Lift ya Jengo la Millenium Towers yaanguka ikiwa na watu, kuzidisha idadi ya Watu kwatajwa kuwa chanzo

Lift ya Jengo la Millenium Towers yaanguka ikiwa na watu, kuzidisha idadi ya Watu kwatajwa kuwa chanzo

Mkuu

"Jeshi la Zimamoto limesema........ lift hiyo ambayo imefanyiwa matengenezo karibuni "

Kwa hiyo haikuwa mbovu uzito ulizidi ndiyo sababu

Mkuu,
Hiyo ni lugha ya kuficha maovu tu! Ilikuwa mbovu au haikutengemaa.ASAP

Lift zinaongea, hata yale ya kizamani bado uzito ukizidi inasema na haiondoki mpaka mpungùe!!
 
Natumaini waliokuwemo wamenusurika!
Hata mimi naomba iwe hivyo kwa kweli na pia je ilikuwa ghorofa ya ngapi?.Haina tofauti na kuanguka kwa ndege labda tofauti ya ndege moto unaweza waka.
Lift zinatakiwa kukaguliwa kila baada ya muda flani nina uhakika serikalini ndio wazembe kupindukia siajabu hiyo hela ya service watu wanaweka mfukoni.
Waige migodini wanvyofanya
 
Watu saba wamejeruhiwa baada ya 'lift' katika jengo la Millenium Tower - II, Dar es Salaam kuporomoka kutoka ghorofa ya 10.

Jeshi la Zimamoto limesema chanzo ni lift hiyo ambayo imefanyiwa matengenezo karibuni kuzidiwa uzito ambapo waliingia zaidi ya watu 10 kwa wakati mmoja.View attachment 2633244
Najaribu kupata picha ya "free fall" kutoka gorofa ya 10, ni hatari sana yaani unakiona kifo hiki hapa
 
Kuna Uwezekano Lift ilikuwa mbovu au Maintanance hazifanyiwi kwa wakati...

Ninachofahamu mimi....Lift uzito ukizidi haiwezi kuondoka... Mlango utafunga kama kawaida ila Inasimama Floor hiyo hiyo hadi Uzito upungue.. Tena hasa hizi lift za Kisasa..

Niwape pole Majeruhi..
 
Back
Top Bottom