Ligi Kuu Bara: Simba SC vs Mwadui FC

Ligi Kuu Bara: Simba SC vs Mwadui FC

FULL TIME : Simba SC 0 - 1 Mwadui FC

KADI NYEKUNDU Ajib analambwa kadi nyekundu baada ya kumrukia kwa makusudi Kabunda

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA

Dk 90, Mgosi anaingia vizuri na kutoa krosi nzuri lakini Mobby anaokoa vizuri kabisa

SUB Dk 89, Salim Khamisi anaingia kuchukua nafasi ya Sabato kwa upande wa Mwadui

KADI Dk 86 Majegwa analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Mnyate

SUB Dk 85, Simba wanamtoa Kiiza na nafasi yake inachukuliwa na Mussa Hassan Mgosi

Dk 81 hadi 84 Mwadui wanaonekana kuuthibiti zaidi mpira hasa katika eneo lao huku wakijaza wachezaji wengi zaidi katika ukabaji

Dk 80, Majegwa anapiga krosi nyingine lakini inaishia kwa mabeki wa Mwadui

Dk 77, Simba wanapoteza nafasi baada ya shuti la Ndemla kutoka nje sentimeta chache

Dk 76, Mrope anaingia vizuri na kupiga mrosi kwa Mnyate, naye anatelezesha kichwa lakini mpira unawahiwa na mabeki Mwadui wanaokoa

GOOOOOOOOOOOOO Dk 73 Jamal Mnyate anawachambua mabeki wa Simba kama karanga na kupiga shuti la kifundi kabisa pembeni mwa lango.

SUB Dk 69, Mwadui wanamtoa Mandawa na nafasi yake inachukuliwa na Julius Mrope

DK 67, Mandawa anaruka na kutuliza vizuri kabisa lakini anakosa balansi na Simba wanauchukua kwa ulaini kabisa

Dk 65, Kiiza anaruka na kupiga kichwa cha kuchupa, mpira unatoka nje

Dk 64, Majegwa anapiga krosi nzuri kabisa, lakini Kiiza anaanguka mwenyewe

Dk 60, inachongwa kona safi kabisa Majabvi anaunganisha lakini mpira mkuubwaaaaa

Dk 58, Majwega anapiga kona, inakuwa kona tena. Anapiga nyingine, hii ni hovyo kabisa

Dk 56, Simba wanafanya shambulizi jingine lakini mabeki wa Mwadui wanaonekana wako makini mipira ya juu

Dk 52 Kiiza anunganisha mpira wa kichwa lakini mpira unamgonga na kutoka nje

Dk 49 Mandawa anajaribu shuti kali lakini linatoka nje. Hata hivyo mwamuzi msaidizi anasema ilikuwa offside

Dk 46 kipindi cha pili kimeanza, Mwadui FC wanaonekana kumiliki zaidi mpira lakini wanacheza chini, yaani upande wa lango lao

MAPUMZIKO

DAKIKA 3+ ZA NYONGEZA

Dk 44, krosi safi ya Mwadui, lakini mabeki Simba wanapambana kuokoa

Dk 41, Mwadui FC wanapata kona, inachongwa na Luhende lakini kipa anadaka kwa ulaini kabisa

Dk 40, Mandawa anaachia bunduki hapa, lakini kipa Agbani anafanya kazi ya ziada kuokoa

KADI Dk 40, Kazimoto analambwa kadi ya njano kwa kucheza madhambi

Dk 39, Kiiza anapoteza nafasi kubwa zaid ya Simba hadi sasa. Beki anaanguka, anabaki yeye na kipa, pamoja na kwamba anamuona Mobby anakwenda kulinda lango, yeye anapiga tu hivyohivyo, beki huyo anaokoa kwa ulaini kabisa

Dk 36 hadi 38, mpira zaidi mpira unahamia katikati kila timu ikigonga pasi nyingi

Dk 35, Simba wanapoteza nafasi nyingine, Ugando anaingia vizuri lakini anakuwa hana mawasiliano na wnzake baada ya kupiga krosi inayokosa mtu

Dk 33, Mnyate anapata mpira mzuri karibu na lango la Simba, lakini anapiga shuti dhaifu ambalo halijalenga lango

Dk 30, Nimuboma anapiga krosi nzuri lakini Mwadui wanaokoa na kuwa kona isiyo na faida

