Ligi Kuu Tanzania Bara: Lipuli FC vs Yanga SC Kutoka dimba la Samora Iringa Machi 16-2019

Ligi Kuu Tanzania Bara: Lipuli FC vs Yanga SC Kutoka dimba la Samora Iringa Machi 16-2019

Ni
Karibuni kwa live updates kwenye mchezo huu wa leo


View attachment 1046968

View attachment 1046970
Mpira umeshaaanza hapa...


Dakika ya 2’ Yanga wameanza kwa kasi hapa lakin Paul Nonga anautoa mpira nje pale

Dakika ya 4’ Yanga wanaenda mbele pale..Kaseke anamuona Shishimbi ila inakuwa ni offside... Lipuli Fc bado hawajatulia

Dakika ya 5 kwenda ya 6 . Kamusoko anaona na Kamusoko pale kwa Feisal... Shishimbi anakwenda palee... aaah kipa anaawahi pale kudaka mpira ule

Dakika ya 8’ Paul Ngalema anarusha mpira unamfikia miraji athuman.. anamimina majaro inamkuta Paul Nonga... inakuwa nini pale...offsidee


Dakika ya 12’ Klaus Kindoki anapiga mpira unamkuta Makambo , makambo kwa Kaseke... Kaseke anampasia Ngassa.. Ngassa anawekwa chini na Zawadi Mauya... inakuwa ni faulo... Faulo inapigwa lakini inakuwa ni goal kick

Dakika 14’ Mrisho ngasa anaingia kwenye box la lipuli pale lakini anazuiwa pale.. ilikuwa hatari sana pale

Dakika ya 16’ Papy Shishimbi, Kamusoko na Makambo wanaonana vizuri pale kwa kufanya shambulizi hatari ila mwamuzi wa pembeni ananyoosha kibendera pale... inakuwa offside

Dakika 19’ Lipuli FC wanapata faulo... inapigwa pale... Gooooooal
Haruna shamte
Lipuli 1- Yanga 0

Dakika ya 21’ Yanga wanapata Faulo inapigwa kule na Kamusoko mabeki wa Lipuli wanaiokoa pale...

kipa wa Lipuli fc na H. Makambo wapo chini pale, ilikuwa patashika nguo kuchanika

Dakika ya 23’ Feisal Toto anachezewa faulo na Wiliam Lucian... kadi ya njano kwa wiliam Lucian.... Kamusoko anapiga Faulo pale kuelekea Lipuli Fc.. inakataliwa kwa kichwa na Haruna Shamte

Dakika ya 26, Yanga wanaonana vizuri Pale. Deus kaseke anaingiza cross pale lakini inatolewa inakuwa ni Kona... Kona inapigwa pale.. inakuwa ni piga nikupige Feisal toto anapiga pale lakini kipa wa Lipuli anaidaka

Dakika ya 28.. Paul Godfrey anampasia Kaseke. Kaseke anautoa nje inakuwa ni wa kurushwa pale

Dakika 31’ Yondani kwake Kaseke. Wiliam Lucian anamzuia Kaseke... anapasiwa Paul Nonga inakuwa ni offside... Yanga wanaanza Fasta inamkuta Makambo ila inatolewa nje

Mabadiliko kwa Lipuli
Darwesh sarboko nje anaingia steven Silvester
Dakika ya 35 sasa
Feisal Toto anaoneshwa kadi kwa kuanzisha mpira bila amri ya refa.. Faulo yanga inapigwa Kamusoko anapiga shuti la kima cha mbuzi mpira unakuwa mrefu unatoka nje... Goal kick


Dakika ya 38’ Yanga wanaonana pale kupitia Said Makapu.. wananyang,’anywa ila Lipuli Fc wanautoa mpira nje wakidhibitiwa na Yondani Kelvin

Dakika 39’ Gadiel Michael anamuona Makambo kwa mbele ila inakuwa ni offside.. namna gani pale

Bado bao ni 1 kwa Lipuli na Sifuri kwa Yanga


Mohamed Yusuf kipa wa Lipuli anaanza mpira fasta unapigwa mbeeele ila kipa wa Yanga anauwahi

