Ligi Kuu Bara: Simba vs Yanga, 08 Machi 2015

Ligi Kuu Bara: Simba vs Yanga, 08 Machi 2015

Japo Simba tumeshinda ila tumempoteza shabiki wetu mmoja,ni mtu naemfahamu na ni doctor kwa wale wanaoishi Magomeni Makanya kuna ka-hospital kapo hapa Popobawa ndipo aliakifanyia shughuli zake,wakati wa tukio sikuwa nae habari nimezipata kutoka kwa watu waliokuwa karibu,goli lilipofungwa alinyanyuka kushangilia but hakurudi kukaa akaishia kuanguka.nimesikitika sana hata raha ya ushindi imenitoka.rip dk Masako.

Poleni sana
 
ImageUploadedByJamiiForums1425842373.032793.jpg
Shabiki wao alichoka sana kulia,,,hahahah sasa hivi anawacheka KANDAMBILI cc😡Ngarna
 
Kweli watani mna furaha mpaka imepitiliza mnatoa na lugha za ajabu kisa kumfunga yanga leo,
aya leo kwenu kesho kwetu.

Kilichonifurahisha pamoja na kuwaziba mdomo ni pasi 28 za mfululizo bila kupoteza mpira za kumalizia mechi. Simba walicheza kwa kujiamini sana tofauti na timu zingine za Bongo ambazo huwa ni butua butua tu dakika za lala salama.
 
Bado Naongoza Ligi... Tena nimempita Simba sports club points Nne (4) Nikiwa na Mchezo mmoja mkononi.
 
Kweli sikio la kufa halisikii dawa na siku ya kufa nyani mti yoteee huteleza........ Kikowapi kile Jerry Muro alichokuwa akikiongea kama msemaji wa Yanga??? ..... ni dhahiri kwamba alikuwa anabwabwaja na hajui anachokiongea kibaya zaidi hajui kwamba hajui ........ Yanga chaliiiiiiiiiiiiiii hongera sana MNYAMA

Kufungwa kunauma sana. Umetoka nyumbani na confidence ya ushindi halafu unafungwa? Aisee ndio maana yanga wanazimia sana
 
Sasa umekuja kivingine baada ya kutahayari. Hatuna haja na ubingwa usio na hela sisi tumemtaka mke wetu na tumempata. Kombe la ndondo tumewaachia wadogo zetu Azam. Na kwa taarifa yenu leo mdogo wetu ameshinda.
Kama haitoshi mimba kadi nyekundu ya taahira kiziwi lenu lisilosikia filimbi Niyonzima litawagharimu mechi mbili zijazo.

Lazima mpoteane tu.

Inapendeza kuona mnashiriki Ligi ili kumfunga Yanga...!

Haya Bhana, ubingwa wenu mshachukua... Tuachieni sisi tikanyanyue ndoo.!
 
Ha ha haaaaaa Masuke mimi mtoto mwema kabisa, ban mods wakinipa watanionea tu, japo niliiomba mwenyewe.
Tumetaka nanyi mikia mfurahie angalau, maana bila hivyo wakina Aveva wangekuwa kwenye hali mbaya sana.

Week inayoisha hii nilikuwa busy sana tu, leo tena uwanjani nikala za uso, zaidi refa kanichefua sana na yellow card zake double double.
Ile red kwa Ninyonzima ndio akanikata maini kabisa, baada ya muda nikajitokea zangu maana km zege lilishalala lile.

Usijali....

Acha tuongoze ligi na mwisho wa siku tuchukue kombe letu.

Wao hapo wameshamaliza ligi.... Si unajua kwamba wanashiriki ligi ili kumfunga Yanga tu.!!!!
 
Last edited by a moderator:
mki mlaumu refa mtakuwa mnakosea kama refa angekuwa makini basi niyonzima, cannavaro, Mrwanda wangepewa red card...wachezaji Wa yanga walikuwa na jaziba ..

Jabali lao canavaro hakutakiwa kuendelea kwa kumsukuma refa wakati ana kadi ya njano tayari! Mrwanda sina la kusema maana hata kocha wa yanga alitambua ingekuja nyingine!
 
Back
Top Bottom