweza kuanza kazi. Kwa namna nilivyokuwa nimechoka na hizi mbilinge za Dar, sikujiuliza mara mbili. Nikawaambia nipo tayari muda wowote.
Nikapangiwa kuanza kazi kesho yake, na baada ya wiki nikasafiri.
Hii kazi ilinisaidia kunirudishia amani ambayo nilikuwa nimeipoteza kwa muda mrefu sasa. Sikutarajia kama Evervess angeweza kuja kuwa na umuhimu kwangu, ila baada ya kuniunganisha na hii kazi nilianza kumpa umuhimu. Kwenye trip yangu ya kwanza, nikajaribu kumpigia simu walau nimshukuru, ila namba yake haikupatikana. Na hata nilivyoendelea kujaribu, jibu nililopata ilikuwa "Hakikisha namba unayoipiga, na upige tena"
Kwa miezi miwili mfululizo, nikawa mtu wa kusafiri tu. Leo nipo mkoa huu, kesho ule. Na ikitokea nimerudi Dar, basi muda mwingi nilikuwa nazima simu au sitoki nje kabisa.
Lakini pamoja na jitihada zangu zote hizo za kujaribu kusahau my past life na ku-move on, ila my past bado iliendelea kuniandama. Kuna siku nilikutana tena na Mtani wangu, bahati.mbaya kwangu yeye ndio alianza kuniona. Alinishtukiza na ngumi ya kifua, kiasi kwamba nikawa nahisi pumzi ninayotoa ni ya moto, maana hadi pua zilikuwa zinauma. Kuna watu mapenzi wanayachukulia serious sana, huyu mtani nae ni mmoja wao. Miaka inaenda lakini jamaa bado kiwango chake cha hasira kipo vile vile. Ile siku nilikuwa nimebeba mali za ofisi pia, kutokana na ile purukushani, nikajikuta nasababisha uharibifu.
Ile hasara ofisini hawakuielewa, hivyo nikaibeba Mimi. Sijakaa sawa, polisi nao hawa hapa. Nilijaribu sana kuwapa hela, ila ni kama waliambiwa wasipokee chochote toka kwangu, nikawekwa ndani. Kipindi kule ofisini nasubiriwa ili niweze kusafiri, kumbe mwenzao nipo polisi. Baadae sana ndio wakaja kujua nilipo, wakanitoa nilivyorudi uraiani wakanipiga benchi kwa muda. Zile stress za mwanzo zikarudi tena, kushoto Mzee KY, kulia yupo Mtani.
Nikajaribu sana kumpigia Evervess, lengo ikiwa ni kuona kama anaweza kunirekebishia tena kule ofisini. Ila kila nikipiga namba yake, naambiwa haipo hewani. Kuna siku nimekaa ghetto nikiwa sina ramani yoyote, nikapigiwa na namba ngeni. Kupokea nakuta ni Evervess;
Analyse: "Niaje broh?"
Evervess: "Fresh tu, imekuwaje tena? Maana nasikia umeharibu pale ofisini".
Ikabidi nimueleze kwa urefu hali halisi ilivyo, kisha nikaomba msaada wake:
Evervess: "Sikia mdogo wangu, chochote unachofanya basi jua kitaleta matokeo mbeleni, yawe mazuri au mabaya. Yanayokutokea sasa, ni matokeo ya uliyokuwa unafanya, huna wa kumlaumu"
Analyse: "Ni kweli sina wa kumlaumu, na siwezi kumlaumu yeyote. Ninachohitaji ni msaada wa kutoka kwenye hii situation ili nianze upya"
Evervess: "Huwezi kuingia kwenye jambo, alafu utegemee wengine wakutoe. Inabidi utafute namna ya kujitoa"
Analyse: "Mpaka hapa nimeshajaribu sana, ila nimeshindwa"
Evervess: "Kila mtu ana ya kwake yanayomsumbua. Nani atakuwa busy na ya kwako?"
Nikabaki kimya;
Evervess: "Ukiweza kujitoa kwenye ili, utapata funzo. Na usipokuwa makini, utapoteza vitu vingi sana. Kwahiyo kuwa makini"
Analyse: "Ila broh...."
