Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hongera zako julio na mwadui..FULL TIME : Simba SC 0 - 1 Mwadui FC
KADI NYEKUNDU Ajib analambwa kadi nyekundu baada ya kumrukia kwa makusudi Kabunda
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 90, Mgosi anaingia vizuri na kutoa krosi nzuri lakini Mobby anaokoa vizuri kabisa
SUB Dk 89, Salim Khamisi anaingia kuchukua nafasi ya Sabato kwa upande wa Mwadui
KADI Dk 86 Majegwa analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Mnyate
SUB Dk 85, Simba wanamtoa Kiiza na nafasi yake inachukuliwa na Mussa Hassan Mgosi
Dk 81 hadi 84 Mwadui wanaonekana kuuthibiti zaidi mpira hasa katika eneo lao huku wakijaza wachezaji wengi zaidi katika ukabaji
Dk 80, Majegwa anapiga krosi nyingine lakini inaishia kwa mabeki wa Mwadui
Dk 77, Simba wanapoteza nafasi baada ya shuti la Ndemla kutoka nje sentimeta chache
Dk 76, Mrope anaingia vizuri na kupiga mrosi kwa Mnyate, naye anatelezesha kichwa lakini mpira unawahiwa na mabeki Mwadui wanaokoa
GOOOOOOOOOOOOO Dk 73 Jamal Mnyate anawachambua mabeki wa Simba kama karanga na kupiga shuti la kifundi kabisa pembeni mwa lango.
SUB Dk 69, Mwadui wanamtoa Mandawa na nafasi yake inachukuliwa na Julius Mrope
DK 67, Mandawa anaruka na kutuliza vizuri kabisa lakini anakosa balansi na Simba wanauchukua kwa ulaini kabisa
Dk 65, Kiiza anaruka na kupiga kichwa cha kuchupa, mpira unatoka nje
Dk 64, Majegwa anapiga krosi nzuri kabisa, lakini Kiiza anaanguka mwenyewe
Dk 60, inachongwa kona safi kabisa Majabvi anaunganisha lakini mpira mkuubwaaaaa
Dk 58, Majwega anapiga kona, inakuwa kona tena. Anapiga nyingine, hii ni hovyo kabisa
Dk 56, Simba wanafanya shambulizi jingine lakini mabeki wa Mwadui wanaonekana wako makini mipira ya juu
Dk 52 Kiiza anunganisha mpira wa kichwa lakini mpira unamgonga na kutoka nje
Dk 49 Mandawa anajaribu shuti kali lakini linatoka nje. Hata hivyo mwamuzi msaidizi anasema ilikuwa offside
Dk 46 kipindi cha pili kimeanza, Mwadui FC wanaonekana kumiliki zaidi mpira lakini wanacheza chini, yaani upande wa lango lao
MAPUMZIKO
DAKIKA 3+ ZA NYONGEZA
Dk 44, krosi safi ya Mwadui, lakini mabeki Simba wanapambana kuokoa
Dk 41, Mwadui FC wanapata kona, inachongwa na Luhende lakini kipa anadaka kwa ulaini kabisa
Dk 40, Mandawa anaachia bunduki hapa, lakini kipa Agbani anafanya kazi ya ziada kuokoa
KADI Dk 40, Kazimoto analambwa kadi ya njano kwa kucheza madhambi
Dk 39, Kiiza anapoteza nafasi kubwa zaid ya Simba hadi sasa. Beki anaanguka, anabaki yeye na kipa, pamoja na kwamba anamuona Mobby anakwenda kulinda lango, yeye anapiga tu hivyohivyo, beki huyo anaokoa kwa ulaini kabisa
Dk 36 hadi 38, mpira zaidi mpira unahamia katikati kila timu ikigonga pasi nyingi
Dk 35, Simba wanapoteza nafasi nyingine, Ugando anaingia vizuri lakini anakuwa hana mawasiliano na wnzake baada ya kupiga krosi inayokosa mtu
Dk 33, Mnyate anapata mpira mzuri karibu na lango la Simba, lakini anapiga shuti dhaifu ambalo halijalenga lango
Dk 30, Nimuboma anapiga krosi nzuri lakini Mwadui wanaokoa na kuwa kona isiyo na faida
Dk 29, krosi nzuri ya Tshabalala, Kiiza anaunganisha lakini anapaisha
