Ligi Kuu Bara: Simba 2-2 KMC FC - Uwanja wa Mkapa, Sept 07 2022

Ligi Kuu Bara: Simba 2-2 KMC FC - Uwanja wa Mkapa, Sept 07 2022

Acha inyeshe tuone panapovuja-

Tatizo la Simba sio kocha, Kama wengi tunavyoaminishwa! Kwa mtazamo wangu tatizo la Simba ni Uongozi, hasa kipindi hiki Cha Try again na Babra.

Wanasajili wachezaji wa viwango vya kawaida Sana, nadhani wanaangalia Sana gharama kuliko ubora, Mambo yakiwa magumu zigo anaangushiwa kocha, mpaka Sasa ni kocha wa tatu huyu kuachana na timu katika uongozi wao! Mfano Try again aliahidi mwaka huu watavunja bank ili kumpata Adabayo mwisho wa Siku haikuwezekana, hivyo hivyo kwa Manzuki.

Hivi viongozi wamewezaje kufunga usajili huku kukiwa hakuna mshambuliaji no 9, na mkabaji wa chini! Unaendaje kwenye mashindano huku timu haijakamilika!

Wachezaji , Banda, Agpani, Onyango, Okwa na Mzungu wote hawa ni mapro, lakini hawana nafasi ya uhakika kikosi Cha Kwanza, hili ni tatizo, pro anakaa benchi! na wanaoanza baadhi yao viwango vyao vinatia mashaka! Matokeo yake wale tuliodhani wamechoka wanapata nafasi

Mm nashauri uongozi wangetengeneza idara ya kurungenzi ya ufundi, waajiri mtu au watu, wataalamu wa mpira ili wawe wanawashauri hasa kipindi Cha usajili! La sivyo tutakuwa tunapoteza Sana mabegi Airport.
Msimu uliopita hatukufanya vizuri! Kwa sababu hatukusajili vizuri- Kuna viashiria msimu huu pia hatujasajili vizuri,. Viongozi wajitafakali.
 
Nafasi ya Kapombe acheze Kennedy, hadi atakapopona. Nafasi ya Inonga acheze Onyango.
Quattara anarekebishika ila sio Inonga. Kashajiona staa huyo.

Mipira yote ni kurudisha nyuma tu. Goli la kwanza ni ujinga wa kurudisha nyuma mpira tena mpira wa adhabu.
Nafasi ya kapombe anacheza vizuri jimsoni mwanuke
 
Tutaingia tuu kwa kudra za Mnyazi Mungu mpira hauna wenyewe huu rafiki
Lakini hii misemo ya kudra za mwenyezi mungu nasikiaga africa tuu. Wazungu hawanaga hii misemo ila tukiingia uwanjani tunachezea vichapo tuu. Sasa ni kwamba wao mungu wao tofauti na wetu?
 
Lakini hii misemo ya kudra za mwenyezi mungu nasikiaga africa tuu. Wazungu hawanaga hii misemo ila tukiingia uwanjani tunachezea vichapo tuu. Sasa ni kwamba wao mungu wao tofauti na wetu?
Waafrica tuna mizaha sana
 
Simba ina kazi bado msimu huu, hasa kujenga kikosi imara
 
makoloooo 😂😂
Screenshot_20220906-175447_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom