Mabeki wa Yanga wamezoea kupambana na washambulia wasio na akili wa timu nyingine za ligi kuu, sasa wakikutana na fowadi zenye kutumia akili kama za Simba lazima mtu apigwe chenga za maudhi ili kumtoa mchezoni. Akitoka mchezoni na zile kelele za mashabiki lazima atacheza rafu na kuzawadiwa kadi ya njano, sasa hapo ndipo utaipenda fowadi wa Simba maana njia itakuwa ni kupitia kwa yule yule mwenye kadi ili kumtafutia nyekundu. Twite ni tambara tu kwa mtoto Messi, Yondani alikuwa anageuzwa na Okwi kama mume anavyomgeuza mkewe usiku ili ale kitu roho inapenda. Canavaro alibaki kumtolea mimacho refa tu kila wakati.
Bahati nzuri kwake kocha PLUIJM aliwahi kumtoa Mrwanda ilikuwa kadi nyekundu zitoke 2 hapo jana na ndipo tungeanza karamu yetu kama ile ya mwaka 2012. Na mwaka huu tulipanga ziwe 7-0.