Dk 28, shambulizi jingine kali la Simba, Kiiza anapiga krosi nzuri. Ndemla anaunganisha lakini kipa anaokoa, beki naye anaosha
Dk 25, Mandawa tena anapoteza nafasi nyingne kwa kupiga shuti na kupaisha juu
DK 24, Ndemla anaingia vizuri na kujaribu kwa mguu wa kushoto, shuti ni kubwa lakini halijalenga lango
Dk 21, Mwadui wanapoteza nafasi nzuri baada ya krosi nzuri ya Mnyate lakini Mandawa anafanya uzembe na kupaisha puuuuu
SUB Dk 19, Kado anatolewa baada ya kuumia. Nafasi yake inachukuliwa na Jackson Abdulrazak
Dk 15, krosi safi kabisa na Nimuboma, Kiiza ajaribu kuiwahi lakini Kado anaruka vizuri na kuokoa vizuri kabisa
Dk 13, Beki Juuko Murshid anamtwanga kiwiko Kelvin Sabato, yuko chini anagaragara. Bahati nzuri kwake waamuzi hawakuona. Hakika si kitu kizuri sana katika mchezo wa soka
Dk 10, Beki Iddy Mobby anaokoa mpira unaoonekana kama ulivuka msitari lakini mwamuzi anasema laaa! Haukuwa umevuka
Dk 9, krosi safi ya kwanza kwa Mwadui FC, lakini anaruka na kushindwa kupiga vizuri
Dk 6 hadi 8 Mwadui FC wanaonekana kumiliki mpira vizuri kuliko Simba
Dk 5, Mwalyanzi anaingia vizuri, anagongwa na kuanguka. Mwamuzi anasema twende...
Dk 3, Simba nao wanaonekana kuchangamka na kugongena vizuri hadi lango mwa MWadui. Bado hakuna hatari kubw ahadi sasa
Dk 1 Mechi imeanza kwa kasi kidogo na Mwadui FC wakionekana kuwa kasi wakigongeana vizuri na kuwapa presha Simba
*************************************
FULL TIME : Simba Sc 0 - 1 Mwadui FC
Jamal Mnyate 73' Mins ( Mwadui FC)
Hongera zako julio na mwadui..
Ndio hivyo mifupa wanagombea wengine nyama tumechukua sie.Yanga sasa hii sifa. Mechi wacheze wengine nyie mtangazwe mabingwa?
Hii picha imetoka vizuri mpigaji alitulia.
Basi Yanga SC watakuwa wana pesa nyingi sana ....Yaani Yanga kwa kununua mechi...hata jana kwa Waangola walinunua.
Mkuu, hapo umeua kabisa. Julio mtu wao!
Hamna lolote!, Yanga inabebwa Tu!, bila kubebwa Yanga haina lolote, acheni kubebwa, kwa mfano Leo Yanga imebebwa kuwa bingwa!. "Na SIMBA lakini!".Ndio hivyo mifupa wanagombea wengine nyama tumechukua sie.
Wewe mtu una maskhara ya ukweli ujue wanaumia sana.Hamna lolote!, Yanga inabebwa Tu!, bila kubebwa Yanga haina lolote, acheni kubwa, kwa mfano Leo Yanga imebebwa kuwa bingwa!. "Na SIMBA lakini!".
Chama langu SIMBA SC IMEKUMBWA NA NINI JAMANI....MBONA MWATUTENDA HIVI MASHABIKI WENU......???
Kipi tumewakosea......kwani Aveva lazima wewe ubaki kuwa kiongozi si ujiuzuru tu.......huoni aibu jinsi timu inavyofanya vibaya........lini wana SIMBA TUTAPANDA NDEGE....???
ZIHURUMIE NYOYO ZETU AVEVA....AU MPAKA TUKUSOMEE ALBADIR.....
UTAMU MCHUNGU KWA SIMBA SC
Azam FC imeifunga kwa Kagera Sugar kwa mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Ushindi huo unairejesha Azam FC katika nafasi ya pili ya Ligi Kuu Bara baada ya Simba kupoteza kwa kuchapwa bao 1-0 na Mwadui FC, leo. Kwani Azam FC imefikisha 70 baada ya kucheza mechi 28 na Simba inaendelea kubaki na pointi 68 ikiwa na mechi 27. Tayari bingwa wa Bara ameishapatikana ambaye ni Yanga na sasa itakuwa ni vita ya Azam na Simba kuwania nafasi ya pili ambayo ni kama heshima tu au wingi wa fedha kutoka Vodacom.