Dk 29, krosi nzuri ya Tshabalala, Kiiza anaunganisha lakini anapaisha

Dk 28, shambulizi jingine kali la Simba, Kiiza anapiga krosi nzuri. Ndemla anaunganisha lakini kipa anaokoa, beki naye anaosha

Dk 25, Mandawa tena anapoteza nafasi nyingne kwa kupiga shuti na kupaisha juu

DK 24, Ndemla anaingia vizuri na kujaribu kwa mguu wa kushoto, shuti ni kubwa lakini halijalenga lango

Dk 21, Mwadui wanapoteza nafasi nzuri baada ya krosi nzuri ya Mnyate lakini Mandawa anafanya uzembe na kupaisha puuuuu

SUB Dk 19, Kado anatolewa baada ya kuumia. Nafasi yake inachukuliwa na Jackson Abdulrazak

Dk 15, krosi safi kabisa na Nimuboma, Kiiza ajaribu kuiwahi lakini Kado anaruka vizuri na kuokoa vizuri kabisa

Dk 13, Beki Juuko Murshid anamtwanga kiwiko Kelvin Sabato, yuko chini anagaragara. Bahati nzuri kwake waamuzi hawakuona. Hakika si kitu kizuri sana katika mchezo wa soka

Dk 10, Beki Iddy Mobby anaokoa mpira unaoonekana kama ulivuka msitari lakini mwamuzi anasema laaa! Haukuwa umevuka

Dk 9, krosi safi ya kwanza kwa Mwadui FC, lakini anaruka na kushindwa kupiga vizuri

Dk 6 hadi 8 Mwadui FC wanaonekana kumiliki mpira vizuri kuliko Simba

Dk 5, Mwalyanzi anaingia vizuri, anagongwa na kuanguka. Mwamuzi anasema twende...

Dk 3, Simba nao wanaonekana kuchangamka na kugongena vizuri hadi lango mwa MWadui. Bado hakuna hatari kubw ahadi sasa

Dk 1 Mechi imeanza kwa kasi kidogo na Mwadui FC wakionekana kuwa kasi wakigongeana vizuri na kuwapa presha Simba
*************************************
FULL TIME : Simba Sc 0 - 1 Mwadui FC

Jamal Mnyate 73' Mins ( Mwadui FC)
Hongera zako julio na mwadui..
 
Hongera zako julio na mwadui..

Karibu sana ndetichia Tulikumiss sana ukipotea wewe na Azam habari zake humu zinapotea. Tumepokea pongezi zako. Na kwa kuwa umeonyesha nidhamu tutawafunga kombe la shirikisho then kwa Hisani ya watu wa jangwani tutawatuma mkashiriki kombe la
Shirikisho kwa niaba ya wababe wenu
 
Ndio hivyo mifupa wanagombea wengine nyama tumechukua sie.
Hamna lolote!, Yanga inabebwa Tu!, bila kubebwa Yanga haina lolote, acheni kubebwa, kwa mfano Leo Yanga imebebwa kuwa bingwa!. "Na SIMBA lakini!".
 
Bora kuwa wa kimataifa,kuliko mchangani
Simba huyu kabakia kufa,anakula jalalani
Mjomba hiyeeee
Mjomba mlipofungwa na coastal,mkasema haijawauma sana kwani hao ni waarabu wa tanga
Mlipopigwa na toto mlisema imewauma sana kwani hao ni watoto wa hasimu wenu yanga
Mjomba football is a performance na sio historia
Ooh tuliwafunga 5 mpaka wazirudishe
Unaishia kushangilia historia
Huku kwetu tuna methali Mjomba
Msiba hauji peke yake
Haya sasa musoti anadai chake
Hamjakaa sawa Julio huyo
Mjomba akija mo
Mpe akunusuru vinginevyo utaendelea kuwa wa mchangani mjomba natania tu ilaaaa.
 
Chama langu SIMBA SC IMEKUMBWA NA NINI JAMANI....MBONA MWATUTENDA HIVI MASHABIKI WENU......???
Kipi tumewakosea......kwani Aveva lazima wewe ubaki kuwa kiongozi si ujiuzuru tu.......huoni aibu jinsi timu inavyofanya vibaya........lini wana SIMBA TUTAPANDA NDEGE....???

ZIHURUMIE NYOYO ZETU AVEVA....AU MPAKA TUKUSOMEE ALBADIR.....


Heheeeeeeee!!!!!!!!!!!!
Mambo bado mtani, mtalia na kusaga meno.

Tunajisikia raha tu!!!!!!!

