mjingamimi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2015
- 42,209
- 51,004
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna Wacongo wengn sinza wanasuka nywele mbona hajaja kuwasalimiaKwani kuna tatizo kusalimiana na WACONGO wenzie?
Kwa hiyo leo habari ni za ZAHERA tu. Aiseeee.Anaanzaje kwa mfano yeye na ndugu zake ndo hawajiamini, kaacha vyura wake wanaogelea vumbi yeye bize na AS vita huyu za hela wenu zinamtosha kweli mtani?
Wacha kuteswa na Zahera Mtani.Kuna Wacongo wengn sinza wanasuka nywele mbona hajaja kuwasalimia
Sent using Jamii Forums mobile app
Acha kuishushia hadhi HABARI, simba ndo habari ya mji kwa sasa zahela anakuwaje habariKwa hiyo leo habari ni za ZAHERA tu. Aiseeee.
Nawaona tu kila anayechangia hapa habari ni Zahera.Acha kuishushia hadhi HABARI, simba ndo habari ya mji kwa sasa zahela anakuwaje habari
Zahera ni nani hivi mtaniNawaona tu kila anayechangia hapa habari ni Zahera.
[emoji28][emoji28][emoji28] Poleni sana sababu Zahera kawafanya hamjiamini hata kidogo.
Karibuni kwa live updates kwenye mchezo huu wa leo
View attachment 1046968
View attachment 1046970
Mpira umeshaaanza hapa...
Dakika ya 2’ Yanga wameanza kwa kasi hapa lakin Paul Nonga anautoa mpira nje pale
Dakika ya 4’ Yanga wanaenda mbele pale..Kaseke anamuona Shishimbi ila inakuwa ni offside... Lipuli Fc bado hawajatulia
Dakika ya 5 kwenda ya 6 . Kamusoko anaona na Kamusoko pale kwa Feisal... Shishimbi anakwenda palee... aaah kipa anaawahi pale kudaka mpira ule
Dakika ya 8’ Paul Ngalema anarusha mpira unamfikia miraji athuman.. anamimina majaro inamkuta Paul Nonga... inakuwa nini pale...offsidee
Dakika ya 12’ Klaus Kindoki anapiga mpira unamkuta Makambo , makambo kwa Kaseke... Kaseke anampasia Ngassa.. Ngassa anawekwa chini na Zawadi Mauya... inakuwa ni faulo... Faulo inapigwa lakini inakuwa ni goal kick
Dakika 14’ Mrisho ngasa anaingia kwenye box la lipuli pale lakini anazuiwa pale.. ilikuwa hatari sana pale
Dakika ya 16’ Papy Shishimbi, Kamusoko na Makambo wanaonana vizuri pale kwa kufanya shambulizi hatari ila mwamuzi wa pembeni ananyoosha kibendera pale... inakuwa offside
Dakika 19’ Lipuli FC wanapata faulo... inapigwa pale... Gooooooal
Haruna shamte
Lipuli 1- Yanga 0
Dakika ya 21’ Yanga wanapata Faulo inapigwa kule na Kamusoko mabeki wa Lipuli wanaiokoa pale...
kipa wa Lipuli fc na H. Makambo wapo chini pale, ilikuwa patashika nguo kuchanika
Dakika ya 23’ Feisal Toto anachezewa faulo na Wiliam Lucian... kadi ya njano kwa wiliam Lucian.... Kamusoko anapiga Faulo pale kuelekea Lipuli Fc.. inakataliwa kwa kichwa na Haruna Shamte
Dakika ya 26, Yanga wanaonana vizuri Pale. Deus kaseke anaingiza cross pale lakini inatolewa inakuwa ni Kona... Kona inapigwa pale.. inakuwa ni piga nikupige Feisal toto anapiga pale lakini kipa wa Lipuli anaidaka
Dakika ya 28.. Paul Godfrey anampasia Kaseke. Kaseke anautoa nje inakuwa ni wa kurushwa pale
Dakika 31’ Yondani kwake Kaseke. Wiliam Lucian anamzuia Kaseke... anapasiwa Paul Nonga inakuwa ni offside... Yanga wanaanza Fasta inamkuta Makambo ila inatolewa nje
Mabadiliko kwa Lipuli
Darwesh sarboko nje anaingia steven Silvester
Dakika ya 35 sasa
Feisal Toto anaoneshwa kadi kwa kuanzisha mpira bila amri ya refa.. Faulo yanga inapigwa Kamusoko anapiga shuti la kima cha mbuzi mpira unakuwa mrefu unatoka nje... Goal kick
Dakika ya 38’ Yanga wanaonana pale kupitia Said Makapu.. wananyang,’anywa ila Lipuli Fc wanautoa mpira nje wakidhibitiwa na Yondani Kelvin
Dakika 39’ Gadiel Michael anamuona Makambo kwa mbele ila inakuwa ni offside.. namna gani pale
Bado bao ni 1 kwa Lipuli na Sifuri kwa Yanga
Mohamed Yusuf kipa wa Lipuli anaanza mpira fasta unapigwa mbeeele ila kipa wa Yanga anauwahi
Dakika 42 Paul Nonga anampasia Steven silvester ila anautoa nje kule inakuwa Goal kick
Klaus kindoki anatibiwa mkono wake wa kushoto ulioumia palee
Makambo anamuona Ngassa anakataliwa pale na mabeki wa Lipuli... Shishimbi anaukimbilia ila anazuiwa na Paul Nonga kwake Miraji Athuman anapiga shuti reefu linatoka nje
Wakati wowote mpira utakuwa halftime
Dakika 45.. Halftime Lipuli 1 - Yanga 0
————————————————————————————————————————————
karibuni tuanze kipindi cha pili hapa Bado matokeo ni Lipuli 1 na 0 kwa Yanga
mpira umeanza, Kamusoko anampasia Makambo.. amakambo anachezewa faulo, Kamusoko anpiga faulo ndefu , Yusuf Mohamed anaudaka
Dakika ya 48’ Shishimbi anawekwa chini, refa anapeta mpira unatoka nje kule
Golikipa wa Lipuli inaonekana anapoteza muda pale
Dakika ya 50’ Makambo H. anakosa goli pale.. alikosa umakini kidogo pale aisee mshambuliaji machachari huyu wa Yanga
Dakika ya 52’ kuna mzozo umetokea kule.. wachezaji wa Yanga na Lipuli wanatunishiana misuli... refa anawaamua pale
Zawadi mauya anaoneshwa kadi ya njano
Wakati huohuo Kamusoko anatoka anaingia Amisi Tambwe
Dakika 54’ Klaus Kindoki anapiga mpira mrefu kwa Makambo, unatoka nje kule... Paul ngalema anampasia Paul nonga,,, Gadiel michael anakataa
Yanga wanakosa nafasi ya wazi kupitia Deus Kaseke pale.. anapiga shuti dhaifu linadakwa na yusuf mohamed
Feisal toto anamuona Gadiel michael kwake Yondani kwa Makapu... anapasiwa Makambo.. Paul ngalema anaokoa mpira ule
dakika ya 59 kwenda 60 (Lipuli fc 1- Yanga 0)
Paul Godfrey wa Yanga anachezewa faulo... Fei Toto anapiga faulo, Ngassa anaupiga ndani ila inatoka nje..
Wakati huo wachezaji wawili kipa na beki wapo chini wakisubiri matibabu baada ya kugongana wakiokoa hatari ile ya mrisho ngassa
Dakika 65’ Deus Kaseke anaoneshwa kadi ya njano pale kwa kucheza faulo
Lipuli wanapata faulo, wanapiga ila inatoka nje... Goal kick
Dakika 66’ Makambo H. Anapasiwa mpira na Mrisho ngassa anashindwa kuucontrol unatoka nje pale
Dakika 67’ Kelvin Yondan anamuona makambo lakini Lipuli wanazuia
Dakika ya 68 ‘ Lipuli wanapata kona wanapiga ndeefu ila inaokolewa inaenda kwa Shishimbi..
Dakika 70’ bado Lipuli 1 - Yanga 0
Yanga wanaonana pale katikati Feisal toto anapasi mbele kule Lipuli Fc wanautoa nje
Dakika ya 73’ Mchezaji wa Lipuli Zawadi Mauya yupo chini baada ya faulo ya Makapu Said.. Lipuli wanaanza faulo ila Paul Nonga anamchezea vibaya Klaus Kindoki..Yanga wanaanza
Dakika 75
Deus Kaseke anaingiza majalo kule langoni mwa Lipuli ila unaokolewa... Yanga wanajitahidi pale kusogelea lango ili wasawazishe..
Zawadi Mauya wa Lipuli anatolewa nje baada ya kupata dhoruba pale
Yanga wanajipanga sasa... Ngassa anamuona Makambo..Feisal toto.. papy Shishimbi pale lakini inakuwa Offside
Sent using Jamii Forums mobile app from my iPhone 5s
😅😅😅 ZAHERA ZAHERA ZAHERA 💃💃
Mkuu upoNi
Nimependa unavyouelezea mtanange huu, kila la heri Lipuli FC
Mridhike na ya wawakilishi wa Tanzania usikuHata hatutaki Mtani.
Mpira una matokeo matatu siku zote. Hivyo hakuna cha ajabu ata.
Hata hatutaki Mtani.
Mpira una matokeo matatu siku zote. Hivyo hakuna cha ajabu ata.
[emoji23][emoji23]anafaa kuwa kwenye wimbo wenu[emoji28][emoji28][emoji28] ZAHERA ZAHERA ZAHERA [emoji126][emoji126]