Ligi Kuu Bara: Simba vs Yanga, 08 Machi 2015

Ligi Kuu Bara: Simba vs Yanga, 08 Machi 2015

Kutabiri inakuwa ngumu maana nasikia wapiga ramli huko Tanzania wanakamatwa
 
Naamin salum abu telela na Dilunga wangeweza kucheza na Mkude zaidi ya twite
 
Habari wakuu,
Baada ya wiki ndefu kisoka, Azam kutoka baada ya kutupa matumaini, kudumisha tamaduni ya vilabu kongwe kuondoa makocha, matatizo ya tiketi mpaka wizara kupindua maamuzi, suala la ratiba na mengineyo. Leo ni mtanange ambao huwa unafuatiliwa na watanzania wengi kuliko mechi zote, kiujumla ni mechi yenye historia bila kujali mtani yupo wapi katika nafasi ya ligi, kumfunga mtani rahaaaa.


Simba anaingia kwenye mechi ya leo akiwa na kumbukumbu nzuri ya kushinda goli tano , kushinda mechi ya leo kutaamaanisha kupunguza uwazi uliopo kati yake na kinara wa ligi na kufufua matumaini japo Yanga ameshika mechi moja mkononi.


Kwa upande wa Yanga, amekaa kileleni kwa utofauti wa point 4, angependa zege lake liongezwe kutegemea matokeo ya mpinzani ama libaki lakini lisipungue pia apate furaha ya kumfunga mtani.


Tuwe pamoja kuona kinachojiri uwanja wa taifa, Simba atachezewa sharubu ama ndala zitaenda.....
 
muda si mrefu barabara kuingia national stadium kutokea keko itafungwa hapo karibia na chang'ombe demonstration secondary . hivyo watumiaji wa barabara hiyo watafute another alternative. hali ni shwari. tunasubiri game. let the best team win.

Yes....let the best team win...
 
Naona Ivo Mapunda analeta ngonjera za kizamani.
 
Taulo la Ivo limezua mzozo kabla ya mpira kuanza
 
Ni Shidaaaaaaaa
 

Attachments

  • 1425820184325.jpg
    1425820184325.jpg
    80.9 KB · Views: 320
Back
Top Bottom