Yebo!!!!! twende kazi mtani wangu.
 
Sasa simba wameamua ubingwa watupe tuu
Daaaah!!!
 
PAKA LA MSIMBAZI FC LINAONA AIBU

6afd73182f5e6fcc1dc56a17dfd9c665.jpg
 
MBWEMBWE ZA JULIO (PART 1)





Kocha Mkuu wa MWadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema ana kikosi bora kabisa ambacho hakiwezi kulinganishwa na kile cha Simba.
Mwadui FC watakuwa wageni wa Simba katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.
Julio anasema atashangazwa sana kama wao watapoteza mechi dhidi ya Simba hii leo.
“Kweli mechi itakuwa na ushinda, huenda inaweza ikawa ngumu. Lakini nitashangazwa sana kama nitafungwa na Simba.

“Nasema hivyo kwa kuwa nina kikosi bora kabisa ambacho huwezi ukakilinganisha na Simba. Tunachotakiwa ni kupambana na kushinda na hilo liko wazi,” alisema Julio aliyewahi kuwa beki wa kati wa Simba, kocha msaidizi na kocha mkuu.
 
MBWEMBWE ZA JULIO (PART 2)


Kocha Mkuu wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amejingaza kuwa kocha bora wa Tanzania.
Julio amesema hayo mara tu baada ya mechi kati yao dhidi ya Simba kwisha na Mwadui FC kushinda kwa bao 1-0.
“Mimi ndiye kocha bora hapa Tanzania. Nilitaka sana kuifunga Simba ili kuwaonyeshea kuwa mimi ninaweza kuwafunga kwa kuwa nina uwezo.
“Hawa Simba walitufukuza mimi na kocha Kibadeni, hii ni laana yetu kwa kuwa nilianza kumfunga kocha wao wa zamani (Patrick Liewig wa Stand United). Leo nimewafunga tena leo kupitia kocha wao sijui nani, sijui Mayanja.
“Nataka wajue makocha wazalendo pia wanapaswa kuthaminiwa. Waache mambo yao ya kizamani kuwa wanaona makocha wazalendo hawana maana. Waache majungu, waache kutudharau,” alisema Julio akionyesha kujiamini.

KIkosi cha Mwadui kilionyesha soka safi na kuizidi Simba ambayo licha ya kucheza vizuri lakini ilishindwa kuonyesha kuwa ingeifunga Mwadui FC.
 
UTAMU MCHUNGU KWA SIMBA SC



Azam FC imeifunga kwa Kagera Sugar kwa mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Ushindi huo unairejesha Azam FC katika nafasi ya pili ya Ligi Kuu Bara baada ya Simba kupoteza kwa kuchapwa bao 1-0 na Mwadui FC, leo. Kwani Azam FC imefikisha 70 baada ya kucheza mechi 28 na Simba inaendelea kubaki na pointi 68 ikiwa na mechi 27. Tayari bingwa wa Bara ameishapatikana ambaye ni Yanga na sasa itakuwa ni vita ya Azam na Simba kuwania nafasi ya pili ambayo ni kama heshima tu au wingi wa fedha kutoka Vodacom.
 
" ikifika May niulizeni , nawahakikishia Simba
SC kubeba vikombe vyote vya ligi kuu na FA.
Tumejipanga vyema "
Haji Manara
February
 
...yaondoke yale matapeli kwanza ndio tuanze kutengeneza timu,majitu yanayopiga panga mpk mishahara ya wachezaji!,bila yale matapeli kuondoka,tutaendelea kusindikiza wengine tu!
 
UTAMU MCHUNGU KWA SIMBA SC



Azam FC imeifunga kwa Kagera Sugar kwa mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Ushindi huo unairejesha Azam FC katika nafasi ya pili ya Ligi Kuu Bara baada ya Simba kupoteza kwa kuchapwa bao 1-0 na Mwadui FC, leo. Kwani Azam FC imefikisha 70 baada ya kucheza mechi 28 na Simba inaendelea kubaki na pointi 68 ikiwa na mechi 27. Tayari bingwa wa Bara ameishapatikana ambaye ni Yanga na sasa itakuwa ni vita ya Azam na Simba kuwania nafasi ya pili ambayo ni kama heshima tu au wingi wa fedha kutoka Vodacom.

Umedesa kwa Saleh Jembe blog.
Kakosea.
Azam INA 60 sasa hivi na sio 70. Na mikia wana 58, sio 68.
 
Back
Top Bottom