Evervess: "Ulitaka kazi, nikakuunganisha sehemu. Sipo kwa ajili ya kusawazisha makosa yako. Na hakuna anayeweza kuyasawazisha zaidi yako wewe mwenyewe. Tafuta namna"
Maongezi yetu yaliishia pale. Na hiyo namba haikupatikana tena. Sio baada ya siku, wiki au miezi.
Baada ya kutafakari sana, nikamkumbuka yule Mzee wa Kongowe (refer kwenye story yangu iliyopita). Nikaamua kumpigia simu, japo sikuwa na uhakika kama angeweza kufanya chochote.
Nilimpata kwenye simu, akaniambia kesho yake nimtafute ili tuweze kuonana.
***** ******* ******** ******
Kesho yake mida ya jioni tukafanikiwa kuonana. Tuliongea mambo mengi sana, na hiyo ni baada ya kumuelezea ombi la kutafuta mchongo popote pale ili mradi nisiwe idle.
Akaniuliza kama naweza ishi nje ya Dar. Jibu langu ilikuwa naweza kuishi popote pale. Mwisho wa siku akaniambia ngoja afanye mawasiliano na watu kadhaa alafu ataniambia.
Nikawa nashinda ndani kama mwali, na hata nikitoka nje basi simu naacha. Baada ya siku tatu akanicheki;
Mzee: "Uko wapi?"
Analyse: "Nyumbani tu"
Mzee: "Andaa vyeti vyako, alafu nakupa namba ya mtu unayetakiwa kwenda kuonana nae"
Akanipa namba, baada ya muda nikawa nishaonana na yule mtu. Uzuri kila kitu kilishakuwa settled na yule Mzee wa Kongowe, hivyo hapakuwa na mambo mengi. Ndani ya wiki nikajikuta nimekuwa rasmi mkazi wa Simiyu. Mazingira hayakuwa favorable, ila niliamua kuyakubali maana nilikuwa na amani lakini pia malipo yalikuwa mazuri tofauti na nilipotoka.
Nilifanya ile kazi kama mwezi mmoja na nusu, haikuwa ni kitu nilichosomea ila nilishaanza kukimudu vizuri tu, pengine kuliko hata wenye fani yao.
Nikiwa nishaanza kuzoea na kuzoeleka kule. Kuna siku yule Mzee wa Kongowe akanipigia simu:
Mzee: "Hivi si ulisomea (.........)?"
Analyse: "Ndio Mzee"
Mzee: "Kuna mtu nimeongea nae, inabidi uende ofisi fulani ukajishikize pale"
Analyse: "Mbona huku nishaanza kupazoea Mzee?"
Mzee: "Kama unataka kukua kitaaluma, inabidi ufanye kazi kwenye taaluma yako"
Analyse: "Ni kweli Mzee lakini...."
Mzee: "Sikia kijana, kwenye maisha tunapigania vitu viwili, furaha na amani. Na hakuna amani kama kufanya kitu unachopenda. Hiyo kazi leo Unaona umeizoea, ila mbeleni itakuboa hasa endapo maslahi yakipungua maana kinachokuweka hapo ni hela"
Analyse: "Lakini..."
Mzee: "Uamuzi ni wako kijana. Niambie kama upo tayari au la"
Kiuhalisia sikuwa tayari, lakini sikutaka kumpoteza huyu Mzee. Nilitamani aendelee kuwa kwenye cycle yangu siku zote. Nikajikuta namkubalia.
Ofisi aliyonipeleka safari hii mazingira yalikuwa mazuri, lakini malipo yake hayakuwa mazuri ukilinganisha na niliyokuwa napata mwanzo. Kibaya zaidi mazingira ya ule mkoa sikuwa nimeyaelewa.
Nilijikuta naenda kazini nikiwa off mood karibia kila siku. Nilifanya kazi pale miezi kama minne hivi bila kupatwa na kashkash yoyote ile. Kuna siku Mzee wa Kongowe akanipigia;
Mzee: "Unaendeleaje kijana?"