Dakika 42 Paul Nonga anampasia Steven silvester ila anautoa nje kule inakuwa Goal kick

Klaus kindoki anatibiwa mkono wake wa kushoto ulioumia palee


Makambo anamuona Ngassa anakataliwa pale na mabeki wa Lipuli... Shishimbi anaukimbilia ila anazuiwa na Paul Nonga kwake Miraji Athuman anapiga shuti reefu linatoka nje


Wakati wowote mpira utakuwa halftime

Dakika 45.. Halftime Lipuli 1 - Yanga 0

————————————————————————————————————————————


karibuni tuanze kipindi cha pili hapa Bado matokeo ni Lipuli 1 na 0 kwa Yanga

mpira umeanza, Kamusoko anampasia Makambo.. amakambo anachezewa faulo, Kamusoko anpiga faulo ndefu , Yusuf Mohamed anaudaka

Dakika ya 48’ Shishimbi anawekwa chini, refa anapeta mpira unatoka nje kule

Golikipa wa Lipuli inaonekana anapoteza muda pale

Dakika ya 50’ Makambo H. anakosa goli pale.. alikosa umakini kidogo pale aisee mshambuliaji machachari huyu wa Yanga


Dakika ya 52’ kuna mzozo umetokea kule.. wachezaji wa Yanga na Lipuli wanatunishiana misuli... refa anawaamua pale

Zawadi mauya anaoneshwa kadi ya njano

Wakati huohuo Kamusoko anatoka anaingia Amisi Tambwe

Dakika 54’ Klaus Kindoki anapiga mpira mrefu kwa Makambo, unatoka nje kule... Paul ngalema anampasia Paul nonga,,, Gadiel michael anakataa


Yanga wanakosa nafasi ya wazi kupitia Deus Kaseke pale.. anapiga shuti dhaifu linadakwa na yusuf mohamed

Feisal toto anamuona Gadiel michael kwake Yondani kwa Makapu... anapasiwa Makambo.. Paul ngalema anaokoa mpira ule

dakika ya 59 kwenda 60 (Lipuli fc 1- Yanga 0)
Paul Godfrey wa Yanga anachezewa faulo... Fei Toto anapiga faulo, Ngassa anaupiga ndani ila inatoka nje..

Wakati huo wachezaji wawili kipa na beki wapo chini wakisubiri matibabu baada ya kugongana wakiokoa hatari ile ya mrisho ngassa

Dakika 65’ Deus Kaseke anaoneshwa kadi ya njano pale kwa kucheza faulo

Lipuli wanapata faulo, wanapiga ila inatoka nje... Goal kick


Dakika 66’ Makambo H. Anapasiwa mpira na Mrisho ngassa anashindwa kuucontrol unatoka nje pale

Dakika 67’ Kelvin Yondan anamuona makambo lakini Lipuli wanazuia

Dakika ya 68 ‘ Lipuli wanapata kona wanapiga ndeefu ila inaokolewa inaenda kwa Shishimbi..

Dakika 70’ bado Lipuli 1 - Yanga 0

Yanga wanaonana pale katikati Feisal toto anapasi mbele kule Lipuli Fc wanautoa nje


Dakika ya 73’ Mchezaji wa Lipuli Zawadi Mauya yupo chini baada ya faulo ya Makapu Said.. Lipuli wanaanza faulo ila Paul Nonga anamchezea vibaya Klaus Kindoki..Yanga wanaanza


Dakika 75
Deus Kaseke anaingiza majalo kule langoni mwa Lipuli ila unaokolewa... Yanga wanajitahidi pale kusogelea lango ili wasawazishe..

Zawadi Mauya wa Lipuli anatolewa nje baada ya kupata dhoruba pale


Yanga wanajipanga sasa... Ngassa anamuona Makambo..Feisal toto.. papy Shishimbi pale lakini inakuwa Offside






Sent using Jamii Forums mobile app from my iPhone 5s

Nimependa unavyouelezea mtanange huu, kila la heri Lipuli FC
 
Ni Jambo la aibu sana taifa kuwa na bingwa kama ýanga, hawa jamaa mpira hawajui aisee
 
Back
Top Bottom