Analyse: "Salama tu Mzee"
Mzee: "Kwenye hiyo ofisi kuna nafasi za kudumu zimejitokeza. Inabidi uapply moja wapo"
Analyse: "Sawa"
Kwa msaada wa Mzee wa Kongowe, ile nafasi ya kujitolea ikageuka kuwa permanent. Nikiwa na wiki tatu tokea niwe permanent, yule Mzee wa Kongowe kuna siku akaniuliza kitu;
Mzee: "Hivi huwaga una passport?"
Analyse: "Hapana Mzee, sijawahi kuwa na kazi nayo"
Mzee: "Passport ni muhimu, hata kama huna kazi nayo. Inaweza kutumika kama kitambulisho tu"
Analyse: "Ni kweli Mzee"
Baada ya hapo tukapiga story zingine, kisha tukaagana.
Nilijifikiria fikiria kwamba kwanini yule Mzee aliniuliza vile? Baada ya kutafakari sana nikaamua kuanza kufanya application ya passport online, japo sikuwa naipa uzito. Ndani ya kama mwezi na nusu nikawa na passport yangu mkononi. Nilitumia muda mrefu kuipata, maana nilichelewa kusubmitt zile form.
Kuna siku tukiwa ofisini, pakatokea nafasi ya kuhudhuria training nje ya nchi. Process zilishaanzaga muda mrefu, ila pakatokea nafasi ya ziada hivyo akawa anahitajika mtu haraka wa kuiziba hiyo nafasi. Upendeleo ulikuwa kwa ajili ya kijana, maana ni training ambayo itahitajika kuleta faida kwenye taasisi kwa muda mrefu ujao. Tulipokuja kuulizwa vijana kama kuna mwenye passport, nikawa nayo peke yangu. Zali likaniangukia Mimi.
Nilifurahi sana, ikabidi nimpigie simu Mzee wa Kongowe kumpa hiyo taarifa. Alichoniambia ni kitu kimoja tu "Bahati inawapendelea waliojiandaa hata kama mpo wengi wenye vigezo"
Katikati ya yale maongezi akaniambia kitu. "Nimefurahi kuona upo sharp na unajua kujiongeza. Kuna mtu nitakukutanisha nae"
Nikamuitikia, alafu tukamaliza maongezi yetu.
****** ****** ****** ******
Siku ya safari nikiwa pale airport nasubiria muda wa kuboard. Nikashangaa kumuona Mzee wa Kongowe nae akiwa maeneo yale anasalimiana na watu kadhaa. Tukakutanisha macho ila hakuonesha ishara yoyote.
Baadae wakati tunajiandaa kwenda kwenye foleni, akaja nilipo tukasalimiana kisha akaendelea kuongea na watu wengine.
Wakati nikiwa kwenye foleni ikaingia msg kwenye simu, mtumaji alikuwa Mzee wa Kongowe:
"Yule mtu niliyesema nitakukutanisha nae, ndio huyo aliyesimama mbele yako. All the best"
Ikabidi nimpe umakini mtu aliyekuwa mbele yangu. Alikuwa Mzee wa makamo ambaye sikuwa namfahamu au kuwahi kumuona kabla ya hiyo siku.
Analyse: "Huyu ni nani?. Natakiwa kumwambia nini?
Mzee: "Nilisema nitakukutanisha nae, na sio kukwambia cha kumwambia. Kama unataka kunyanyuka kwenye career yako au kupiga hatua kwa namna yoyote, huyo ni mtu sahihi sana"
Analyse: "Kwahiyo nifanyeje? "
Mzee: "Safari ni ndefu hii, utakuwa na muda wa kutosha, so figure it out "
Conversations ikaishia hapo.
Tulivyoingia ndani, nikatafuta seat yangu ilipo, nikakaa. Muda kidogo, akaja abiria mwingine funzzakakaa pembeni yangu. Kumwangalia vizuri , ni yule Mzee aliyekuwa mbele yangu kwenye foleni. Kama Mzee wa Kongowe asingeniambia kwamba huyu Mzee ni muhimu na natakiwa kujenga nae ukaribu, nisingepata tabu kumuingia. Ila tayari nilishajawa na tension. Nilishaanza kumpa umuhimu japo sijajua ni kwa namna gani atakuja kunisaidia.
Tukiwa tumekakaa huku abiria wengine wanatafuta siti zao, nikaanza kujipanga namna gani namuingia huyu Mzee....